Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sitisheni vita ili kuruhusu watu kupata njia salama za kuondoka Ukraine – Antonio Guterres

Tarehe 5 Machi 2022 mashariki mwa Ukraine, watoto na familia wakielekea katika mpaka kuvuka kuingia Poland.
© UNICEF/Viktor Moskaliuk
Tarehe 5 Machi 2022 mashariki mwa Ukraine, watoto na familia wakielekea katika mpaka kuvuka kuingia Poland.

Sitisheni vita ili kuruhusu watu kupata njia salama za kuondoka Ukraine – Antonio Guterres

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo Jumapili ametoa wito kusitishwa kwa mapigano ili kuruhusu raia kuondoka maeneo yenye migogoro nchini Ukraine, huku shirika la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu, OHCHR likitangaza kuwa limerekodi vifo vya raia 1,123 tangu kuanza kwa mashambulizi ya silaha ya Urusi nchini humo. 

Kupitia ujumbe mfupi aliouweka katika ukurasa wake wa mtadao wa Twitter, Katibu Mkuu Guterres ameeleza kwamba ni muhimu kabisa kusitisha mapigano ambayo yanaendelea nchini Ukraine, kuruhusu kupita kwa usalama kwa raia kutoka maeneo yote ya migogoro, na pia kuhakikisha kwamba misaasa ya kibindamu kama vile ile inayotoka Umoja wa Mataifa ambayo imeanza kuwasili jana Jumamosi iweze kuingia na kuwasaidia wale waliosalia.  

Tweet URL

Bwana Guterres ametaja miji ya Mariupol, Kharkiv na Sumy kama mifano ya maeneo ambayo ni hatari sana ambapo raia wako katika hatari. Majaribio ya kuruhusu raia wapatao 200,000 kuondoka salama Mariupol yanaendelea kuzuiwa, huku chama cha kimataifa cha hilal nyekundu, ICRC kikiripoti "matukio mabaya ya mateso ya wanadamu" katika jiji hilo. 

ICRC imeripoti leo kwamba wakati timu zao ziko tayari kusaidia katika uhamishaji, zinahitaji dhamana ya usalama ili kufanya kazi. Dhamana hizi hadi sasa hazijapatikana, na shirika hilo limetoa wito kwa pande zinazozozana kukubaliana na masharti maalum ambayo yataruhusu njia salama nje ya jiji.