Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatma ya Madagascar mashakani kwani watoto 3 kati ya 10 hawahitimu elimu ya msingi

Hatimaye Clarissa amerejea darasani kufuatia juhudi za Mwalimu wake Bi. Fracia Romindo.
UNICEF VIDEO
Hatimaye Clarissa amerejea darasani kufuatia juhudi za Mwalimu wake Bi. Fracia Romindo.

Hatma ya Madagascar mashakani kwani watoto 3 kati ya 10 hawahitimu elimu ya msingi

Utamaduni na Elimu

Nchini Madagascar utimizaji wa lengo la maendeleo endelevu namba 4 la elimu bora bado ni mtihani mkubwa hasa ukizingatia kwamba watoto 3 kati ya 10 hawahitimu elimu ya msingi, limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF.

Clarissa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12 ni miongoni mwa maelfu ya watoto wanaoshindwa kuhuduria shule Madagascar na anasema amelazimika kuwa nje ya shule kwa mwaka mmoja sasa na sababu kubwa baba yake ameshindwa kumnunulia vifaa vya shule vinavyohitajika. 

Kwa mujibu wa UNICEF elimu ya msingi ni muhimu sana kwa ajili ya mustakbali wa mtoto lakini wengi kama Clarissa nchini Madagascar umasikini unawanalazimika kukatiza ndoto zao. 

Mwalimu wake Francia Romindo ambaye ndiye mkuu wa shule aliyokuwa anasoma alijaribu kumsaka Clarissa ili arejee shuleni  kwani ni mtoto mwenye upeo na ndoto kubwa 

Bi. Romindo anasema, “wakati wa usaili tunajaribu kubaini watoto walioacha shule . Kwa sababu mimi ni mkuu wa shule na mwalimu wa Clarissa mara moja nilibaini kwamba jina lake halikuwepo kwenye orodha na ndipo nilipoamua kuzungumza na wazazi wake. Nilimwambia baba yake kama tatizo ni vifaa vya shule tu , basi amlete mtoto shuleni kwani vifaa tunavyo” 

Shule inaweza kumudu kuwasaidia vifaa watoto kama Clarisa kwa sababu ya msaada inaopewa na  UNICEF. Shirika hili pia linasaidia kutoa masomo ya marudio kwa watoto walioacha shule kwa muda mrefu. 

Asante UNICEF baba asilikiziza wito wa mwalimu na sasa Clarissa amerejea shuleni na anasema “ "nina furaha sana , sikutarajia kama ntaweza kurejea tena shuleni. Na sasa niko tayari kusoma ili niweze kufikia malengo yangu ya kuwa mwalimu na kufundisha watoto walio katika mazingira magumu kama yangu.”