Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni nini Umoja wa Mataifa unaweza kufanya? Majibu ya maswali yako 5 

Nyumba iliyoharibiwa wakati wa mzozo nchini Ukraine.
© UNICEF/Anton Skyba for The Globe and Mail
Nyumba iliyoharibiwa wakati wa mzozo nchini Ukraine.

Ni nini Umoja wa Mataifa unaweza kufanya? Majibu ya maswali yako 5 

Masuala ya UM

Vita ya sasa nchini Ukraine kufuatia uvamizi na Urusi, imezua maswali ya kila aina kuhusu Umoja wa Mataifa, hususan jukumu la Baraza la Usalama, Baraza Kuu na Katibu Mkuu. 

Hapa kwenye UN News Kiswahili, tumezama kwa kina katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa ili kujaribu kukupa majibu ambayo unaweza kuwa unatafuta. 

Je, Baraza la Usalama linaweza kusimamisha vita? 

Hebu kwanza tuangalie wajibu wake. 

Kazi na mamlaka ya Baraza la Usalama vimeainishwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa, nyaraka  ambayo ni muongozo wa Umoja wa Mataifa. Mkataba huo ulitiwa saini tarehe 26 Juni 1945, huko San Francisco, Marekani katika hitimisho la Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Umoja huo na ilianza kutumika tarehe 24 Oktoba 1945. 

Baraza la Usalama, lina wajumbe 15 ambapo viti vitano ni vya kudumu vikishikiliwa na China, Ufaransa, Shirikisho la Urusi, Uingereza na Marekani, na viti 10 visivyo vya kudumu vinavyozunguka kwa uchaguzi kati ya nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa. Baraza la Usalama lina jukumu la msingi la kudumisha amani na usalama wa kimataifa. Inachukua nafasi ya kwanza katika kuamua kuwepo kwa tishio kwa amani, uvunjifu wa amani au kitendo cha uchokozi. 

Jambo ambalo huenda hukujua ni kwamba kabla ya mwaka 1965, Baraza la Usalama lilikuwa na wajumbe 11, sita kati yao wakiwa sio wa kudumu. Upanuzi wa wajumbe 15 ulitokea mwaka 1991 baada ya marekebisho ya Ibara ya 23 (1) ya Mkataba kupitia kupitishwa kwa azimio (A/RES/1991(XVIII)) la Baraza Kuu

Ingawa bado kuna baadhi ya Mataifa 60 Wanachama wa Umoja wa Mataifa ambao hayajawahi kuketi kwenye Baraza la Usalama, wanachama wote wa Umoja wa Mataifa, hata hivyo, wanakubaliana chini ya Kifungu cha 25 cha Mkataba huo, kukubali na kutekeleza maamuzi yaliyopitishwa na Baraza la Usalama. Kwa mantiki hiyo, hatua zinazochukuliwa na Baraza zinawabana nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa. 

Wakati wa kushughulikia mizozo, Baraza, likiongozwa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama linaweza kuchukua hatua kadhaa. 

Kwa mujibu wa sura ya VI ya Mkataba, Baraza linaweza kuziita pande zinazohusika kusuluhishwa kwa njia ya amani na kupendekeza mbinu za marekebisho au masharti ya utatuzi. Inaweza pia kupendekeza kupelekwa kwa uhasama kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), ambayo inajulikana sana kama ‘Mahakama ya Dunia’ na ndicho chombo kikuu cha mahakama cha Umoja wa Mataifa, kilichoko  Hague nchini Uholanzi. 

Katika baadhi ya matukio, Baraza la Usalama linaweza kuchukua hatua chini ya Sura ya VII ya Mkataba na kuamua kuweka vikwazo au hata inaweza kuidhinisha, kama njia ya mwisho, wakati njia za amani za kutatua mzozo zimegonga mwamba, matumizi ya nguvu, na nchi wanachama, muungano wa wanachama au shughuli za amani zilizoidhinishwa na Umoja wa Mataifa kudumisha au kurejesha amani na usalama wa kimataifa. 

Muhimu zaidi, hatua inayohitajika kutekeleza maamuzi ya Baraza la Usalama kwa ajili ya kudumisha amani na usalama wa kimataifa itachukuliwa na wanachama wote wa Umoja wa Mataifa au na baadhi yao, kama Baraza la Usalama litakavyoamua kwa mujibu wa Sura ya VII. 

Mara ya kwanza Baraza liliidhinisha matumizi ya nguvu ilikuwa mwaka 1950, chini ya kile kilichojulikana kama hatua ya utekelezaji wa kijeshi, ili kuhakikisha kuondolewa kwa vikosi vya Korea Kaskazini kutoka Jamhuri ya Korea. 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likiwa katika mkutano wa dharura kuhusu Ukraine.
© UN Photo/Mark Garten
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likiwa katika mkutano wa dharura kuhusu Ukraine.

