Visa vipya vya COVID-19 vyapungua duniani: WHO

Nchi barani Afrika zinapata chanjo kupitia Kituo cha COVAX.
WHO
Nchi barani Afrika zinapata chanjo kupitia Kituo cha COVAX.

Visa vipya vya COVID-19 vyapungua duniani: WHO

Afya

Ripoti mpya ilitolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kuhusu janga la COVDI-19 inaonesha matukio ya kila wiki ya visa vipya vya wagonjwa yamepungua kwa asilimia 5 na vifo vinavyohusiana na janga hilo vikipungua kwa asilimia 10 katika wiki ya kuanzia tarehe 6 mpaka 10 Desemba 2021.

Pamoja na kupungua huko lakini bado kuna kesi mpya za wagonjwa wa Corona zaidi ya milioni 4 zilizothibitishwa na vifo vipya chini ya 47,000. 

Kanda ya Afrika imeripoti ongezeko la asilimia 111 la kesi mpya kwa wiki iliyopita na hadi kufikia Desemba 12, mwaka huu kulikuwa na karibu kesi milioni 269 zilizothibitishwa na karibu vifo milioni 5.3 vimeripotiwa ulimwenguni kote.

kusoma ripoti nzima bofya hapa