Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliokuwa wakimbizi nchini DRC wafurahia kurejea nyumbani Burundi  

Mpaka wa Burundi na DR Congo. UNHCR inawasaidia wakimbizi wa Burundi waliokuwa DR Congo kurejea nyumbani.
Screenshot
Mpaka wa Burundi na DR Congo. UNHCR inawasaidia wakimbizi wa Burundi waliokuwa DR Congo kurejea nyumbani.

Waliokuwa wakimbizi nchini DRC wafurahia kurejea nyumbani Burundi  

Wahamiaji na Wakimbizi

Raia 272 kutoka familia 78 wa Burundi waliorejea nchini Burundi kutoka kambi ya wakimbizi ya Lusenda katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwishoni mwa wiki iliyopita wamekaribishwa na wanachi wenzao, serikali na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi ili waanze maisha katika nchi yao waliyoikimbia kwa vipindi tofauti kutokana na hali mbaya ya usalama 

Idadi kubwa kati ya waliorejea walikimbia migogoro ya mwaka 2015 ingawa pia kuna ambao walikuwa na zaidi ya miaka 50 ukimbizini uko DRC baadhi yao wakieleza kuwa waliondoka Burundi mwaka 1972.  

Mkataba wa kimataifa wa wakimbizi, Global Compact on Refugees, ulipitishwa tarehe 17 mwezi Desemba mwaka 2018 na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa baada ya miaka miwili ya mijadala ya kina baina ya UNHCR, nchi wanachama, mashirika ya kimataifa, wakimbizi, mashirika ya kiraia, sekta binafsi na wataalamu. Mkataba huo una maeneo makuu manne nayo ni mosi, kupunguza shinikizo kwa kusaidia nchi zinazohifadhi wakimbizi, pili kuwezesha wakimbizi kujitegema, tatu kusaka mbinu za kuhamishia wakimbizi nchi ya tatu na nne ni kusaidia mazingira ya nyumbani kwao ili waweze kurejea kwa hiari, na hili la nne ndilo limefanyika kwa wakimbizi wa hao wa Burundi waliokuweko DRC. 

Soundcloud

Raia hao wa Burundi kutoka ukimbizini DRC walipokelewa kwenye kituo maalum cha Gihanga ambapo wanapimwa kwanza ugonjwa wa COVID-19 na kisha kupokea misaada ya chakula na pesa ili kuwasaidia kwa angalau miezi cha miezi mitatu. Baada ya saa 48 za mapokezi na uangalizi, waliorejea wanapelekwa katika makao makuu ya wilaya zao ili waweze kurejea kwao kirahisi.

Tunafurahi

“Ninafurahia sana kufika hapa katika nchi ya Burundi. Tangu mwaka 1972 niko katika nchi ya DR Congo.” Anasema Ndikumagenge Jean, mmoja wa waliorejea.  

Raia hao wa Burundi wanasema wito uliotolewa na viongozi wao akiwemo Rais wa Burundi Evariste Ndaishimiye umechangia kuwafanya warejee nyumbani. 

Niyongere Nadine anasema, “tuliona wakubwa wa Burundi walikuja kututembelea wakatuomba kama tunaweza kurundi nyumbani.” 

“Ndio tukasikia mzee wetu (Rais Ndaishimiye) wa huku Burundi ametuita tuje nyumbani ndio tukaona sasa tuje tu nyumbani tuone kama tunaweza kupumzika. Wametupokea vizuri.” Anaeleza Irakoze Vestine. 

Naye Harerimana Francoise anasema, “tulifurahi sana walifika katika kambi ya Lusenda nchini DRC, tukawaona wakatuambia mtoke ukimbizini mrudi kuna amani. Tukafurahi sana kwa kuwa tulisikia hilo neno zuri rais wetu alituma watumishi wake.” 

Jean Cyriaque Grahoun ni Msimamizi wa ulinzi wa UNHCR katika wilaya ya Baraka, Jimboni Kivu Kusini  nchini DRC anasema kuwa, “sababu ya kutorejeshwa makwao mapema kama ambavyo wakimbizi hao wangetaka ni kutokana na ukosefu wa usalama barabarani nchini DRC na anaeleza kuwa wito mkuu wa UNHCR ni kuhakikisha usalama wa wakimbizi.” 

Msafara huu ni wa kwanza kufika Burundi kwa mwaka huu wa 2022 na Burundi imekubaliana na DRC kila wiki kuwarejesha nyumbani wanaohitaji hadi ifikie wakati isiwe tena na wakimbizi wa Burundi. 