Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Covid-19, vita ya Urusi na Ukraine na tabianchi vimeathiri Afrika - UNDP 

Mji wa Johannesburg Aprili 3, 2020 nchini Afrika Kusini.
IMF Photo/James Oatway
Mji wa Johannesburg Aprili 3, 2020 nchini Afrika Kusini.

Covid-19, vita ya Urusi na Ukraine na tabianchi vimeathiri Afrika - UNDP 

Ukuaji wa Kiuchumi

Kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), sehemu tatu ya athari zinazoendelea za janga la Covid-19, athari mpya za vita vya Urusi na Ukraine, na changamoto zinazohusiana na tabianchi zimeathiri sana juhudi za kudumisha amani na kupunguza umaskini na ukosefu wa usawa katika bara la Afrika. 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Ahunna Eziakonwa, Msimamizi Msaidizi wa UNDP na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kanda ya Afrika, amesema kuwa "hatujawahi kupata shinikizo na changamoto kubwa juu ya uwezo wetu wa kudumisha amani na maendeleo katika sayari yenye afya kama tunavyoshuhudia hivi sasa. Janga la ulimwengu ambalo lilivuruga  ulimwengu na kuibadilisha milele. Tumeona matokeo yake, lakini pia kwa hali ya awali, kuongezeka kwa umaskini na ukosefu wa usawa.” 

Akisisitiza kwamba mshikamano wa kimataifa unahitajika zaidi kuliko hapo awali, Ahunna Eziakonwa wa UNDP ameongeza kuwa "tuliona jinsi Covid-19 inavyotatiza juhudi za kudumisha au kuondokana na ukosefu wa usalama unaosababishwa na nguvu nyingi ikiwa ni pamoja na itikadi kali na athari za hii, matokeo yake, yaliathiri maisha na ustawi lakini pia kuleta hali ya kutoridhisha sana kuhusu watu, ambayo inasababisha kushuka kwa demokrasia.” 

Vita vya Ukraine vinaathiri chakula, mafuta na ufadhili wa bara la Afrika. Kwa Raymond Gilpin, Mchumi Mkuu wa Afrika wa UNDP na Mkuu wa Timu ya Mkakati, Uchambuzi, na Utafiti, "hili ni janga ambalo halijawahi kutokea kwa bara hili, na halijawahi kutokea kwa sababu bara linakabiliwa na mambo matatu: athari zinazoendelea za janga la Covid, ambalo halijawahi kutokea, athari za vita vya Urusi na Ukraine na tatu changamoto na shinikizo zinazohusiana na tabianchi.” 

Baadhi ya nchi barani Afrika hutegemea hadi asilimia 80 ya ngano inayotoka Urusi na Ukraine. Kupanda kwa bei kunaweza kusababisha hali nyingine ya kutoridhika na pengine machafuko, amenya Gilpin. "Mfumuko wa bei duniani umeingizwa katika uchumi wa Afŕika kwasababu Afŕika inategemea sana uagizaji wa chakula, mafuta, madawa, na bidhaa zinazodumu kwa matumizi. Tunaenda kuona taharuki. Ikiwa hii itaelekea kwenye maandamano yenye vurugu au la, haijulikani. Lakini kile ambacho historia, hasa historia ya hivi karibuni, imetuambia ni kwamba hii ni uwezekano wa kipekee.” 

UNDP imesisitiza kuwa hasa katika nchi zenye chaguzi zijazo ambapo mazingira ya uchaguzi tayari yana hisia nyingi kunaweza kusababisha shinikizo la ziada la kijamii. 

TAGS: UNDP, Afrika, Covid-19