Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki ni msingi wa kuondokana na ukatili wa kingono vitani

Mizozo na ukosefu wa utulivu vinaweza kuchochea viwango vya juu vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana
© UNICEF/STARS/Kristian Buus
Mizozo na ukosefu wa utulivu vinaweza kuchochea viwango vya juu vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana

Haki ni msingi wa kuondokana na ukatili wa kingono vitani

Amani na Usalama

Haki za wanawake ni haki za binadamu n ani kwa kila mahali wakati wa vita na amani, amesema Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala y ukatili wa kijinsia kwenye maeneo ya mizozo.

Akihutubia mjadala wa wazi wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika Jumatano kujadili maudhui ya Wanawake: Amani na Usalama, Bi. Patten ametumia hadhira huyo kusihi mabalozi wanaowakilishi nchi zao kuhakikisha kuna uwajibikaji dhidi ya wale wanaotekeleza ukatili wa kingono kwenye mizozo.

Kauli yake hiyo inatokana na ukweli kwamba hivi sasa ubakaji unatumika kama silaha kwenye vita na hivyo anataka hatua ichukuliwe ili manusura na waathirika wa ukatilili huo waweze kupata haki yao na wakati huo kuepusha vitendo vya aina hiyo visitokee tena.

Uhalifu wa muda mrefu wa vitani lakini usioadhibiwa

Akirejelea kuwa Baraza hilo limepitisha maazimio 10 kuhusu Wanawake, Amani na Usalama, matano kati yao yakijikita katika kuzuia na kushughulikia ukatili wa kingono kwenye mizozo, Bi. Patten ameanza kwa kuuliza maazimio hayo yana maana gani hivi sasa kwa wanawake walioko Ukraine, Afghanistan, Myanmar au Tigray Kaskazini mwa Ethiopia.

“Kila wimbi jipya la vita linaleta ongezeko la janga la kibinadamu, ikiwemo wimbi jipya la uhalifu wa siku nyingi vitani lakini ambao hufumbiwa midomo na nadra sana kuadhibiwa,m” amesema Bi, Patten.

Ongezeko kubwa la matukio

Bi. Patten, katika ripoti yake mpya,  amewasilisha shuhuda za visa lukuki vya ubakaji na ukiukwaji mwingine vikifichua kile alichokiita athari zinazochochea ukwepaji wa sheria.
Ripoti hiyo inahusisha nchi 18 ikiwa na visa 3,298 vilivyothibitishwa na Umoja wa Mataifa na vimetekelezwa mwaka jana, idadi ambayo ni visa 800 zaidi kuliko mwaka 2022, ikiwa ni ongezeko kubwa.

Pramila Patten, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN kuhusu ukatili wa kingoni kwenye mizozo akihutubia Baraza la Usalama kuhusu Wanawake na amani na  ulinzi.
UN /Loey Felipe
Pramila Patten, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN kuhusu ukatili wa kingoni kwenye mizozo akihutubia Baraza la Usalama kuhusu Wanawake na amani na ulinzi.

Idadi kubwa ya walengwa, saw ana asilimia 97 ni wanawake na wasichana, ilhali visa 83 vilihusisha wanaume na wavulana, wengi wao wakiwa ni wale wanaoshikiliwa korokoroni. Visa 12 ni vya LGBTQI ambao ni wasagaji, mashoga, wasiotambua jinsia zao, na wenye mahusiano na zaidi ya jinsia moja

Ufunguliaji mashtaka kama kinga

Bi. Patten amesisitiza umuhimu wa ufunguliaji wa mashtaka kama njia mojawapo muhimu ya kuzuia vitendi hivyo, kwa kuwa vinaweza kusaidia kubadili utamaduni wa ukwepaji sheria kwenye uhalifu huo na badala yake kujengwa kwa utamaduni wa kujizuia kufanya vitendo hivyo.“Wakati ukwepaji sheria unahalalisha ghasia, haki inaimarisha maadili ya kimataifa. Ni wakati wa kuzingatia uwajibishaji na kuhakikisha kuwa uwekaji nyaraka wa matukio ya leo ni mwanzo wa kuanza mashtaka kesho yake,” amefafanua Bi. Patten.

Kuhusu kinachopaswa kufanyika, ripoti iyo inatoa wito wa kujenga utamaduni wa kuchukua hatua ya kuzuia, kama vile kupitia ushirikishaji wa kisiasa na kidiplomasia ili kujadili masuala ya kukomesha ukatili wa kingono katika mijadala ya kusitisha mapigano na mikataba ya amani.

Hatua nyingine ni matumizi ya viashiria vya awali vya maonyo kuhusu ukatili wa kingono sambamba na uchambuzi wa vitisho, udhibiti wa usafirishaji wa silaha ndogo ndogo, mfumo wa haki unaozingatia jinsia, marekebisho ya sekta ya ulinzi pamoja na kupaza sauti za manusura.

Ubakaji na visasi Tigray

Mkutano huo pia ulipata fursa ya kusikia sauti kutoka wawakilishi wa mashirika ya kiraia akiwemo Hilina Berhanu kutoka Ethiopia ambaye amezungumzia kile alichoshuhudia wakati wa ziara yake ya hivi karibuni jimboni Tigray, ambako ubakaji umegeuzwa kuwa mbinu  ya vita au mbinu ya kulipa visasi.

Ghasia hii inachochewa kikabila, amesema, na hutumiwa kudhalilisha manusura na jamii zao. Wanaume na wavulana nao pia ni manusura, ilhali wanawake wenye ulemavu, na wale kutoka jamii za asili wamekuwa hatarini Zaidi.

Matukio ya ukatili wa kingono na kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana vimeshamiri khuko Tigray, Amhara na Afar nchini Ethiopia
© UNICEF Ethiopia/Esiey Leul
Matukio ya ukatili wa kingono na kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana vimeshamiri khuko Tigray, Amhara na Afar nchini Ethiopia

Bi. Bernahu amesihi Baraza la Usalama kuhakikisha harakati zote za kuweka rekodi za matukio, kuchunguza na kuzuia ukatili wa kingono kwenye mizozo, kitovu chake kinakuwa ni manusura.
“Mabalozi lazima wazitake pande kinzani ziruhusu njia salama za kupitisha misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wahitaji huko Tigray na kwingineko na kwamba misaada lazima ijumuishe huduma za afya za kina za masuala ya afya ya uzazi na viungo vya uzazi.

“Ukosefu wa usaidizi wa kisaikolojia pia kuna maanisha kuwa huduma ya afya ya akili kwa manusura inakuwa mashakani. Wengi tayari wamekufa kwa kujiua,” amesema.

Bi. Berhanu alikuwa na ombi maalum kwa mataifa matatu ya Afrika yenye ujumbe Barazani: Gabon, Ghana na Kenya – akizisihi kushirikiana kwenye Umoja wa Mataifa na pia kupitia Muungano wa Afrika kuchochea hatua kuhusu wanawake, amani na ulinzi.

Nchi hizo tatu pia zilipatiwa jukumu la “kuwa na mtazamo madhubuti ya mtazamo ulioko hivi sasa nchini Ethiopia ya kwamba kuunga mkono juhudi za uchunguzi wa ukatili wa kingono nchini humo, kunaweza kupeleka mrama kwa kiasi ajenda ya serikali ya sasa ya mapendekezo ya marekebisho ya miundo.