Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yapongeza hukumu ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia  Syria

(Maktaba) Pramila Patten, Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika mizozo akifungua kikao cha Baraza la Usalama kuhusu wanawake, amani na ulinzi wa amani.
UN Photo/Eskinder Debebe)
(Maktaba) Pramila Patten, Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika mizozo akifungua kikao cha Baraza la Usalama kuhusu wanawake, amani na ulinzi wa amani.

UN yapongeza hukumu ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia  Syria

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono kwenye mizozo, Pramila Patten amekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Juu huko Koblenz, Ujerumani, dhidi ya kanali wa zamani wa Syria Anwar R. kuhusu uhalifu dhidi ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

Patten amesema hukumu hiyo iliyotolewa leo inatoa haki kwa manusura wa Syria ambao wamesubiri kwa muda mrefu kuona watu waliohusika wakichukuliwa hatua katika mahakama ya sheria kwa uhalifu wao dhidi ya ubinadamu.

"Ripoti za mateso katika vituo vya kuweka watu kizuizini vya serikali ya Syria, ambavyo ni pamoja na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, zimekuwa za kutisha,”

Mashirika ya kiraia

Mwakilishi huyo Maalum pia ameyapongeza mashirika ya kiraia na makundi ya waathirika kwa utetezi wao wa kuhakikisha uhalifu wa unyanyasaji wa kingono unafunguliwa mashtaka huko Koblenz.

“Haki ya uhalifu wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro, na uhalifu mwingine wa kimataifa nchini Syria imecheleweshwa sana, lakini tutaendelea kujitolea ili kuhakikisha hakuna haki inayonyimwa.”

Jukumu la serikali na dunia

Mwakilishi Maalum Patten ametoa wito kwa serikali kutumia aina zote za mamlaka walizonazo kuhakikisha waathirika wanapata haki zao kutokana na uhalifu wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro.

“Kutokujali kwa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro sio lazima iwe kanuni. Wakati serikali za kitaifa hazipo tayari au haziwezi kushtaki wahusika wa unyanyasaji wa kijinsia unaohusiana na migogoro ndani ya nchi, mamlaka ya ulimwengu inajukumu la kuhakikisha wanashtakiwa katika.”