UN yazindua mashamba huru bila tumbaku Kenya:FAO/WHO/WFP

Reginald Omulo mkulima ambaye aliachana na kilimo cha tumbaku na kugeukia kulima maharagwe nchini Kenya.
© WHO
Reginald Omulo mkulima ambaye aliachana na kilimo cha tumbaku na kugeukia kulima maharagwe nchini Kenya.

UN yazindua mashamba huru bila tumbaku Kenya:FAO/WHO/WFP

Ukuaji wa Kiuchumi

Mamia ya wakulima kwenye kaunti ya Migori nchini Kenya sasa kuachana na kilimo hatari cha tumbaku na kuhamia kwenye uzalishaji wa mazao endelevu na hasa maharagwe, kupitia mradi wa "Mashamba huru bila tumbaku” uliozinduliwa jana Machi 23 na Umoja wa Mataifa.

Mmoja wa wakulima wa tumbaku wa muda mrefu kwenye kaunti ya Migori ambaye ameshuhudia athari za kiafya zitokanazo na kilimo hicho, lakini sasa kwa msaada wa mafunzo kupitia mradi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ya mashamba hutru bila tumbaku ameanza kilimo cha maharagwe.

Mradi huo ambao umekuwa kwa majaribio kwa muda Kenya, umezinduliwa rasmi jana Machi 23 na ni mradi wa pamoja wa shirika la chakula na kilimo FAO, shirika la afya duniani WHO, shirika la mpango wa chakula duniani WFP na ukiishirikisha serikali ya Kenya.

Reginald Omulo amekuwa mkulima kwlakini baada ya kuelimishwa athari zake sasa ameachana na kilimo hicho, "Tuligundua kwamba tumbaku haikuwa safi hasa kwa familia, kuna magojwa tofautitofauti huja na kilimo cha tumbaku, n ahata vifio vilikuwa vinatokea kwa aina ya ghafla hata huwezi kujua, kuanzia kwa baba wanakufa ghafla, Watoto ambao wamelelewa katika familia hiyo wanaendelea kulina nao wanakufa bure, kwa sababu mfumo wa maisha ni uleule.”

Lakini hiyo sio changamoto pekee inayowakumba wakulima wa tumbaku kama anavyosema Alice Achieng, “Kilimo cha tumbaku kilikuwa na kazi ngumu, wakati wa kulima tumbaku tulikuwa tunaanza mwezi wa kumi hadi mwezi wa nane mwaka unaofuata. Kilikuwa kinanipa kazi ngumu hata watoto wanakuweza kwenda shuleni. Pia kazi ya tumbaku unaanza na kukata miti na matawi unasomba, na ndani ya nyumba ya tumbaku moshi huwa umejaa na unavuta moshi huo, hata kama huvuti tumbaku tayari unavuta moshi”

Kwa kugeukia kilimo cha maharagwe ambacho miongoni mwa wanunuzi wake ni WFP wote Reginald na Alice wameona faida zake na wanatoa wito kwa wakulima wengine kufuata nyayo zao.

Wizara ya afya ya Kenya imeushukuru sana mradi huo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikisema utawasaidia wakulima kuachana na kilimo cha hatari cha tumbaku na kuokoa afya zao na za familia zao, kuwapunguzia gharama za matibabu na kuimarisha uchumi wa familia kwa kuuza maharagwe.

Kenya ni nchi ya kwanza iliyochaguliwa kuanza mradi huo ikichukuliwa kama mdau mkubwa katika mapambano dhidi ya magonjwa yatokanayo na tumbaku.