Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yashirikiana na wadau kuhakikisha wenye VVU nchini Ukraine wanapata huduma

Mvulana mwenye  umri wa miaka 19 akiwa ameketi kitandani kwake kwenye makazi ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu huko Odessa, Ukraine.Kijana huyu anatumia madawa na anaishi na VVU. Lakini hana uwezo wa kupata dawa.(Picha ya 2019)
© UNICEF/Giacomo Pirozzi
Mvulana mwenye umri wa miaka 19 akiwa ameketi kitandani kwake kwenye makazi ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu huko Odessa, Ukraine.Kijana huyu anatumia madawa na anaishi na VVU. Lakini hana uwezo wa kupata dawa.(Picha ya 2019)

UNAIDS yashirikiana na wadau kuhakikisha wenye VVU nchini Ukraine wanapata huduma

Afya

Vita nchini Ukraine inaendelea kuathiri huduma katika sekta ya afya pamoja na minyororo ya ugavi ambayo mamia ya maelfu ya watu wanaoishi na ukimwi na walioathiriwa na virusi vya ukimwi, VVU wanategemea kuishi.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na harakati za kutokomeza uKimwi, UNAIDS kwa kushirikiana na serikali ya Ukraine na wadau wa mashirika ya kiraia nchini humo wanafanya kazi pamoja  ili kuhakikisha kuna mwendelezo wa huduma za VVU na ulinzi kwa watu muhimu na watu wanaoishi na VVU walioathiriwa na vita.

Baadhi ya watu wamekimbia Odessa lakini wengine wamesalia.
© IMF/Brendan Hoffman
Baadhi ya watu wamekimbia Odessa lakini wengine wamesalia.

Hali ya UKIMWI ikoje Ukraine

Kabla ya vita kuanza nchini Ukraine mwezi Februari 2022, takwimu za UNAIDS zimeeleza watu 260, 000 walikadiriwa kuishi na VVU, 152, 000 kati yao walikuwa wakipata dawa za kuokoa maisha za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi. Hadi kufikia tarehe 3 Mei 2022, maeneo 39 ya matibabu ya kutoa dawa za kupunguza mkali ya ukimsi yalifungwa kutokana na vita.

Wakati akiba ya kutosha ya dawa za VVU nchini Ukraine imehakikishwa na washirika wengi, usambazaji wa dawa kwa watu wanaohitaji nchini humo bado ni changamoto kubwa. 

Mchakato wa upimaji wa UKIMWI nao umeathiriwa na vita. Watu wachache wanagundulika na watu wachache wanaanza matibabu ya VVU. 

Kumekuwa na upungufu wa asilimia 30 ya idadi ya watu wanaoishi na VVU ambao walianza matibabu ya kupunguza makali ya ukimwi mwaka 2022 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2021 (Jan-Mei).

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake  UN Women na shirika la CARE International inaangazia hitaji la kutoa huduma za afya kwa wanawake nchini Ukraine.

Ripoti hiyo inasisitiza hitaji la mkabala wa makutano wa mzozo ambao unashughulikia hatari zilizokithiri kwa jamii zilizotengwa, watu wanaojihusuisha na mapenzi ya jinsia moja pamoja na watu wenye jinsia mbili, watu wanaoishi na ulemavu na watu wanaoishi na magonjwa sugu ambao wanakabiliwa na matatizo makubwa na wana mahitaji maalum kuhusiana na afya na usalama wao

Nini kinafanyika

Shukrani kwa juhudi za pamoja za shirika la PEPFAR, mfuko wa kimataifa wa kukabiliana na UKIMWI, kifua kikuu na Malaria, kituo cha afya ya umma cha Ukraine, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya Ulimwenguni WHO, UNAIDS na mashirika ya kiraia, jumla ya vifaa vya tiba ya kupunguza makali ya ukimwi ndani ya nchi vinatosha, lakini changamoto za vifaa na usalama bado zipo.

Tiba ya kupunguza makali ya ukimwi imewasilishwa kwa mikoa yote (na utoaji wa vifurushi 2500 unaendelea kidogo kwenye eneo la a Kherson), isipokuwa mikoa ya Donetsk na Luhansk.

Tiba ya kupunguza makali ya ukimwi ya post-exposure prophylaxis (PEP) kwa waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia nayo pia inapatikana. 

PEP inasambazwa katika maeneo ya tiba ya kupunguza makali y ukimwi, vituo vya UKIMWI na hospitali na inapatikana saa 24, siku saba za wiki.

Kazi katika mazingira magumu

Japo kuwa vita inaendelea nchini Ukraine, tahadhari sasa ipo katika kuhakikisha dawa za kuokoa maisha za VVU zinawafikia watu wanaohitaji kwa wakati na huduma za VVU zinaendelea.

Kupata vifaa vya matibabu na huduma kwa makundi ya watu walio katika mazingira magumu bado ni changamoto kubwa na UNAIDS inaunga mkono washirika wanaofanya kazi nchini Ukraine na kimataifa ili kuendeleza kupata suluhisho za haraka za kutoa msaada wa kimatibabu na wa kibinadamu kwa mamia ya maelfu ya Wananchi wa Ukraine.

Mashirika ya kiraia, kwa ushirikiano na kituo cha afya ya umma cha Ukraine, yanaongeza juhudi za kishujaa kuwasilisha vifaa na huduma muhimu kwa watu wanaoishi na walioathirika na VVU, ikiwa ni pamoja na watu walio katika mazingira magumu. Wanawafikia watu katika maeneo yenye changamoto nyingi licha ya kuwepo kwa  vizuizi vikubwa.