Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwepo wa lahaja mpya ya VVU waonesha uharaka wa kushughulikia janga la UKIMWI

Kumbukumbu ya mishumaa kwa wale waliopoteza maisha kwa VVU na UKIMWI, Yerevan, Armenia.
Photo IOM Armenia 2018
Kumbukumbu ya mishumaa kwa wale waliopoteza maisha kwa VVU na UKIMWI, Yerevan, Armenia.

Uwepo wa lahaja mpya ya VVU waonesha uharaka wa kushughulikia janga la UKIMWI

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI, UNAIDS limesema utafiti upya uliochapishwa kutoka nchini Uholanzi umeonesha kuwepo kwa lahaja mpya ya kirusi cha UKWIMI ambacho licha ya kusambaa kwa kasi pia kina madhara zaidi.

Taarifa ya UNAIDS kutoka Geneva, Uswisi imeeleza kuwa watu wanaoishi na aina mpya ya Virusi Vya UKIMWI - VVU hali zao za mwili hudhoofika mara mbili ya kiwango cha kupungua kwa kinga mwili ( CD4), pia wana viwango vya juu vya virusi vya UKIMWI  (kiasi cha virusi kwenye damu) na wanakuwa hatarini kusambaa haraka kwa VVU mara mbili hadi tatu baada ya kugundulika ikilinganishwa na kirusi cha zamani ya UKIMWI.

Utafiti huo, ulioongozwa na Chuo Kikuu cha Oxfords katika Taasisi yake ya  Takwimu, ulikuwa wa kwanza kugundua lahaja ndogo ya B ya virusi. Utafiti huo pia umebaini kuwa lahaja hiyo imekuwa ikisambazwa nchini Uholanzi kwa miaka mingi na inakuwa ikipokea matibabu ya VVU.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Eamonn Murphy amesema watu milioni kumi wanaoishi na VVU duniani kote lakini bado hawapati matibabu, na hivyo kuchochea kuenea kwa virusi hivyo na uwezekano wa kuwepo kwa aina nyingine. 

“Tunauhitaji wa dharura wa kupeleka ubunifu wa hali ya juu wa matibabu kwa njia zinazofikia jamii zenye uhitaji zaidi. Iwe ni matibabu ya VVU au chanjo ya COVID-19, ukosefu wa usawa katika ufikiaji unaendeleza magonjwa ya milipuko kwa njia zinazotudhuru sisi sote.” Amesema Murphy

UKIMWI

Virusi vya UKIMWI  au VVU ndio janga kuu zaidi la wakati huu, inakadiriwa kuwa watu milioni 79 wameambukizwa virusi hivyo, ambavyo bado hakuna chanjo na hakuna tiba. 

Takriban watu milioni 36 wamekufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI  tangu kuanza kwa janga hilo na watu wapya milioni 1.5 wameambukizwa VVU mwaka 2020. 

Kati ya watu milioni 38 wanaoishi na VVU leo, milioni 28 wanatumia tiba ya kuokoa maisha ya virusi vya UKIMWI  tiba inawaweka hai, wenye afya na kuzuia maambukizi ya virusi kwa wengine