Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UN apokea tuzo ya Taa ya Amani

Katibu Mkuu apokea tuzo ya Taa ya Amani. Tuzo hii, iliyotolewa na Kanisa Takatifu la Watawa la Assisi, nchini Italia, inalenga kuwaenzi wale wanaofanya kazi ya kuendeleza amani na upatano.
UN News
Katibu Mkuu apokea tuzo ya Taa ya Amani. Tuzo hii, iliyotolewa na Kanisa Takatifu la Watawa la Assisi, nchini Italia, inalenga kuwaenzi wale wanaofanya kazi ya kuendeleza amani na upatano.

Katibu Mkuu wa UN apokea tuzo ya Taa ya Amani

Amani na Usalama

•    Asema katika ulimwengu ambao tunaweza kuchagua chochote, tuchague amani.
•    Ahamasisha diplomasia ya Amani 
•    Ashukuru kazi kubwa inayofanywa na wafanyakazi wa UN duniani kote

Katibu Mkuu António Guterres alipokea tuzo ya Taa ya Amani hii leo nchini Italia, ikiwa ni Tuzo ya heshima kubwa kutoka kwa Kanisa Katoliki, ambapo amesema linatambua kazi inayofanywa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa "kupigania amani duniani kote".

Akipokea tuzo hiyo Guterres alishukuru na kukumbusha maafa baada ya Vita vya Kidunia katika Karne ya 20, "Umoja wa Mataifa - UN iliundwa kwa jina la amani", akithibitisha kwamba tumeungana hapa leo katika harakati zetu za kutafuta amani". Amani inasalia kuwa nyota yetu inayoongoza na lengo la thamani zaidi”.

Mtu wa Imani

Taa ya Amani ya Wafransisko ni mfano wa taa ya glasi ya mafuta ambayo inawaka kwenye kaburi la watawa la Mtakatifu Francis wa Assisi, ambaye, katika maisha yake yote, alivutiwa na uongozi wa kujali  maadili ya mazingira.

Tuzo hiyo ilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1981 na waliopewa tuzo hiyo hapo awali ni pamoja na Papa John Paul II, Dalai Lama, Mtakatifu Teresa wa Calcutta na kiongozi wa zamani wa Soviet Mikhail Gorbachev.

“Kama mtu wa imani mwenye shukrani na heshima kubwa kwa utume wa Mtakatifu Francis, tuzo na sherehe hii ni ya maana sana”, alisema mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.

Kuhamasisha Amani

Tangu kuanza kwa muhula wake wa kwanza, Katibu Mkuu wa UN ameweka uendelezaji wa amani kuwa kipaumbele chake kikuu.

Pnegine hii imekuja kufuatia kitendo cha yeye kushuhudia baadhi ya athari mbaya zaidi za migogoro wakati wa utumishi wake akiwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi, ambapo alizindua lizindua "kuongezeka kwa diplomasia kwa amani".

Akizungumza kwa njia ya video wakati wa kupokea tuzo hiyo alisema “Ninaweka mkazo zaidi katika kuzuia, kuanzisha mifumo na kuweka mifumo madhubuti zaidi ya kuchanganua hatari, kuimarisha ufanyaji maamuzi na kuunga mkono nchi wanachama kuchukua hatua kabla ya ghasia kuongezeka.” 

Aliongeza kuwa “COVID-19 iliposhika kasi, nilielewa kuwa itakuwa tishio jipya kwa amani na nikatoa wito mara moja kusitishwa kwa mapigano duniani kote ili kupigana na adui yetu  sote – virusi”. 

Kuangalia mbele

Majukumu ya Katibu Mkuu wa UN ni pamoja na kufanya kazi kama dalali mwadilifu, mjenzi wa madaraja na mjumbe wa amani, na Guterres amedhamiria kutumia ofisi hizo nzuri kuendeleza mipango hiyo.

"Lakini mapambano ya amani mara nyingi ni kazi ya isiyoisha kutokana na utata wa migogoro ya leo ambayo imeunganika . Tunaishi katika ulimwengu ambao hakuna amani, na tupo chini ya matishio makubwa."

Bw. Guterres alitoa taswira  halisi ya nchi na maeneo yanayokumbwa na migogoro na maeneo ambayo mara kwa mara amani haithaminiwi na kudhoofishwa, na kusisitiza kwamba nyakati kama hizi ni muhimu zaidi "kuheshimu amani, na kutafakari wajibu wetu wa kuilinda na kuiendeleza".

Mahitaji ya amani

Kwa sababu lengo sio kukubali tu hali iliyopo bali ni kitendo halisi, kuna wakati mwingine Amani ni chaguo gumu, amesema afisa huyo Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kubainisha kuwa kuna wakati “ Amani inatudai.” 
"Lakini katika ulimwengu wetu uliovunjika na wenye matatizo, ni muhimu sana. Ni pekee. Inasalia kuwa nguvu inayosukuma kazi ya Umoja wa Mataifa, kila siku, katika kila nchi”,
aliongeza.

Akinukuu waraka wa Papa Francis, Fratelli Tutti, Katibu Mkuu alikariri kwamba ni kwa kutembea tu katika njia ya amani, kwa mshikamano, tunaweza kujenga mustakabali mwema kwa wote, "kwa sababu amani inaweza kufikia maajabu ambayo vita haitawahi".

"Katika ulimwengu ambao tunaweza kuchagua chochote, tuchague amani", alihitimisha.