Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inaonya juu ya kuongezeka kwa tishio la moto wa nyika

Wazima moto huko California na maeneo mengine ya Pwani ya Magharibi ya Marekani wamejitahidi kuzuia moto wa nyika.
San Francisco Fire Department
Wazima moto huko California na maeneo mengine ya Pwani ya Magharibi ya Marekani wamejitahidi kuzuia moto wa nyika.

Ripoti inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inaonya juu ya kuongezeka kwa tishio la moto wa nyika

Tabianchi na mazingira

Moto wa nyika unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 50 ifikapo mwisho wa karne hii kutokana na mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi na mabadiliko ya matumizi ya ardhi. 

 

Hali ya hewa na Mazingira 

Moto wa nyika unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 50 ifikapo mwisho wa karne hii kutokana na mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi na mabadiliko ya matumizi ya ardhi, kulingana na ripoti iliyochapishwa leo na shirila la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira (UNEP) na GRID-Arendal, shirika lisilo la kiserikali ambalo ni kituo cha mawasiliano ya mazingira kilichopo Norway. 

Utafiti huo umegundua kuwa hata maeneo ya Arctic na maeneo mengine ambayo hapo awali hayakuathiriwa na moto wa nyika sasa yanakabiliwa na hatari kubwa. 

Waandishi wa ripoti hiyo wanatoa wito wa mabadiliko makubwa katika hatua za serikali ambazo zinazingatia kuzuia na kujitayarisha kukabili hatari hiyo. 

Moto wa nyika katika picha za setilaiti zikionyesha sehemu za Siberia zinazoteketea
NASA Earth Observatory
Moto wa nyika katika picha za setilaiti zikionyesha sehemu za Siberia zinazoteketea

Msaada na uwekezaji 

Inger Andersen, mkurugenzi mtendaji wa UNEP amesema kwa sasa, pesa mara nyingi huwekwa mahali pasipofaa. "Wale wafanyakazi wa huduma ya dharura na wazima moto walio mstari wa mbele ambao wanahatarisha maisha yao ili kupambana na moto wa nyika wanahitaji kuungwa mkono. Tunapaswa kupunguza hatari ya moto wa nyika uliokithiri kwa kujitayarisha vyema, kuwekeza zaidi katika kupunguza hatari ya moto, kufanya kazi na jumuiya za wenyeji, na kuimarisha dhamira ya kimataifa ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi,”  

Ripoti hiyo, iliyopewa jina la “Kuenea kama Moto wa nyika:Kuongezeka kwa tishio la mioto ya ajabu ya mazingira,” imetolewa kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa kitakachofanyika Nairobi, Kenya, wiki ijayo likihudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi 193. 

Moto wa nyika umezuka kote Queensland na New South Wales nchini Australia.
Queensland Fire and Emergency Services
Moto wa nyika umezuka kote Queensland na New South Wales nchini Australia.

Afya na wanyamapori walioathirika 

Moto wa nyika unaathiri kwa kiasi kikubwa mataifa maskini zaidi duniani, na athari ambazo hudumu kwa muda mrefu baada ya moto huo kupungua na hivyo kuzuia maendeleo maendeleo endelevu na kuzidisha pengo la usawa wa kijamii. 

Moshi kutoka kwa moto wa nyika huathiri moja kwa moja afya za watu, kwa mfano, kusababisha athari za kupumua, moyo na mishipa, wakati gharama ya kujenga upya inaweza kuwa kubwa zaidi ya uwezo wa nchi za kipato cha chini. 

Wanyamapori, pamoja na makazi ya asili, pia hunusurika mara chache. Moto wa nyika umesababisha baadhi ya wanyama na mimea kukaribia kutoweka. Mioto ya nyika ya mwaka 2020 nchini Australia inakadiriwa kuwa iliangamiza mabilioni ya wanyama wa kufugwa na wa porini. 

Uhusiano na mabadiliko ya tabianchi 

Moto wa nyika na mabadiliko ya tabianchi "vinazidisha adha pande zote", kulingana na ripoti hiyo. 

Ripoti imeongeza kuwa "Moto wa nyika unafanywa kuwa mbaya zaidi na mabadiliko ya tabianchi kupitia kuongezeka kwa ukame, joto la hali ya juu, unyevu kiasi kikubwa, umeme, na upepo mkali na kusababisha misimu ya joto zaidi, hali kame na ya muda mrefu ya moto wa nyika," 

"Wakati huo huo, mabadiliko ya tabianchi yanafanywa kuwa mabaya zaidi na moto wa nyika, hasa kwa kuharibu mazingira nyeti na yenye kiwango kikubwa cha hewa ukaa kama vile peatlands na misitu ya mvua. Hii inageuza mandhari kuwa visanduku vidogo, na kuifanya kuwa vigumu kukomesha halijoto inayoongezeka." Imesema ripoti hiyo. 

Ripoti inasisitiza hitaji muhimu la kuelewa vyema tabia ya mioto ya nyika. Kuzuia kunahitaji mchanganyiko wa takwimu na mifumo ya ufuatiliaji inayozingatia sayansi na maarifa asilia, na kwa ushirikiano thabiti wa kikanda na kimataifa. 

Mzima moto akipambana na moto wa msituni
Unsplash/Fabian Jones
Mzima moto akipambana na moto wa msituni

Kichocheo cha moto 

Serikali zinahimizwa kupitisha kinachojulikana kama "Mfumo uliotayari kwa ajili ya moto", ambayo inataka theluthi mbili ya matumizi yatumike katika kupanga, kuzuia, kujitayarisha na kurejesha na theluthi moja kwa ajili ya kukabiliana na moto wa nyika. 

Kwa sasa, hatua za moja kwa moja kwa ajili ya moto wa nyika hupokea zaidi ya nusu ya matumizi yanayohusiana, na chini ya asilimia moja imetengwa kwa ajili ya kupanga na kuzuia,moto huo kulingana na ripoti. 

Waandishi hao wa ripoti zaidi wanatoa wito wa kuwepo kwa viwango imara vya kimataifa kwa ajili ya usalama na afya ya wafanyakazi wa zima moto na kupunguza vitisho vinavyowakabili kazini. 

Hii ni pamoja na kuongeza ufahamu wa hatari za kuvuta pumzi ya moshi, kupunguza uwezekano wa mitego ya kutishia maisha, na kuwapa ufikiaji wa unyevu wa kutosha, lishe, na kupumzika kati ya zamu zao za kazi.