Bila usawa wa chanjo kwa wote COVID-19 itaendelea kuwa mwiba:Bachelet

8 Disemba 2021

Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu Michelle Bachelet amesema kutokuwepo kwa usawa wa chanjo ya COVID-19  si haki na ni kinyume na maadili.

Akizungumza hii leo kwenye semina maalum mjini Geneva inayoangalia changamoto, maendeleo na fursa za chanjo ya COVID-19 amesisitiza kuwa “Hakuna aliye salama hadi pale kila mtu atakapokuwa salama na kukosekana kwa usawa wa fursa ya chanjo kwa watu wote hivi sasa kunaongeza muda wa kuendelea kwa janga la COVID-19 .

Janga hili ni mgogoro wa kimataifa na linahitaji mshikano na hatua za kimataifa.: 

Ameongeza kuwa na watu wanaoathirika zaidi ni wale wanaokabiliwa na ubaguzi wa kimfumo na pengo la usawa ndani ya nchi na ndani ya jamii zao. 

Takwimu za chanjo

Kamishina mkuu amesema kimataifa fursa ya kupata chanjo ya COVID-19 haina usawa jambo ambalo linasikitisha, ameongeza kuwa hadi kufikia Desemba 1 mwaka huu ni asilimia 8% pekee ya watu wazima ndio waliopata chanjo dhidi ya COVID-19 katika nchi za kipato cha chini ikilinganishwa na asilimia 65% katika nchi cha kipato cha juu. 

Amesema hii ni hali isiyokubalikam hata kidogo. Amekumbusha kwamba “Ongezeko jipya la maambukizi ya COVID-19 na kuzuka kwa aina mpya ya virusi vya Omicron vinauwezekano mkubwa wa kujitokeza miongoni mwa watu wasiopata chanjo ambapo ni tishio kubwa kwa kila mtu.” 

Amesema kutrokana na mwenendo wa sasa wa chanjo kuna uwezekano mkubwa malengo ya shirika la afya duniani WHO ya kutaka asilimia 40% ya watu wote duniani kupata chanjo kamili ifikapo mwisho wa mwaka 2021 itakuwa changamoto kubwa kufikia na lengo la kuchanja asilimia 70% ifikapo katikati yam waka 2022 liko mashakani na katika tishio kubwa.” 

Ameonya kwamba kwa kutoweza kutimiza malengo hayo “Matokeo yake yatakuwa ni vifo vingi vinavyoweza kuepukwa na ulemavu wa muda mrefu wa COVID-19 ambao hadi sasa haujafahamiaka vizuri.” 

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet
UN Photo/Antoine Tardy
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet

Chanjo ni kwa faina ya umaa wa dunia 

Bi. Bachelet amehimiza kwamba chanjo dhidi ya COVID-19 ni kwa ajili ya faida ya umma “TunNjia zote zinahitaji kufanyiwa tathimini ili kupanua wigo wa uwezo wa upatikanaji wa chanjo , kama vile utoaji leseni wa hiyari na kuhamisha teknolojia lakini pia kulegeza masharti ya vitu kama haki miliki ya chanjo.” 

Pia amesema hatua hizo lazima ziharakishwe ili kupiga jeki uwemo wa COVAX kwa ajili ya kuzisaidia nchi za kipato cha chini na za kipato cha kati. 

Kuhusu nchi kuanza hatua ya ulazima wa watu lupata chanjo Kamishina Mkuu amekumbusha kwamba “Ni muhimu kufikiria athari za hatua hiyo. Haki za binadamu hazizuii mamlaka ya  kulazimisha chanjo, lakini zinaweka mipaka mikubwa juu ya lini na jinsi mamlaka hizo zinavyotumika.” 

Bi. Bacheletet ameongeza kwamba “Kwanza, ninataka kusisitiza kwamba upatikanaji wa chanjo na kwa gharama nafuu ni muhimu kwa sera yoyote inayofanya chanjo kuwa za lazima, hadi pale watu wote watakapopata chanjo, mahitaji ya chanjo hayataambatana na haki za binadamu. Chini ya masharti haya, inaweza kukubalika kuweka masharti ya utekelezaji wa haki na uhuru fulani kama vile ufikiaji wa shule au maeneo ya umma kwa chanjo. Lakini, katika hali yoyote hakuna mtu anayepaswa kupewa chanjo kwa nguvu. Kukataa kwa mtu kufuata sera ya chanjo ya lazima kunaweza pia kuhusisha matokeo mengine ya kisheria, ikiwa ni pamoja na, kwa mfano, faini zinazofaa. Pale ambapo adhabu zinatolewa, zinapaswa kuwa sawia na kuchunguzwa na mamlaka za mahakama.” 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter