Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mimi ni mwanamke, mkimbizi, na hivi ndivyo nilivyo: IOM

Siku ya kimataifa kupinga chuki dhidi ya wageni, waliobadili jinsia  na chuki dhidi ya wanofanya mapenzi na jinsia tofauti imeadhimishwa makao makuu ya UNHCR, Geneva
© UNHCR/Susan Hopper
Siku ya kimataifa kupinga chuki dhidi ya wageni, waliobadili jinsia na chuki dhidi ya wanofanya mapenzi na jinsia tofauti imeadhimishwa makao makuu ya UNHCR, Geneva

Mimi ni mwanamke, mkimbizi, na hivi ndivyo nilivyo: IOM

Haki za binadamu

Nilipigwa na kukataliwa 

Baba aliponiona hivi, alinipiga. Alinipiga kwa fimbo sana hadi nikazimia huku damu zikinitoka masikioni mwangu.  

Wakati mwingine alinichoma kisu kwenye mkono, na bado nina kovu hilo mwilini.

Unachoona si mimi, Mimi ni Leyla 

Hakuwahi kunikubali. Ingawa, nilikuwa msichana. Nilijua wakati huo, na leo ingawa mimi ni baba, bado sijisijisi kama mwanaume.  

Nimenaswa katika mwili wangu. Sitaki kuwa na ndevu. Unachoona sio nilivyo, mimi ni Leyla. 

Haijakuwa rahisi, chaguo hili, maisha haya. Nilinyanyaswa bila huruma shuleni. Baba yangu hata alijaribu kunifukuza. Alinifukuza nyumbani, na nililazimika kufanya kazi ili kumaliza shule. 

Kisha ilikuwa chuo kikuu. Ungedhani huko ningeweza kuvumiliwa. Haikuwa hivyo hadithi ni ileile ya uonevu na ubaguzi, uonevu na ubaguzi.  

Ninajua kuwa elimu ndio ufunguo wa mafanikio na uvumilivu. Na elimu ilikuwa kama tunda lililokatazwa kwangu. Kadiri walivyojaribu kuzuia maendeleo yangu, ndivyo nilivyokuwa na hamu ya kuitumia hali hiyo kutimiza malengo yangu. 

Lelya akionesha nyumba anakoishi na wanae wawili.
© IOM Turkey/Begum Basaran
Lelya akionesha nyumba anakoishi na wanae wawili.

Niliamua kujificha 

Baada ya kumaliza chuo kikuu, nilifanya kazi katika vyombo vya habari na kuficha utambulisho wangu.  

Hatua kwa hatua, nilianza kutambua watu wengi kama mimi. Tuliwasiliana kupitia ishara za siri wakati wa mchana, lakini usiku nilificha ndevu zangu, nikavaa wigi na kufurahia hisia ya kuwa huru, nikiwa mimi. 

 “Nilioa mwanamke msagaji ili kutuliza familia yangu na tulijaliwa na watoto wawili wawazuri” 

Licha ya wakati mzuri tuliokuwa nao maisha bado yalikuwa magumu. Magumu sana. Nilioa mwanamke msagaji ili kuridhisha familia yangu na tulipata watoto wawili wazuri katika ndoa yetu ya miaka saba. 

Hatimaye, niliamua kuacha kukana mimi ni nani na kufanyia kazi haki zetu za LGBTQI+. Niliungana na watu wengine katika jumuiya hiyo na kuwa mwanaharakati, mwandishi wa blog na kuendesha tovuti ya LGBTQI+. 

Kwa hiyo, hapo nilikuwa mimi sasa. Licha ya matatizo yote, ya kuishi maisha ya aina mbili niliyoishi, na dhiki zote nilizopitia lakini nilikuwa na maisha mazuri sana Lebanoni. Nilikuwa na nyumba, gari zuri, kazi nzuri, marafiki, na watoto wazuri, warembo…hata hivyo shida nazo zilikuwa zikiniandama. 

Watu walikuwa wanakuja kuniua 

Usiku mmoja nikiwa nyumbani nilisikia kelele kutoka nje nikajua wanaume wanakuja kuniua.  

Maisha yangu yalikuwa dhambi na yalistahili kufa, machoni pao. Niliruka kutoka kwenye varanda na kukimbia. 

Sikuchukua chochote kwa sababu nilitaka tu kuepuka kukamatwa na kuuawa. Nilifika uwanja wa ndege saa 3 asubuhi, na nilikuwa Istanbul kabla ya mapambazuko. 

Nilipofika Uturuki, nilihisi kuhamasishwa na uhuru ambao wanajamii wa LGBTIQ+ walifurahia katika jamii.  

Walinipa matumaini kwamba naweza kuwa mwanamke ninayetaka kuwa. Nilipata marafiki wapya na nikaanza kuvaa mavazi mazuri, kujipodoa, na kwenda nao mjini.  

Hata hivyo, ingawa kulikuwa na mshikamano katika jamii yetu, katika jamii pana zaidi, nilikabiliwa na ubaguzi na matamshi ya chuki yale yale ambayo nilikumbana nayo huko Lebanon. 

Leyla akiwa na watoto wake mvulana na msichana.
© IOM Turkey/Begum Basaran
Leyla akiwa na watoto wake mvulana na msichana.

Mama na baba 

Kisha mambo mawili mazuri yakatokea. Kwanza, miezi sita iliyopita, mke wangu wa zamani alisaidia kupatikana nyaraka zote za watoto na dada yangu aliwaleta hapa, na sasa wanaishi nami. Mimi ni mama na ni baba kwao. 

Pili, niliwasiliana na kituo cha wahamiaji kinachoendeshwa na IOM, ambacho kilinisaidia katika masuala ya kisheria, kama vile kuwapeleka watoto wangu shuleni na kupata huduma za afya mara kwa mara. Walinisaidia hata kupata kazi katika mkahawa wa Kiarabu. 

Nataka kuishi kama nilivyo bila wasiwasi. Na tena, sina budi kuishukuru IOM kwa kunisaidia 

“Maisha ni shwari, hofu imekwisha, na nina watoto wangu pamoja nami. Walakini, huu sio mwisho wa safari yangu. “ 

Uturuki imekuwa nzuri kwangu, kwa ujumla. Nataka kuishi kama nilivyo bila wasiwasi. Na tena, sina budi kuishukuru sana IOM kwa kunisaidia kupata mguu kwenye barabara hiyo. 

Nilienda kwenye ofisi ya uhamiaji ya mkoa kwa mahojiano, na baada ya siku mbili, nilipewa hadhi ya mkimbizi kwa masharti. Bado sijapokea taarifa zaidi kuhusu makazi mapya.  

Niko tayari 

Niko tayari wakati wote. Sina hakika nitaishia wapi. Nafikiri itakuwa vyema kuhamia nchi inayozungumza Kiingereza au Kifaransa kwa sababu hizo ndizo lugha ninazozungumza. 

Nataka nimalizie kwa kusema kwamba ubaguzi ni bure kabisa si jambo jema. Hakuna faida yake. Hauna manufaa yoyote, unaathiri watu tu, na unaharibu jamii. 

Kwangu mimi, ulinifanya kuwa imara zaidi, na sasa nina familia mpya, jumuiya ya LGBTIQ+. Sio tu jamii yangu na familia yangu, bali pia ni maisha yangu, na ni ishara ya utambulisho wangu.  

“Na najua jambo moja kwa hakika, sote tumezaliwa sawa, na sote tunastahili kutendewa hivyo.”