Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Naomi mwenye umri wa miaka 22, ni mkimbizi kutoka DRC anaishi kambini Mantapala nchini Zambia pamoja na watoto wake na mama yake mzazi.

Mgao wa fedha wakidhi mahitaji yangu na familia - Mkimbizi Naomi

WFP/Andy Wiggins
Naomi mwenye umri wa miaka 22, ni mkimbizi kutoka DRC anaishi kambini Mantapala nchini Zambia pamoja na watoto wake na mama yake mzazi.

Mgao wa fedha wakidhi mahitaji yangu na familia - Mkimbizi Naomi

Wahamiaji na Wakimbizi

Kutana na Naomi, mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa anaishi kwenye makazi ya wakimbizi ya Mantapala nchini Zambia, makazi ambayo asilimia 80 ya wakazi wake 18,000 ni wanawake.
 
Katika makazi haya, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP linaendelea na utaratibu wake wa kupatia wakimbizi msaada wa fedha ili kuweza kukimu mahitaji yao ikiwemo ya chakula.

Mathalani hivi karibuni WFP ilipokea mchango wa dola 650,000 kutoka Marekani ikiwa ni kuitikia wito wa kuongeza mchango ili kuepusha kupunguza mgao kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wanaoishi makazi ya wakimbizi ya Mantapala nchini Zambia.

Fedha hizo zitasaidia kupatia msaada wa fedha kwa wakimbizi kwa kipindi cha miezi mitatu.
Miongoni mwa wanufaika wa misaada ya aina hiyo ya fedha ni Naomi mwenye umri wa miaka 22.

Fedha za WFP zinamsaidia vipi Naomi?

Naomi akinunua mahitaji ya familia yake kwenye soko lililoko kwenye makazi ya wakimbizi ya Mantapala nchini Zambia
WFP/ Andy Wiggins
Naomi akinunua mahitaji ya familia yake kwenye soko lililoko kwenye makazi ya wakimbizi ya Mantapala nchini Zambia

Naomi alianza kuishi kwenye makazi hayo ya Mantapala, yeye na watoto wake pamoja na mama yake mzee tangu mwaka 2020. Anasema anapenda kupokea msaada wa fedha badala ya chakula kwa sababu fedha inamwezesha kununua mahitaji ya halisi ya familia yake.

Naomi anatumia msaada wa fedha anaopata kununua mahitaji mbalimbali ya familia yake ikiwemo chakula kama vile dagaa na nyanya.
WFP/ Andy Wiggins
Naomi anatumia msaada wa fedha anaopata kununua mahitaji mbalimbali ya familia yake ikiwemo chakula kama vile dagaa na nyanya.

“Kwa msaada wa fedha ninazopatiwa, nanunua mahindi, mafuta ya kupikia, chumvi, dagaa, mihogo na mboga ya majani. Ninapenda kupatiwa msaada wa fedha kwa sababu naweza pia kununua dawa kwa ajili ya watoto wangu pindi wanapougua,” anasema Naomi.

Naomi akiandaa mlo wa asubuhi au staftahi ambao ni wali kwa mayai nje ya makazi ya nyumba yao huko Mantapala nchini Zambia.
WFP/ Andy Wiggins
Naomi akiandaa mlo wa asubuhi au staftahi ambao ni wali kwa mayai nje ya makazi ya nyumba yao huko Mantapala nchini Zambia.

Asilimia 80 ya wakimbizi Mantapala ni wanawake

Makazi ya wakimbizi ya Mantapala, yaliyoko wilaya ya Nchelenge jimbo la Luapula nchini Zambia yalianzishwa mwaka 2018 na kwa mujibu wa takwimu za karibuni zaidi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, kuna idadi ya wakimbizi 18,000.

Miongoni mwao ni wasichana 5419, wavulana 5358, wanawake, 3712 na wanaume 3523. Hii ina maana kuwa asilimia 60 ya wakazi kambini hapa ni watoto wenye umri wa chini  ya miaka 18. Asilimia 80 ya wakazi wote ni wanawake.

Wapwa zake Naomi wakiwa na bibi yao mbele ya makazi yao huko Mantapala.
WFP/ Andy Higgins
Wapwa zake Naomi wakiwa na bibi yao mbele ya makazi yao huko Mantapala.

Zaidi ya asilimia 90 ya wakimbizi wanapatiwa msaada wa fedha taslimu. Kaya ambazo zinaongozwa na  mtoto, msaka hifadhi, mkimbizi asiye na kitambulisho au mkimbizi mpya hupatiwa mgao wa chakula kila mwezi badala ya fedha taslimu.

Mama mzazi wa Naomi aitwaye Mbishwa na mwenye umri wa miaka 71 akiwa mbele ya makazi yao Mantapala, Zambia
WFP/ Andy Higgins
Mama mzazi wa Naomi aitwaye Mbishwa na mwenye umri wa miaka 71 akiwa mbele ya makazi yao Mantapala, Zambia

Mgao wa fedha unachochea uchumi wa Mantapala

Mgao wa chakula unajumuisha unga wa mahindi, vyakula vyenye virutubisho, maharage, mafuta ya kupikia yenye virutubisho pamoja na chumvi yenye madini ya Iodine.

Naomi akiwa kwenye kioski tayari kuchukua fedha taslimu za msaada kutoka WFP
© WFP/Andy Higgins
Naomi akiwa kwenye kioski tayari kuchukua fedha taslimu za msaada kutoka WFP

WFP inasema mgao wa fedha unapanua wigo wa aina ya mlo ambao mkimbizi atakula na familia yake, inachochea ukuaji wa uchumi wa eneo ambako wakimbizi wanaishi na pia inamjengea uwepo mpokeaji kuchagua aina ya chakula anachotaka kula.

Mtoto wa Naomi, Paapo akipata staftahi iliyoandaliwa na mama  yake kwenye makazi yao huko Mantapala.
WFP/ Andy Wiggins
Mtoto wa Naomi, Paapo akipata staftahi iliyoandaliwa na mama yake kwenye makazi yao huko Mantapala.