Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu ya afya ya uzazi haipaswi kuwa aibu – Tumaini Community Services Mbeya Tanzania 

Utepe mwekundu- ishara ya kimataifa ya kampeni ya kupambana na VVU na UKIMWI
Public Health Alliance/Ukraine
Utepe mwekundu- ishara ya kimataifa ya kampeni ya kupambana na VVU na UKIMWI

Elimu ya afya ya uzazi haipaswi kuwa aibu – Tumaini Community Services Mbeya Tanzania 

Wanawake

Nchini Tanzania, Shirika la Tumaini Community Services linatekeleza mradi wa ‘Dreams’ yaani ‘Ndoto’ katika wilaya ya Mbeya mjini, Kyela na Mbarari mkoani Mbeya kwa ufadhili wa mfuko wa rais wa Marekani wa harakati za kupambamba na UKIMWI, PEPFAR kanda ya Tanzania, lengo likiwa kuwawezesha vijana balehe elimu ya afya ya uzazi, elimu ya kujitambua na elimu ya kiuchumi ili kupunguza maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI.

Tatu Mwambungu wa wilayani Kyela ni mnufaika wa mradi wa Dreams unaotekelezwa mkoani Mbeya na shirika lisilo la kiserikali la Tumaini Community Services anaeleza sababu anazofikiri kuwa ni sababu zinazowaweka matatizoni vijana balehe akisema ni kutokana na kwamba wanakuwa hawana elimu sahihi ya afya ya uzazi akisema kwamba wanafika umri wa kubalehe lakini, “tunakuwa hatujui kutokana na jamii yetu wanaficha au wzazi wanaficha vile vitu ambavyo binti anatakiwa kuvijua akishakua amebalehe.”  

 

Tatu Mwambungu yeye ameema sababu ni ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi, Vaileth Bukuku yeye ni  mkazi wa Mbeya mjini naye anaeleza kuwa elimu ya afya ya uzazi ina umuhimu mkubwa kwa vijana balehe n ani elimu ambayo inatakiwa, “ipewe kipaumbele sana.” 

“Wengine wanakatisha masomo kwa sababu ya kuzaa. Yaani ingekuwa ni elimu kubwa ningefurahi sana ingekuwa ni elimu kubwa ambayo ingetolewa sana hususani kuanzia darasa la 7 au la 6 kwenda juu mpaka vyuo huku juu inatakiwa iwe elimu ambayo ni namba moja.” Anasisitiza Vailet.  

Dkt. Steward Kilumile ni Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Miyombweni kilichopo Wilaya ya Mbarari anasema elimu kuhusu afya ya uzazi inayotolewa kwa vijana anaona inaleta mabadiliko. Akisema, “kupitia mradi kama huu wa dreams kwa kuwa wanapata elimu kwenye vikundi inazidi kuwapa vijana upeo dhidi ya mazingirea hatarishi.” 

Jonathan Mwashilindi ni Mkurungezi wa shirika hilo la Tumaini anasema wasichana wenye umri mdogo kutokana na kukosa muongozo mzuri ndipo wanajikuta wanapata ujauzito wakiwa bado watoto wadogo na hawajui hao watoto watakaozaliwa watawatunza kwa namna gani. Kwa msingi huo anatoa wito kwa kila mtu katika jamii kushiriki katika kusaidia “ili hawa mabinti ndoto zao waweze kziishi baadaye.”