Usinyanyapae watu wenye umri mkubwa kwenye Akili bandia
Sera mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO kuhusu ubaguzi wa uzee katika mifumo ya akili bandia iliyoandaliwa kwa ajili ya huduma za afya, inawasilisha hatua za kisheria, zisizo za kisheria na za kiufundi ambazo zinaweza kutumika kupunguza hatari ya kuzidisha au kuanzisha ubaguzi wa umri mkubwa au uzee kupitia teknolojia hizi.
Teknolojia za akili Bandia (AI) zinaleta mapinduzi katika nyanja nyingi ikijumuisha afya ya umma na dawa kwa wazee ambapo zinaweza kusaidia kutabiri hatari na matukio ya kiafya, kuwezesha ukuzaji wa dawa na mengine mengi lakini kuna wasiwasi kwamba ikiwa hazitadhibitiwa, teknolojia za akili bandia zinaweza kuendeleza ubaguzi wa uzee uliopo katika jamii na kudhoofisha ubora wa afya na huduma za kijamii ambazo wazee hupokea.
Teknolojia za akili Bandia (AI) zinaweza kuboresha afya na ustawi wa watu wazee, lakini tu iwapo ubaguzi wa umri mkubwa au uzee utaondolewa kwenye muundo, utekelezaji na matumizi yao.