TANBATT-5 wasambaza maji kwa wakazi wa Mambéré-Kadéï

20 Januari 2022

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBATT-5 kwenye ujumbe wa umoja huo unaolinda amani nchini humo MINUSCA, kando mwa jukumu lao la ulinzi wa raia wamechukua jukumu la kusambaza huduma za maji safi na salama kwa wakazi wa maeneo  ambako wanalinda amani kama njia mojawapo ya kuimarisha ulinzi wa raia.

Ulinzi wa amani kwa raia na mali zao huenda sambamba na upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii kwa raia wanaolindwa. 

Upatikanaji wa maji safi na salama ni moja ya changamoto kwa wananchi wengi wa mijini na vijijini.

TANBATT – 5 kwa kulitambua hilo imeamua kuwapunguzia machungu wanakijiji huko Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï kwa kuwapelekea maji safi na salama katika eneo lao.

Wakazi wa Kijiji hicho akiwemo Bi Ruth aliishukuru TANBATT 5 kwa huduma hiyo na kuwataka waendelee kuwakumbuka kila inapowezekana.

Utoaji wa huduma ya maji ni moja ya utekelezaji wa majukumu yao kwa jamii wanayoihudumia na hufanya hivyo kila hali inaporuhusu.

 

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter