Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC, MONUSCO Bintou Kieta amelaani mashambulizi yaliyofanyika katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini humo.
Taarifa kutoka DRC inasema mashambulizi hayo yalifanywa na kundi la waasi la M23 dhidi ya wanajeshi wa Kongo na walinda amani wa Umoja wa Mataifa.
Kufuatia shambulio hilo, operesheni ya pamoja ilianzishwa ili kukomboa eneo hilo kutoka kwa M23, na kutekeleza lengo la kipaumbele la Umoja wa Mataifa ambalo ni kuwalinda raia.
Bi. Keita ameeleza sikitishwa na kitendo cha uhamisho mpya wa watu kutokana na mapigano haya na ametoa wito kwa M23 kusitisha mara moja uhasama wote na kushusha silaha bila masharti.
Tayari kuna tathmini inayofanyika ili kubaini athari za mashambulizi haya, pamoja na mahitaji ya kibinadamu.