Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ina uwezo wa kuwa mkombozi wa elimu wakati wa majanga:UNESCO

Bango la siku ya Lugha mama
UNESCO
Bango la siku ya Lugha mama

Teknolojia ina uwezo wa kuwa mkombozi wa elimu wakati wa majanga:UNESCO

Utamaduni na Elimu

Leo ni siku ya kimataifa ya lugha ya mama, mwaka huu kaulimbiu ikiwa “Kutumia teknolojia katika kujifunza kwa lugha mbalimbali: Changamoto na fursa”.  

Katika ujumbe wake wa siku hii shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO limesema  teknolojia ina uwezo mkubwa wa kushughulikia baadhi ya changamoto kuu katika elimu zama hizi na inaweza kuharakisha juhudi kuelekea kuhakikisha fursa sawa na jumuishi za kujifunza maisha yote kwa wote ikiwa itaongozwa na kanuni za msingi za ujumuishiaji na usawa.  

 

Mkurugenzi mkuu wa UNESCO Audrey Azouley katika ujumbe wake amesema mfano wakati wa janga la COVID-19 shule zilipofungwa nchi nyingi zilitumia suluhu ya teknolojia ili watoto kuendelea kusoma asilimia 96 ikiwa ni katika nchi za kipato cha juu, lakini kiwango kilikuwa cha chini asilimia 58 pekee katika nchi zenye kipato cha chini. 

 

Lengo kubwa la kaulimbiu yam waka huu ni kuimarisha jukumu la waalimu katika kuchagiza ubora wa kufundisha na kusoma kupitia lugha mbalimbali, lakini pia kuzimulika teknolojia na uwezo wake katika kusaidia ufundishaji na usomaji kupitia lugha mbalimbali.

 

Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imeshinda tuzo ya kimataifa ya Shaaban Robert kwa kukuza msamiati wa lugha hiyo kimataifa.
UNIC/Ahimidiwe Olotu
Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imeshinda tuzo ya kimataifa ya Shaaban Robert kwa kukuza msamiati wa lugha hiyo kimataifa.

Bado kuna pengo katika teknolojia

 

Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni wa UNESCO, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Benki ya Dunia na OECD kuhusu hatua za kitaifa za elimu kwa kufungwa shule wakati wa COVID-19 katika nchi 143, ulionyesha kuwa asilimia 96 ya nchi zenye mapato ya juu zilitoa mafunzo kupitia majukwaa ya mtandao kwa angalau kiwango kimoja cha elimu ikilinganishwa na asilimia 58 pekee kwenye nchi zenye kipato cha chini.

 

Katika muktadha wa mapato ya chini, nchi nyingi ziliripoti kutumia vyombo vya habari vya utangazaji kama vile televisheni asilimia (83%) na redio asilimia (85%) ili kusaidia kuendelea kusoma kwa wanafunzi

 

Kwa mujibu wa UNESCO ni dhahiri, walimu walikosa ujuzi, vifaa na utayari wa kufundishaji kwa masafa ya mbali.

 

Wanafunzi wengi walikosa vifaa muhimu, ufikiaji wa mtandao, walikosa nyenzo masomoyaliyohitajika na vifaa kama vitabu na usaidizi wa kibinadamu ambao ungewaruhusu kusoma kutoka mbali nan je ya maeneo ya shuleni.

 

Zaidi ya hayo, zana za kufundishia na kujifunzia wakiwa mbali, programu na maudhui si mara zote vinaweza kuakisi utofauti wa lugha.