Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUSCA yazindua kampeni ya kusaidia upatikanaji wa amani CAR 

Mlinda amani wa MINUSCA akiwa katika doria nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR-Kutoka Maktaba
MINUSCA/Herve Cyriauqe Serefi
Mlinda amani wa MINUSCA akiwa katika doria nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR-Kutoka Maktaba

MINUSCA yazindua kampeni ya kusaidia upatikanaji wa amani CAR 

Amani na Usalama

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA umezindua kampeni ya ulinzi wa raia ili kusaidia upatikanaji wa amani pamoja na kuwezesha mamlaka za serikali nchini humo kutekeleza majukumu yake.

Uzinduzi wa kampeni hiyo iliyoendeshwa kwa njia ya mdahalo katika kutafakari maudhui ya mamlaka ya MINUSCA katika mkoa wa mamberé-Kadéi ilipambwa na burudani mbalimbali ikiwemo ngoma za asili kutoka katika kikundi cha ngoma cha TANBATT- 05. 

 

Mdahalo huo ulihudhuriwa na vikosi vinavyoundwa na MINUSCA kikiwemo Kikosi cha TANBATT 5 kutoka Tanzania,  viongozi mbalimbali wa kiserikali ya, wasimamizi wa uchaguzi, wadau wa masuala kijinsia na kijamii.  

Aidha mdahalo huo uliwapa fursa wananchi wa Mabere kadei  kutoa maoni na mapendekezo kuhusu mamlaka ya MINUSCA. Mwananchi mmoja kwa niaba ya wengine anasema, “uwepo wa vikosi vya MINUSCA hapa Berberati na mkoa mzima wa Mambere kadei, umesaidia kuondoa vikundi vya waasi vilivyokuwa vimejificha katika maeneo mbalimbali kwa ajili kutekeleza vitendo vya kihalifu. lakini pia uwepo wa vikosi hivyo vimeweza kurejesha na kusimamia haki za binaadamu. kwa sasa berberati kuna amani, na wananchi wanaweza kufanya shughuli mbalimbali za kujipatia kipato tofauti na awali.kupitia mdahalo huu tunawapongeza kwa juhudi wanazozifanya za kurejesha amani iliyopotea kwa kipindi kirefu. Asanteni.” 

Naye Mkuu wa Wilaya wa Berberati Bwana Goumindji Jacques Antoine alishuhudia akaeleza namna  vikosi vya MINUSCA ikiwemo kikosi cha TANBATT-05 vimejitolea kusaidia uwepo wa amani katika mkoa wa Mambere Kadei na kuwezesha mamlaka za serikali kuweza kutekeleza majukumu yao, “MINUSCA wamefanya mambo mengi kwa nchi yetu sio tu hapa Berberati. MINUSCA imefanya mambo mengi kama; kulinda amani ya nchi yetu, kusaidia kuwezesha uchaguzi, kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kama   ujenzi wa majengo ya ofisi za meya na kwa wahusika waliopo hapa leo wakawe wajumbe wazuri kwa wengine walioshindwa kufika kwenye mdahalo huu.” 

TANBATT 5 ni miongoni mwa vikosi vya ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA.