Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji yasisitiza kuzingatia uwezo wao

Tangu kuzuka kwa COVID-19, wakimbizi wahamiaji wa Venezuela wamekabiliwa na changamoto nyingi nchini Colombia.
PAHO/Karen González
Tangu kuzuka kwa COVID-19, wakimbizi wahamiaji wa Venezuela wamekabiliwa na changamoto nyingi nchini Colombia.

Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji yasisitiza kuzingatia uwezo wao

Haki za binadamu

Leo ni siku ya Kimataifa la Wahamiaji chini ya kauli mbiu “Kutumia uwezo wa uhamaji wa kibinadamu”. Umoja wa Mataifa unaangazia mafanikio yaliyopatikana kutokana na uhamiaji na kutoa wito wa kulindwa haki zao katika dunia yenye wahamiaji milioni 281 wa kimataifa. 

Katika ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kwa siku hii amesisitiza kuwa mshikamano na wahamiaji haujawahi kuwa wa dharura hivi. Dunia inahitaji ushirikiano wenye ufanisi zaidi na mtazamo wa huruma zaidi wa uhamiaji.

“Leo, watu wengi zaidi kuliko wakati mwingine wowote wanaishi katika nchi nyingine isipokuwa ile walikozaliwa. Ingawa watu wengi wanahama kwa kupenda, wengine wengi huondoka nyumbani kwa lazima.”

Takwimu

Tafiti zinaonesha kuwa sababu kuu za kuondoka katika nchi ya asili ni majanga, changamoto za kiuchumi, umaskini uliokithiri na migogoro.

Takriban watu milioni 281 walikuwa wahamiaji wa kimataifa mwaka 2020, wakiwakilisha asilimia 3.6 ya watu duniani.

Katika ujumbe wake, António Guterres alisema wale walio katika hatua hiyo "wanaendelea kukabiliwa na unyanyapaa ulioenea, ukosefu wa usawa, chuki dhidi ya wageni na ubaguzi wa rangi. Wanawake na wasichana wahamiaji wanakabiliwa na hatari kubwa ya unyanyasaji wa kijinsia na wana chaguzi chache za kutafuta msaada".

Pamoja na mipaka kufungwa kwa sababu ya janga hili, Bw. Guterres alikumbuka kwamba wahamiaji wengi wamekwama bila mapato au makazi, hawawezi kurudi nyumbani, kutengwa na familia zao, na wanakabiliwa na mustakabali usio na uhakika.

Wahamiaji katika kituo cha kuzuiliwa cha mji wa Zawiya nchini Libya
Photo: Mathieu Galtier/IRIN
Wahamiaji katika kituo cha kuzuiliwa cha mji wa Zawiya nchini Libya

Covid-19

Miongoni mwa masuala yanayozingatiwa zaidi ni usimamizi wa mipaka wa kibinadamu, kuheshimu haki za binadamu na mahitaji ya kibinadamu, na kuhakikisha kwamba wahamiaji wanajumuishwa katika mipango ya kitaifa ya chanjo ya Covid-19.

"Bado katika janga hili, wahamiaji wameboresha jamii kila mahali na mara nyingi wako kwenye mstari wa mbele katika kusaidia kipindi cha majanga , mfano wanasayansi, wataalamu wa afya na wafanyakazi katika idara muhimu".

Kuwapinga wahamiaji

Mwaka huu, Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji inaadhimishwa takriban miaka 70 tangu mkutano wa kihistoria wa Brussels uliopelekea kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM).

Katika ujumbe wake, Mkurugenzi Mkuu wa IOM, António Vitorino, alikumbuka picha kali za mipaka iliyofungwa na familia zilizotenganishwa, huku kukiwa na msukosuko wa kiuchumi unaotokana na janga la COVID-19, ambazo zimekuwa za kawaida zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Vitorino amesema janga hilo la ulimwengu pia limezua wimbi jipya la chuki dhidi ya wahamiaji na kuongezeka kwa utumiaji wa wahamiaji kama njia za kisiasa.

"Yote wawili hawakubaliki," Bw. Vitorino alisema. Kwake, majibu ya janga hili pia yamesisitiza umuhimu wa wafanyakazi wahamiaji katika kuweka kila mtu salama.

" Kuna athari chanya za kijamii na kiuchumi katika nchi wanamoishi, jumla ya dola bilioni 540 zilizotumwa mwaka jana 2020 kwa jamii katika nchi za kipato cha chini na cha kati, kiasi hicho kinaonesha ni namna gani wanaweza kusaidia kwenye masuala ya ujasiriamali na jamii yote ikanufaika.”

Namna ya kunufaika na Wahamiaji

Mkuu wa IOM alisema kuwa ili kutambua uwezo kamili wa uhamaji wa binadamu, mambo mawili lazima yatokee.

Kwanza, serikali lazima zihama kutoka kwa maneno hadi kwa vitendo na kujumuisha wahamiaji bila kujali hali zao za kisheria, katika mipango yao ya kufufua mataifa yao kijamii na kiuchumi.

Pili, lazima waimarishe njia za kisheria za uhamiaji unaoheshimu uhuru wa kitaifa na haki za binadamu za watu wanaohama.

"Mtazamo wa kina unahitaji kwamba tuache kando mkao wa kujihami ambao mara nyingi huwaathiri watu katika safari zao za uhamaji", Bw. Vitorino alisema.