Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UN afanya ziara nchini Lebanon

Katibu Mkuu wa UN António Guterres wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Rais wa Lebanon, Michel Aoun mjini Beirut.
UN Photo/Eskinder Debebe)
Katibu Mkuu wa UN António Guterres wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Rais wa Lebanon, Michel Aoun mjini Beirut.

Katibu Mkuu wa UN afanya ziara nchini Lebanon

Ukuaji wa Kiuchumi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewataka viongozi wa Lebanon kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua migogoro iliyopo nchini humo, huku akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuimarisha kuiunga mkono Lebanon kutokana na matatizo yake ya sasa.

Wito huu ulikuja wakati wa mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari uliofanyika katika Ikulu ya Rais nchini Lebanon, mkutano ambao Rais wa Lebanon Michel Aoun amem amesemwa umekuwa  "wenye matunda".

Katika mkutano huo Katibu Mkuu Guterres amewaambiwa waandishi wa habari “Nimekuja Lebanon na ujumbe mmoja rahisi, Umoja wa Mataifa unasimama kwa mshikamano na watu wa Lebanon.”

Ziara hiyo inalenga kujadili njia bora za kuwasaidia watu wa wa nchi hiyo kuondokana na mgogoro wa sasa wa kiuchumi na kifedha na kukuza amani, utulivu na maendeleo endelevu. 

Wafanyakazi wa ndani wahamiaji  nchini Lebanon wamepoteza ajira zao
IOM/Muse Mohammed
Wafanyakazi wa ndani wahamiaji nchini Lebanon wamepoteza ajira zao

Wakimbizi wa Syria

Katika hotuba yake  ya kumkaribisha, Rais Aoun alisema kuwa mkutano wao umegusia suala la wahamiaji wa Syria na kwamba amemwambia Katibu Mkuu wa UN  kuwa “Kuna haja ya kutafuta mbinu mpya ya suala la Wasyria waliokimbilia nchini Lebanon," akibainisha kuwa mgogoro huu umekuwa ukiendelea na kuongezeka kwa zaidi ya miaka 10, na umekuwa mzigo mkubwa kwa Lebanon hasa katika hali inayolikabili taifa hilo hivi sasa.

Rais wa Lebanon alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua majukumu yake na kuhimiza kuwarejesha salama wakimbizi hao katika vijiji na nchi yao.

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Antonio Guterres amekiri kwamba “Jumuiya ya Kimataifa haijafanya vya kutosha kuiunga mkono Lebanon, kuiunga mkono Jordan, na kuzisaidia nchi nyingine duniani ambazo zimefungua mipaka, milango na mioyo yao kwa wakimbizi, huku kwa bahati mbaya baadhi yamataifa Tajiri zaidi na wenye nguvu zaidi yakifunga mipaka yao wenyewe."

Uchaguzi Lebanon

Lebanon imepanga kufanya uchaguzi wa wabunge mapema mwakani 2022.

Akizungumzia uchaguzi huo Katibu Mkuu alisema uchaguzi wa mwakani ni muhimu na kwamba  "Watu wa Lebanon lazima washiriki kikamilifu katika kuchagua jinsi nchi inavyosonga mbele."

Pia alisisitiza umuhimu wa makundi yote ya jamii kuwakilishwa "Wanawake na vijana lazima wapate kila fursa ya kutekeleza sehemu yao kikamilifu wakati Lebanon inapojitahidi kushinda changamoto zake nyingi na kuweka msingi wa maisha bora ya baadaye."

"Na Umoja wa Mataifa utaiunga mkono Lebanon katika kila hatua ya safari hii," alisisitiza Katibu Mkuu.