Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Msikiti wa Sheikh Zayed ulioko Falme za Kiarabu

Buriani Sheikh Khalifa Bin Zayed Al Nahyan: Guterres

Unsplash/Azhar J
Msikiti wa Sheikh Zayed ulioko Falme za Kiarabu

Buriani Sheikh Khalifa Bin Zayed Al Nahyan: Guterres

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya kifalme, kwa Serikali na watu wa umoja wa nchi za Falme za Kiarabu UAE kwa kuondokewa na rais wao Sheikh Khalifa Bin Zayed Al Nahyan. 

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake mjini New York Marekani Katibu Mkuu amesema Sheikh Khalifa aliongoza Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu tangu mwaka 2004, akimrithi babake, Sheikh Zayed bin Sultan Al Nahyan, mwanzilishi wa nchi hiyo.  

Ameongeza kuwa Sheikh Khalifa pia aliongoza UAE kupitia kipindi muhimu cha maendeleo yake, kilichoangaziwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi na kuongezeka kwa ushawishi wake wa kikanda na kimataifa. 

Katibu Mkuu amesisitiza ahadi ya Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano wake wa karibu na Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu, ikiwa ni pamoja na masuala ya kibinadamu na mazungumzo ya kidini, pamoja na amani ya kikanda na kimataifa, usalama na maendeleo endelevu. 

Duru za Habari zinasema amefariki dunia leo Ijumaa akiwa na umri wa miaka 73 na alikuwa akijulikana kama miongoni mwa wafalme tajiri zaidi duniani.