Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Virusi vya Monkeypox vinakaribia vile vya surua.

UNAIDS yaonya hatari ya unyanyapaa juu ya ugonjwa wa Monkeypox

© CDC/Cynthia S. Goldsmith
Virusi vya Monkeypox vinakaribia vile vya surua.

UNAIDS yaonya hatari ya unyanyapaa juu ya ugonjwa wa Monkeypox

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa lakutokomeza UKIMWI UNAIDS limeelezea wasiwasi wake kwamba baadhi ya ripoti na maoni yanayotolewa kwa umma juu ya Monkeypox yanatoa lugha na taswira za chuki,ubaguzi na unyanyapaa hasa kwa wa Afrika na watu wanaishiriki mapenzi ya jinsia moja LGBTI 

“Unyanyapaa na kutupia lawama hudhoofisha uaminifu na uwezo wa kushughulika ipasavyo wakati wa milipuko kama hii,” ameisema Matthew Kavanagh, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNAID. 

Taarifa iliyotolewa leo na shirika hilo imeeleza kwa uzoefu wao kutokana na kushughulika na masuala ya UKIMWI inaonesha kuwa unyanyapaa na lawama zinazoelekezwa kwa baadhi ya makundi ya watu zinaweza kudhoofisha mwitikio wa jamii kuhusu mlipuko kwa haraka kama wa ugonjwa wa Monkeypox uliotangazwa kusambaa barani ulaya. 

“Uzoefu unaonesha kuwa matamshi ya unyanyapaa yanaweza kulemaza haraka majibu yanayotegemea ushahidi kwa kuchochea mizunguko ya hofu, kuwafukuza watu Kwenda kupata huduma za afya, kuzuia juhudi za kutambua kesi mpya, na kuhimiza hatua zisizofaa na za kuadhibu.”

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwengini WHO ugonjwa wa Monkeypox umeenea barani ulaya na wengi waliogundulika kuwa nao ni jamii za watu wanaoshirika mapenzi ya jinsia moja hata hivyo UNAIDS imeshukuru jamii hizo kwakuwa wawazi na kutoa taarifa. 

“Tangu Mei 13, 2022, mlipuko wa Monkeypox umeripotiwa katika nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambapo kesi haziripotiwi kwa kawaida, na kufikia Mei 21, WHO lilipokea ripoti za kesi 92 zilizothibitishwa na maabara na kesi 28 zinazoshukiwa kutoka kwa Mataifa 12 Wanachama ambao hawakuwa na ugonjwa huo. Sehemu kubwa ya visa hivyo vimetambuliwa miongoni mwa wapenzi wa jinsia moja, watu wa jinsia mbili na wanaume wengine wanaofanya mapenzi na wanaume, huku visa vingine vikitambuliwa kupitia kliniki za afya ya ngono.

Usambaaji wa kijiografia wa kesi zilizothibitishwa na zinazoshukiwa za tumbili katika zisizo za kawaida kati ya 13 hadi 21 Mei 2022.
WHO
Usambaaji wa kijiografia wa kesi zilizothibitishwa na zinazoshukiwa za tumbili katika zisizo za kawaida kati ya 13 hadi 21 Mei 2022.

Uchunguzi unaendelea. WHO inabainisha kuwa ushahidi uliopo unaonyesha kwamba walio katika hatari zaidi ni wale ambao wamegusana kimwili na mtu aliye na Monkeypox  hata hivyo hatari hiyo haiko tu kwa wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao”
Nikutokana na sababu hiyo ndio maanaa UNAIDS inahimiza vyombo vya habari, serikali, na jamii kw aujumla kuhakikisha wanatoa taarofa kwa kwa msingi wa haki, kuwa na mtazamo wa ushahidi unaoepuka unyanyapaa.

“Mlipuko huu unaonesha hitaji la haraka la viongozi kuimarisha uzuiaji wa janga, ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo wenye nguvu unaoongozwa na jamii na miundombinu ya haki za binadamu ili kusaidia kupata matokeo madhubuti na yasiyo ya unyanyapaa kwa milipuko,” alibainisha Dk. Kavanagh na kuongeza kuwa “Unyanyapaa unaumiza kila mtu, dunia iliyo na mshikamano wa kijamii husaidia kila mtu.”

UNAIDS inahimiza vyombo vyote vya habari vinaripoti ugonjwa wa Monkeypox kufuata miongozo ya inayotolewa na WHO.