Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kimbunga Rai au Odette chasababisha madhara Ufilipino, mashirika ya misaada yanajipanga

Picha ya maktaba ikimwonesha mtoto mvulana akivuta mzigo wake katika maji baada ya kimbunga.
© ADB
Picha ya maktaba ikimwonesha mtoto mvulana akivuta mzigo wake katika maji baada ya kimbunga.

Kimbunga Rai au Odette chasababisha madhara Ufilipino, mashirika ya misaada yanajipanga

Msaada wa Kibinadamu

Baada ya kutua kwa mara ya kwanza huko Siargao, Surigao del Norte jana tarehe 16 Desemba, Kimbunga Rai (kinachoitwa Odette nchini humo), leo Desemba 17 kimepitia katika baadhi ya maeneo ya kusinimagharibi mwa Ufilipino kikiwa na upepo wa kasi ya kilomita 155 kwa saa, na karibia  upepo mkali wa hadi kilomita 235 kwa saa katika kitovu chake.  

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA kwa kushirikiana na mamlaka za Ufilipino pamoja na mashirika mengine ya misaada wanaendelea kufanya tathmini na kuweka mazingira mazuri ya kusaidia watu.  

Kimbunga hicho kimeleta mvua kubwa, upepo mkali, maporomoko ya ardhi na mawimbi ya Dhoruba na kusababisha maporomoko ya ardhi tisa katika  majimbo saba.   

Tathmini za awali zinaonesha mafuriko, kufungwa kwa barabara, kukatika kwa umeme na kukatika kwa mawasiliano. Mafuriko yanaripotiwa hadi Lanao Del Sur, kama vile katika jiji la Marawi. 

“Pia kuna hatari ya wastani hadi kubwa ya mawimbi ya dhoruba ya urefu wa hadi mita 3.0 katika saa 24 zijazo ambayo inaweza kusababisha mafuriko ya kutishia maisha katika maeneo ya tambarare ya pwani ya Mikoa ya Negros, Iloilo, Antique, Guimaras, na maeneo kadhaa. katika sehemu ya kaskazini ya Palawan. Rai inatarajiwa kuondoka katika Eneo la Wajibu la Ufilipino tarehe 18 Desemba.” Imeeleza taarifa iliyosambazwa na OCHA. 

Watoto wataathirika – UNICEF 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF lilielezea wasiwasi wake hapo jana Alhamisi kuhusu hatima ya watoto nchini Ufilipino wakati Kimbunga huu wa kimbunga Rai/Odette.  

"Mamilioni ya Wafilipino, takriban 700,000 kati yao wakiwa watoto walio katika mazingira hatarishi, wanakabiliwa na vitisho kama vile upepo mkali, mvua kubwa, mafuriko, maporomoko ya ardhi, kuhama makazi na hatari ya kupoteza maisha, makazi, riziki na kilimo." ilisema UNHCR