Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 10 walipotiwa kufariki dunia kutokana na kimbunga Batsirai, Madagascar 

Kimbunga cha kitropiki, Batsirahi kimeleta uharibifu mkubwa pwani ya mashariki mwa Madagascar.
© WFP/Nejmeddine Halfaoui
Kimbunga cha kitropiki, Batsirahi kimeleta uharibifu mkubwa pwani ya mashariki mwa Madagascar.

Watu 10 walipotiwa kufariki dunia kutokana na kimbunga Batsirai, Madagascar 

Msaada wa Kibinadamu

Kimbunga cha Tropiki kinachofahamika kwa jina Batsirai kilitua kama Kimbunga Kikali sawa na ngazi ya tatu ya nguvu za vimbunga kikipiga kwenye pwani ya mashariki ya Madagascarkilomita 14 kaskazini mwa jiji la Mananjary saa mbili usiku saa za Madagascar mchana mnamo Jumamosi, Februari 5, 2022.  

Kimbunga Batsirai kilipotua katika pwani hiyo kilikuwa na kasi ya upepo ya kilomita 165 kwa saa (165km/h) na mawimbi ya upepo ya hadi kilomita 230 kwa saa (230km/h.) 

“Takriban watu 10 wamefariki, wengine 43,236 wamekimbia makazi yao katika maeneo 180, na takribani shule 211 zimeathirika.” Zimesema taarifa za awali zilizopokelewa kutoka kwa Wakala wa Kitaifa wa Kudhibiti Hatari (BNGRC) nchini Madagascar. 

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA inaeleza kuwa taarifa za awali zinaonesha wilaya zilizoathirika zaidi ni Nosy Varika, Mananjary na Manakara. 

Aidha ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa takwimu hizi zinatarajiwa kuongezeka katika siku zijazo, kwa kuwa taarifa zaidi zinaendelea kupatikana, ikiwa ni pamoja na katika maeneo ambayo bado hayajaripoti kuhusu uharibifu uliosababishwa na Kimbunga Batsirai, ikiwa ni pamoja na wilaya ya Mananjary ambako hakufikiki. 

OCHA inaripoti kuwa upepo na mvua za Kimbunga cha Tropiki, Batsirai zimesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya usafiri, na kuacha baadhi ya maeneo yaliyoathirika zaidi kushindwa kupitika kwa barabara. Takribani barabara 19 na madaraja 17 yamekatika.