Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lakataa "azimio la kibinadamu" lililowasilishwa na Urusi

Baraza la Usalama
UN Photo/Manuel Elías
Baraza la Usalama

Baraza la Usalama lakataa "azimio la kibinadamu" lililowasilishwa na Urusi

Amani na Usalama

Baraza la Usalama lililokaa hii leo Jumatano katika kikao chake cha pili cha dharura, halikupitisha rasmu ya azimio lililowasilishwa na Urusi. 

Rasimu hiyo ya azimio haikutaja vita wala jukumu la taifa hilo katika vita hiyo na lilitaka kusitishwa kwa mapigano kwa njia ya mazungumzo na kulaani mashambulizi dhidi ya raia. 

Azimio hilo limepata kura mbili pekee za kuliunga mkono ikiwa ni kura ya Urusi yenyewe na China huku wengine 13 wakiamua kushiriki kufanya maamuzi kwa kutopiga kura na hivyo kuliangusha azimio hilo. Hakukuwa na kura iliyopinga moja kwa moja.   

Katika maelezo yake baada ya upigaji kura, mwakilishi wa kudumu wa Urusi Vassily Nebenzia ameonesha kwamba hatua iliyochukuliwa na wanachama wengine wa Baraza la Usalama ya kutopiga kura ni hatua inayochochewa kisiasa na kwamba kutoidhinishwa kwa azimio hilo bila shaka kunatatiza maisha ya wale wanaosimamia misaada ya kibinadamu nchini Ukraine. 

Mwakilishi wa kudumu wa Urusi katika Umoja wa Mataifa akiwa katika Baraza la Usalama.
Picha ya UN
Mwakilishi wa kudumu wa Urusi katika Umoja wa Mataifa akiwa katika Baraza la Usalama.

 

Bwana Nebezia amesema hatua ya kukataliwa azimio la Urusi, "itaruhusu upande wa Ukraine kuendelea kupuuza matakwa ya kuanzishwa kwa usitishaji vita kwa ajili ya kuwahamisha watu kwenye shoroba za kibinadamu, Kyiv itaendelea kutumia raia kama ngao za binadamu na, kinyume na sheria ya kimataifa ya kibinadamu, Kyiv itaendelea kusambaza silaha nzito karibu na hospitali.” 

Mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield, amehalalisha uamuzi wake wa kutopiga kura dhidi ya azimio hilo kwa kusema kwamba maandishi hayo hayastahili matumizi ya "nguvu yake ya thamani ya kura ya turufu" na kwamba kutoshiriki kwa wajumbe kumi na watatu wa Baraza "ilikuwa kila kitu kilichofanya kushindwa kwa azimio hilo.” 

Balozi wa Marekani Linda Thomas-Greenfield akihutubia Baraza la Usalama.
Picha ya UN
Balozi wa Marekani Linda Thomas-Greenfield akihutubia Baraza la Usalama.

Balozi Greenfield amesema kuwa Marekani ina nia ya kujiepusha na rasimu ya azimio hilo kwa sababu, “kueleza waziwazi, Urusi haijali kuzorota kwa hali ya kibinadamu, au mamilioni ya maisha na ndoto ambazo vita vimesambaratika. Ikiwa wangejali, wangeacha kupigana. Urusi inajaribu kulifanya Baraza hili lishiriki katika upotoshaji wake duni kwa kuweka azimio ambalo halitaji jukumu lake kama sababu pekee ya mzozo huu na kura yetu itaonesha kuwa hatutachukua sehemu yoyote ya hilo, na kuongeza kuwa "Urusi. inaendelea kulizuia Baraza hili kutekeleza majukumu yake." 

"Zaidi. Ninataka kuongeza kwamba hatuhitaji mzaha huu wa azimio la kutoa msaada wa kibinadamu, Marekani imetoa msaada wa kibinadamu wa zaidi ya dola milioni 600 kwa watu wa Ukraine," amefafanua akionesha kuwa nchi yake ingeweza kutoa "msaada wote unaohitajika kwa Ukraine na kwa nchi jirani ambazo zinakaribisha na kusaidia watu wa Ukraine kwa ukarimu."  

Kwa upande wake, mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa kura yake kuhusu rasimu ya azimio hilo ilitokana na wito wake kwa jumuiya ya kimataifa kuweka umuhimu mkubwa kwa hali ya kibinadamu nchini Ukraine, na ili pande zinazohusika "ziimarishe uratibu katika masuala ya kibinadamu, ili kulinda ipasavyo usalama wa raia, hasa wanawake, watoto na makundi mengine yaliyo hatarini, na kuwezesha uondoaji wa wafanyakazi na shughuli za misaada ya kibinadamu."