Kura ya turufu ni nini na inaweza kutumika vipi? 

Utaratibu wa upigaji kura katika Baraza la Usalama unaongozwa na Kifungu cha 27 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa ambacho kinabainisha kwamba kila mwanachama wa Baraza ana kura moja. 

Wakati wa kuamua juu ya "utaratibu wa mambo", wanachama tisa wanahitaji kupiga kura kuunga mkono ili uamuzi kupitishwa. Katika mambo mengine yote kura ya uthibitisho ya wanachama tisa "pamoja na kura zinazolingana za wanachama wa kudumu" zinahitajika. 

Hiyo ikimaanisha , kura yakupinga ya kura yoyote kati ya tano za kudumu (China, Ufaransa, Shirikisho la Urusi, Uingereza au Marekani) inaweza kuzuia kupitishwa na Baraza kwa rasimu ya azimio lolote linalohusiana na masuala muhimu. 

Tangu mwaka 1946, wanachama wote watano wa kudumu - almaarufu kama 'P5' - wametumia haki ya kura ya turufu wakati mmoja au mwingine katika masuala mbalimbali. Hadi sasa, takriban asilimia 49 ya kura za turufu zilipigwa na Muungano wa Jamhuri za Kisoshalisti za Kisovieti na baadaye Shirikisho la Urusi (uanachama wa USSR katika Umoja wa Mataifa, pamoja na Baraza la Usalama, uliendelea na Shirikisho la Urusi). Asilimia 29 na Marekani, asilimia 10 na Uingereza, na asilimia sita kila moja na China na Ufaransa. 

Pata habari zaidi hapa kuhusu kura za turufu katika Mabaraza ya Usalama tangu 1946. 

Familia zinawasili Berdyszcze, Poland baada ya kuvuka mpaka kutoka Ukraine baada ya kukimbia machafuko.
© UNICEF/Tom Remp
Familia zinawasili Berdyszcze, Poland baada ya kuvuka mpaka kutoka Ukraine baada ya kukimbia machafuko.

Je, Baraza Kuu linaweza kuingilia kati pale Baraza la Usalama linashindwa kufanya maamuzi ya kuzuia vita? 

Kwa mujibu wa azimio la 377A (V) la Baraza Kuu la mwaka 1950, ambalo linajulikana sana kama 'Kuungana kwa ajili ya Amani', ikiwa Baraza la Usalama haliwezi kuchukua hatua kwa sababu ya kukosekana kwa umoja kati ya wanachama wake watano wa kudumu wenye kura ya turufu, Baraza hilo lina uwezo wa kutoa mapendekezo kwa wanachama wengine wa Umoja wa Mataifa kwa hatua za pamoja za kudumisha au kurejesha amani na usalama wa kimataifa. 

Kwa mfano mara nyingi zaidi, Baraza la Usalama huamua ni lini na wapi operesheni za amani za Umoja wa Mataifa zinapaswa kutekelezwa, lakini kihistoria, wakati Baraza la Usalama halijaweza kuchukua uamuzi, Baraza Kuu limefanya hivyo. Kwa mfano, mwaka 1956, Baraza Kuu lilianzisha Kikosi cha kwanza cha Dharura cha Umoja wa Mataifa (UNEF I) Mashariki ya Kati. 

Aidha, Baraza Kuu linaweza kukutana katika Kikao Maalum cha dharura iwapo litaombwa na wajumbe tisa wa Baraza la Usalama au na wajumbe wengi wa Baraza hilo. 

Hadi sasa, Baraza Kuu limefanya Vikao Maalum 11 vya dharura (8 kati ya hivyo vimeitishwa na Baraza la Usalama). 

Hivi majuzi, tarehe 27 Februari 2022, Baraza la Usalama, kwa kuzingatia kwamba ukosefu wa umoja wa wanachama wake wa kudumu kulizuia kutekeleza jukumu lake la msingi la kudumisha amani na usalama wa kimataifa, liliamua kuitisha Kikao Maalum cha Dharura cha Baraza la Kuu. Mkutano Mkuu katika azimio lake 2623 (2022)

Kufuatia hilo, mnamo Machi 1, 2022, Baraza Kuu, lililokutana katika kikao cha dharura, lilipitisha azimio ambalo lilishutumu "uchokozi wa Shirikisho la Urusi dhidi ya Ukraine kwa kukiuka Kifungu cha 2 (4) cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa, na kutaka Shirikisho la Urusi lisitishe mara moja matumizi yake ya nguvu dhidi ya Ukraine na kuondoa kabisa na bila masharti vikosi vyake vyote vya kijeshi kutoka eneo la Ukraine ndani ya mipaka yake inayotambulika kimataifa. 

Hata hivyo, tofauti na maazimio ya Baraza la Usalama, maazimio ya Baraza Kuu si ya lazima, ikimaanisha kwamba nchi hazilazimiki kuyatekeleza. 

Kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukraine
UN / Evan Schneider
Kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukraine

Je nchi inaweza kuondolewa kutoka kutoka kuwa mwanachama wa UN? 

Kifungu cha 6 cha Mkataba kinasomeka kama ifuatavyo: 

Mwanachama wa Umoja wa Mataifa ambaye ameendelea kukiuka kanuni zilizomo katika Mkataba huu anaweza kufukuzwa kutoka kwa Shirika na Baraza Kuu baada ya mapendekezo ya Baraza la Usalama. 

Hii haijawahi kutokea katika historia ya Umoja wa Mataifa. 

Kifungu cha 5 kinatoa masharti ya kusimamishwa kwa nchi mwanachama: 

Mwanachama wa Umoja wa Mataifa ambaye hatua ya kuzuia au ya utekelezaji imechukuliwa na Baraza la Usalama anaweza kusimamishwa kutekeleza haki na fadhila ya uanachama na Baraza Kuu baada ya mapendekezo ya Baraza la Usalama. Utekelezaji wa haki na fadhila unaweza kurejeshwa na Baraza la Usalama. 

Kusimamishwa au kufukuzwa kwa nchi mwanachama kutoka kwa Jumuiya kunafanywa na Baraza Kuu kufuatia mapendekezo ya Baraza. Pendekezo kama hilo linahitaji kura ya pamoja ya wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama. 

Isipokuwa wakubali kufukuzwa au kusimamishwa kwao wenyewe, wanachama wa kudumu wa Baraza wanaweza tu kuondolewa kupitia marekebisho ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kama ilivyobainishwa katika Sura ya XVIII

Umoja wa Mataifa, hata hivyo, umechukua hatua dhidi ya baadhi ya nchi kukomesha dhuluma kubwa. Mfano mmoja ni kisa cha Afrika Kusini na mchango wa chombo hicho cha dunia katika mapambano ya kimataifa dhidi ya ubaguzi wa rangi, kwa kumulika kwa ulimwengu kuhusu unyama wa mfumo huo, kuhalalisha upinzani wa watu wengi, kuendeleza hatua za kupinga ubaguzi wa rangi na mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali. Kuweka vikwazo vya silaha, na kuunga mkono vikwazo vya mafuta na kususia kazi kwa ajili ya kupinga ubaguzi katika nyanja tofauti.  

Katika kuelekea kumaliza ubaguzi wa rangi, Baraza la Usalama, mwaka wa 1963, liliweka vikwazo vya hiari vya silaha dhidi ya Afrika Kusini, na Baraza Kuu lilikataa kukubali sifa za nchi hiyo kutoka 1970 hadi 1974. Kufuatia marufuku hii, Afrika Kusini haikushiriki katika shughuli za Baraza Kuu hadi mwisho wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres akizungumza na wanahabari jijini New York, Marekani
UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na wanahabari jijini New York, Marekani

Ni upi msaada wa Katibu Mkuu kwa watu wanaojaribu kutekeleza jambo? 

Chini ya Kifungu cha 99 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja huo "anaweza kuwasilisha kwa Baraza la Usalama suala lolote ambalo kwa maoni yake linaweza kutishia amani na usalama wa kimataifa." 

Jukumu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kama mhusika muhimu wa kuleta amani limebadilika kufuatia uzoefu mwingi. Shughuli mbalimbali zinazofanywa na Katibu Mkuu zimejumuisha kutoa msaada kwa wale wanaojaribu kutekeleza jambo, usuluhishi, uwezeshaji, michakato ya mazungumzo na hata kushirikisha msuluhishi. 

Mojawapo ya majukumu muhimu ya Katibu Mkuu ni matumizi ya (hadi sasa katika historia ya miaka 75 ya Umoja wa Mataifa, Makatibu Wakuu wote tisa wamekuwa wanaume) msaada wake  -hatua zilizochukuliwa hadharani na kwa faragha, kwa kuzingatia uhuru wao, kutopendelea na uadilifu, na uwezo wa diplomasia, kuzuia migogoro ya kimataifa kutokea, kuongezeka au kuenea. 

Kimsingi, hii ina maana Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaweza kutumia mamlaka yake, na uzoefu wake na utaalamu wa kidiplomasia wa timu yake ya juu kukutana na wakuu wa nchi na maafisa wengine na kujadiliana kumaliza mizozo kati ya pande zinazokinzana. 

Mwishoni mwa mwezi Machi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliomba matumizi ya uwezo wake kutoa msaada na kumwomba mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths, , kuchunguza uwezekano wa kusitisha mapigano ya kibinadamu kati ya Urusi na Ukraine, na nchi zingnine zinazotafuta suluhu la amani kwa vita. 

Kwa taarifa zaidi kuhusu vita ya Ukraine tembelea ukurasa wetu maalum.

Fahamu UN na kazi zake kwa lugha ya kiswahili hapa.