Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bachelet: Ushiriki wa wanawake katika kuleta amani duniani kote, umekuwa 'mbaya zaidi' baada ya COVID-19 

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Michelle Bachelet alipotembelea Bunia, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC mwezi Januari mwaka huu wa 2020
MONUSCO
Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Michelle Bachelet alipotembelea Bunia, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC mwezi Januari mwaka huu wa 2020

Bachelet: Ushiriki wa wanawake katika kuleta amani duniani kote, umekuwa 'mbaya zaidi' baada ya COVID-19 

Wanawake

Kutokana na COVID-19, hali ya wanawake watetezi wa haki za binadamu na matarajio ya ushiriki kamili wa wanawake katika kujenga amani, imekuwa "mbaya zaidi." Kamishna Mkuu Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Michelle Bachelet amesema leo Jumanne.

Bi Bachelet ameyasema hayo alipokuwa akishiriki katika mjadala wa Baraza la Usalama mahususi kwa ajili ya mada, "Kulinda Ushiriki: Kushughulikia unyanyasaji unaowalenga wanawake katika michakato ya amani na usalama". 

Mkuu huyo wa haki za binadamu amedokeza kwamba, kati ya mwaka 1992 na 2019, ni asilimia 13 tu ya wapatanishiwaliohusika katika michakato mikubwa ya amani duniani kote walikuwa wanawake.  

Kwa upande wa usaidizi, takriban asilimia 1 tu ya ufadhili katika nchi tete au zilizoathiriwa na migogoro huenda kwa mashirika ya kutetea haki za wanawake. 

"Na hiyo ilikuwa kabla ya janga hilo kuanza - na kabla ya wimbi la mizozo inayozidi, mabadiliko ya kisiasa yasiyo ya kidemokrasia na majanga ya kibinadamu yalitawala katika jamii nyingi, na kupunguza zaidi haki za wanawake." Amesema Bachelet. 

Ufuatiliaji wa ukiukaji 

Mnamo 2020, Ofisi ya Kamishna Mkuu (OHCHR) ilithibitisha mauaji 35 ya watetezi wa haki za binadamu wanawake, waandishi wa habari na wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi katika nchi saba zilizoathiriwa na migogoro. Idadi hiyo, ambayo kwa hakika ni ndogo, ilizidi idadi iliyothibitishwa ya mauaji mwaka wa 2018 na 2019. 

OHCHR pia imekusanya taarifa za mifumo ya mashambulizi dhidi ya wanawake wanaofanya kazi kuhusu usawa wa kijinsia; masuala ya afya ya uzazi na na haki; rushwa, haki za kazi na migogoro ya mazingira na ardhi. 

Kwa mujibu wa Bi Bachelet, katika kila eneo, wanawake wamekuwa wakikamatwa na kuwekwa kizuizini; vitisho, unyanyasaji wa kijinsia, na unyanyasaji kupitia kampeni kampeni za kukandamiza wanawake. 

Akielezea "wimbi" hili la changamoto, Kamishna Mkuu Bachelet amesema kwamba jumuiya ya kimataifa lazima "kusukuma nyuma majaribio ya kushambulia, kunyamazisha na kuharamisha haki za wanawake za kutetea haki, kushiriki katika kufanya maamuzi na kutoa maoni yanayopinga."