Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

PAKISTAN wakamilisha zoezi lakuwasajili wakimbizi wa Afghanistan kieletroniki.

Wakimbizi watoto raia wa Afghanistan wakiwa nje ya shule huko Islamabad. Zaidi ya wakimbizi 3,000 wanaishi eneo hilo
© UNHCR/Roger Arnold
Wakimbizi watoto raia wa Afghanistan wakiwa nje ya shule huko Islamabad. Zaidi ya wakimbizi 3,000 wanaishi eneo hilo

PAKISTAN wakamilisha zoezi lakuwasajili wakimbizi wa Afghanistan kieletroniki.

Amani na Usalama

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR limeipongeza serikali ya Pakistan kwa kukamilisha zoezi kubwa la kupitia na kusajili mpya kwa njia ya kielektroniki wakimbizi wa Afghanistan walioko nchini humo. 

Msemaji wa UNHCR Babar Baloch akiwa mjini Geneva Uswisi amesema zoezi hilo lilitanguliwa na kampeni kubwa ya kutoa uelewa wa umuhimu wa kuwasajili wakimbizi wote na kuweka vituo zaidi ya 40 vya usajili, imekuwa na matokeo chanya kwakuwa zaidi ya wa Afghan Milioni 1.4 wamesajiliwa. 

Miongoni mwa waliosajiliwa ni pamoja na watoto zaidi ya 200,000 ambapo awali walikuwa wanatambulika kupitia usajili wa wazazi wao.

Kadi hizi za kielektroniki zitasaidia upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa urahisi zaidi ikiwemo huduma za elimu, afya na kibenki. 

Zoezi hilo la usajili limekamilika rasmi tarehe 31 Decemba 2021 na tayari vitambulisho 700,000 vimeshatolewa huku zoezi la utoaji wa vitambulisho likiendelea.