UNHCR yaomboleza kifo cha mfanyakazi wake aliyeuawa Ethiopia 

29 Disemba 2021

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limeshtushwa na kifo cha mfanyakazi mwenzao kilichotokea Kaskazini mwa Ethiopia kutokana na machafuko yanayoendelea. 

Akizungumzia kifo hicho mkurugenzi wa UNHCR kanda ya Mashariki , Pembe ya Afrika nae neo la maziwa Makuu Clementine Nkweta-Salami, amesema “Tumeshtushwa sana na pigo hili kubwa la mfanyakazi mwenzetu na tunatuma salamu zetu za pole kwa familia na wapendwa wake” 

UNHCR imetoa wito kwa pande zote katika mzozo kuwalinda raia wakiwemo wahudumu wa misaada , wakimbizi na wale waliolazimishwa kukimbia makwao na wawalinde kwa kuzingatia wajibu wao chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu.  

Mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa “Ni muhimu sana kukomesha mgogoro huo wa Ethiopia ambao umesababisha machungu makubwa kwa binadamu, kupoteza maisha ya watu na kufanya mamilioni ya watu kulazimika kutawanywa.” 

Shirik la UNHCR linaendelea kufanyakazi na wadau ili kuhakikisha kwamba wakimbizi na wakimbizi wa ndani nchini Ethiopia wanapata msaada wanaouhitaji. 

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter