WFP imesitisha opereshen El Fasher Sudan kufuatia mashambulizi katika maghala yake

31 Disemba 2021

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, limelazimika kusitisha operesheni zake kwenye jimbo zima la Darfur Kaskazini kufuatia mfululizo wa mashambulizi katoika maghala yake yote matatu kwenye mji mkuu wa jimbo hilo El Fasher. 

Kufuatia taarifa ya shirika hilo iliyotolewa leo usitioshaji wa operesheni hizo utaathiri karibu watu milioni 2 katika eneo hilo mwaka 2022. 

Mashambulizi dhidi ya vituo hivyo vya hifadhi ya WFP yalianza jioni ya tarehe 28 Desemba na uporaji umeendelea hadi asubuhi ya Desemba 30. 

Bidhaa zilizoporwa 

WFP inasema zaidi ya tani 5,00 za chakula zimekuchukuliwa huku mamia ya waporaji wakisambaratisha maghala hayo. 

Akizungumzia uhalifu huo mkurugenzi mtendaji wa WFP David Beasley amesema “WFP imekasirishwa na mashambulizi haya ya kipumbavu na inalaani vikali vitendo vya kuendelea na uporaji wa misaada na uharibifu wa mali zake. Kutokana na hali hiyo, tumelazimika kusimamisha mara moja shughuli za WFP Kaskazini mwa Darfur” 

Bwana Beasley ameongeza kuwa “Wizi huu umewaibia karibu watu milioni mbili chakula na lishe wanayoihitaji sana. Na hatua hii sio tu ni kikwazo kikubwa kwa shughuli zetu kote nchini, lakini pia inahatarisha usalama wa wafanyikazi wetu na kuhatarisha uwezo wetu wa kukidhi mahitaji ya familia zilizo hatarini zaidi.” 

Kwa mantiki hiyo WFP inatoa wito kwa serikali ya Sudan kutoa kwa dharura usalama wa kutosha, kurejesha bidhaa zilizoporwa na kutoa dhamana ili WFP iweze kurejesha operesheni zake kwa usalama huko Darfur Kaskazini. 

Shirika hilo limeongeza kuwa hasara iliyopatikana El Fasher haiwezi kuzibwa tena na na akiba iliyoko nchini Sudan bila kuathiri usaidizi uliokusudiwa kwa watu walio hatarini katika maeneo mengine ya nchi hiyo. 

Jumla ya watu milioni 10.9 nchini Sudan wanahitaji uhakika wa chakula na usaidizi wa kibinadamu ili kujikimu kwa mwaka 2022 

 

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter