Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Usambaaji wa kijiografia wa kesi zilizothibitishwa na zinazoshukiwa za tumbili katika zisizo za kawaida kati ya 13 hadi 21 Mei 2022.

Wagonjwa wa Monkeypox wafikia 92 kutoka nchi 12

WHO
Usambaaji wa kijiografia wa kesi zilizothibitishwa na zinazoshukiwa za tumbili katika zisizo za kawaida kati ya 13 hadi 21 Mei 2022.

Wagonjwa wa Monkeypox wafikia 92 kutoka nchi 12

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limetoa taarifa za kuendelea kusambaa kwa ugonjwa wa Monkeypox na sasa imefikia katika nchi 12 ikiwa ni ongezeko la nchi 8 zilizotangazwa hapo awali.


Mpaka kufikia tarehe 21 Mei, saa 13:00, jumla ya kesi 92 zilithibitishwa kimaabara, na kesi 28 zinazokuwa zimeshukiwa za monkeypox huku uchunguzi ukiendelea,zimeripotiwa kwa WHO. Hakuna vifo vinavyohusiana vilivyoripotiwa hadi leo.
Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imeeleza lengo la utoaji wa taarifa ni kujulisha umma juu la mlipuko wa Ugonjwa huo na kuongeza uhamasishaji, kufahamisha utayari, na kuhakikisha kuna juhudi za kukabiliana pamoja na kutoa mwongozo wa kiufundi kwa ajili ya kuchukua hatua zinazopendekezwa mara moja.

WHO imesema tangu tarehe 13 Mei 2022, visa vya ugonjwa wa Monkeypox vilivyoripotiwa kwa kwa shirika hilo ni kutoka Mataifa 12 Wanachama ambayo si kawaida kuwa na virusi vya monkeypox.

Uchunguzi wa magonjwa ya mlipuko unaendelea, hata hivyo, kesi zilizoripotiwa kufikia sasa hazina uhusiano na safari za kwenda katika maeneo yanayojulikana kuwa na ugonjwa huo ambayo ni nchi za Afrika Magharibi na Kati na kwamba taarifa zilizopo kwa sasa zimebainisha kesi zimetambuliwa hasa miongoni mwa wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao ambao walienda kufata huduma katika kliniki za afya ya ngono.

Jadwali la WHO lenye kuonesha nchi na idadi ya wagonjwa  

country    confirmed      Suspect 
Australia    1-5                 -
Belgium    1-5                 1-5
Canada     1-5                11-20
France    1-5                    -
Germany     1-5                   -
Italy     1-5                           -
Netherlands    1-5                -
Portugal     21-30                   -
Spain     21-30                       6-10
Sweden     1-5                           -
United Kingdom    21-30             -
United States of America 1-5        -
Total     92                                      28
        

Kesi za wagonjwa wa monkeypox kama ziliripotiwa kwa WHO kati ya tarehe 13 hadi 21 Mei 2022 saa 13:00.
WHO
Kesi za wagonjwa wa monkeypox kama ziliripotiwa kwa WHO kati ya tarehe 13 hadi 21 Mei 2022 saa 13:00.