Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madagascar yajiandaa kukumbwa na kimbunga Batsiria

Mwanaume akitoa huduma ya usafiri kwa kutumia mkokoteni katika barabara kuu iliyofurika maji wilayani Ilanivato, Antananarivo, Madagascar.
© UNICEF/Rindra Ramasomanana
Mwanaume akitoa huduma ya usafiri kwa kutumia mkokoteni katika barabara kuu iliyofurika maji wilayani Ilanivato, Antananarivo, Madagascar.

Madagascar yajiandaa kukumbwa na kimbunga Batsiria

Msaada wa Kibinadamu

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Madagascar na washirika wake wengine wa misaada ya kibinadamu wanaongeza juhudi za kujitayarisha na Kimbunga Batsirai ambacho kinatarajiwa kuipinga nchi ya Madagascar mwishoni mwa wiki.

Kimbunga hicho ambacho tayari kimepita katika nchi ya Mauritius inahisiwa huenda kikaleta madhara katika taifa la Madagascar ambalo mwezi uliopita wa Januari lilikumbwa na Kimbunga Ana na kuleta madhara ambayo bado athari zake zinaendelea kuonekana kwa wananachi.

Serikali ya Madagascar ikiongoza maandalizi hayo ya kimbunga Batsiria wameanza kupanga timu za uokoaji katika maeneo yanayotazamiwa kuathirika, ndege za kutoa msaada zipo katika hali ya tahadhari pamoja na mahitaji mengine yanayohtajika kusaidia watu.

Kimbunga Kusini mwa Afrika

Nchi za Kusini mwa Afrika tayari zimeathiriwa na dhoruba ya Kimbunga Ana ambacho Kilikuja na upepo mkali, mvua kubwa, na kufanya uharibifu pamoja na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka serikalini, mwezi Januari (2022) takriban watu 131,000 waliathiriwa na kimbunga Ana nchini Madagascar ikiwa ni pamoja na 71,000 kuyakimbia makazi yao.

Kimbunga hicho pia kimeua watu 58 karibu wote wakiwa katika mji mkuu wa Antananarivo ambapo nyumba za asilii zilibomoka, na wengine kusombwa na maporomoko ya ardhi.

Misaada ya kibinadamu

Watoa huduma za kibinadamu waliwasaidia waathirika kwa kuwapatia fedha, chakula, maji, kuwajengea vyoo vya muda na vifaa vya usafi, pamoja na msaada wa uangalizi wa afya za watu walioathiriwa na mafuriko.

Ingawa baadhi ya watu wameanza kurejea makwao, lakini hali inaweza kuwa mbaya tena kutokana na Kimbunga cha Tropiki cha Batsirai.