Watu milioni 59.1 walikuwa wakimbizi wa ndani mwaka 2021: IOM Ripoti 

19 Mei 2022

Ripoti mpya iliyotolewa leo na kituo cha kimataifa cha kufuatilia watu wanaotawanywa cha IDMCA ambacho ni sehemu ya shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM inasema watu milioni 59.1 walikuwa wakimbizi wa ndani mwaka 2021.  

Kwa mujinbu wa ripoti hiyo ya kimataifa “Kuhusu wakimbizi wa ndani GRID” idadi hiyo ni ongezreko la watu milioni ya watu waliotawanywa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2021 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2020. 

Ripoti inasema kwa miaka 15 iliyopita, majanga yamesababisha watu wengi kuhama makazi yao, huku idadi ya kila mwaka ikiwa juu zaidi kuliko ile inayohusiana na migogoro na vurugu.  

Changamoto inaendelea  

Mwaka 2021 haukuwa tofauti kwani kulikuwa na wakimbizi wa ndani milioni 23.7, hasa katika Asia-Pasifiki, na ni kutokana na matukio yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi ikiwa ni pamoja na mafuriko, dhoruba na vimbunga.  

Kwa athari zinazotarajiwa za mabadiliko ya tabianchi na bila kuchukua hatua kabambe ya mabadiliko hayo ya tabianchi, ripoti inasema idadi hiyo itaongezeka katika miaka ijayo.. 

Kwa mujibu wa ripoti mizozo na ghasia vimesababisha watu milioni 14.4 kuhama makazi yao mwaka 2021, likiwa ni ongezeko la karibu asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka uliopita.  

Idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani walitokea barani Afrika, haswa nchini Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, huku ghasia na mzozo wa Afghanistan na Myanmar pia uikisababisha idadi isiyo ya kawaida ya watu kutawanywa. 

Katibu Mkuu Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumzia sula hilo katika jukwaa la kimataifa kuhusu uhamiaji amesema "Uhamiaji ni hali halisi ya maisha kwa kweli, ni wa zamani kama yalivyo maisha yenyewe ya mwanadamu. Lakini mara nyingi, imekuwa umekuwa ukichukuliwa vibaya, haujaratibiwa, kutoeleweka, na kudhalilishwa.” 

Ameongeza kuwa leo hii, zaidi ya asilimia 80 ya wahamiaji duniani wanahama baina ya nchi na nchi kwa njia salama na yenye utaratibu.  

“Lakini uhamiaji usiodhibitiwa eneo katili la wasafirishaji haramu unaendelea kusababisha gharama mbaya. Ni lazima tufanye juhudi zaidi ili kuvunja ngome ya wasafirishaji haramu wa binadamu na kuwalinda vyema wahamiaji walio katika mazingira hatarishi, hususan wanawake na wasichana. Maelfu ya wahamiaji bado hufa kila mwaka wakifuata kile ambacho sisi sote tunafuata fursa, utu na maisha bora.” 

Guterres amehitimisha taarifa yake akisisitiza kwamba “Ni lazima tufanye jitihada zaidi kuzuia upotevu wa maisha kama wajibu wetu wa kibinadamu na wajibu wa kimaadili na kisheria."  

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter