Skip to main content

Kenya tuna mengi ya kujivunia na expo2020 ni fursa ya kuyaonesha:Macheso

Banda hili katika maonesho ya Dubai, Dubai Expo 2020 limepatiwa jina banda la fursa. Kila jambo linawezekana.
Expo 2020 Dubai/Suneesh Sudhakaran
Banda hili katika maonesho ya Dubai, Dubai Expo 2020 limepatiwa jina banda la fursa. Kila jambo linawezekana.

Kenya tuna mengi ya kujivunia na expo2020 ni fursa ya kuyaonesha:Macheso

Ukuaji wa Kiuchumi

Maonesho ya kimataifa au Expo2020 ambayo mwaka huu yanafanyika Dubai katika nchi za Falme za Kiarabu au Emarati ni fursa nzuri ya washiriki kutoka kila pembe ya dunia kunadi uwezo wao katika Nyanja mbalimbali iwe kilimo, biasahara, nishati, teknolojia na kadhalika lengo likiwa kuvutia fursa za kibiashara, ushirikiano, utalii  na hata uwekezaji.

Kwa sababu ya janga la COVID-19 lililoikumba dunia mwishoni mwa mwaka 2019 mwaka jana 2020 mashindano hayo ya kila mwaka hayakufanyika yaliahirishwa hadi mwaka huu kuanzia  1 Oktoba 2020 na yataendelea hadi Machi 31  mwaka 2022. Nchi 192 zinashiriki maonesho hayo  na miongoni mwao ni Kenya.

Austin Machezo ana kibarua kikubwa katika banda la maonesho la Kenya mjini Dubai cha kuhakikisha kila anayepita kwenye banda hili miongoni mwa wageni milioni 2.3 wanaotembelea maonesho haya kwenye ukumbi wa Al Wasl Plaza anaondoka na kumbukumbu kuhusu Kenya.

Lakini ni kwa nini imekuwa muhimu kwa Kenya kushiriki maonesho haya? Macheso anaeleza 
“Katika hili banda la Kenya tuna maonesho mbalimbali lakini cha muhimu zaidi tunataka kuonesha ule uwezo ambao Kenya imezingatia katika kilimo, katika jamhuri yetu ya Kenya tuko na bidhaa mbalimbali za mimea ambazo tunakuza , tunayo majani ya chai, ambapo tunashikilia nafasi kubwa katika ulimwengu wa kuzalisha chai na tuna masoko mengi ambako tunauza chai kama Uingereza na hapa Uarabuni, tuko na mimea mingine pia kama mkonge ambao unatumika kutengeneza vitu kama dashbodi za magari, halafu kuna matunda ambayo yanaitwa maparachichi, Kenya ina nafasi kubwa katika kuzalisha matunda hay ana kuuza katika soko la nje. Sana sana tunauza hapa katika soko la Uarabuni na Ulaya pia. Halafu zao la muhimu sana pia ni kahawa ambayo tunazalisha kwa wingi sana , na ubora wake wa viwango umetambulika duniani pote  na Kenya iko vizuri sana katika kuzalisha bidhaa za kilimo” 

Kwa mujibu wa Macheso kilimo sio silaha pekee kwani ubunifu Kenya haijabaki nyuma “Kwenye hili bamba la Kenya kuna yale maonesho pia ya ubunifu, tunataka kuonyesha mchango wa Kenya katika hilo hasa kuboresha wafanyabiashara. Kuna ubunifu wa teknolojia inayohusiana na ukulima agri-tech, kuna teknolojia zinazohusiana na wafunzi na shule tunaita Edu-tech na kuna zile za tunazoziita Filied-tech ambazo sana sana wakenya wanatumia kwa usambazaji wa fedha. Halafu Kenya ni nchi inayotambulika sana kwa mambo ya uzalishaji wa umeme , tunashikilia nambari moja katika uzalishaji umeme wa kutumia miale ya jua yaani sola, kuna shamba kubwa la uzalishaji wa paneli za sola liko Garissa , na pia ndio kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati. Halafu Kenya pia kunai le nishati ya mvuke wa joto, Kenya inashikilia nafasi ya pili baada ya Marekani. Hivyo hivi ni baadhi ya vitu ambavyo tuko hapa kuonyesha na kuuambia ulimwengu kwamba Kenya ni nchi ambayo imeboresha mambo mengi ili kuchangia katika maendeleo endelebvu.” 

Na kuhusu sekta ya viwanda na masuala ya mioundombinu Macheso anahakikisha washiriki wa maonesho wanalitambua hilo
“Tunaonyesha wageni wetu pia kwamba Kenya imechukua hatua katika uongezaji wa thamani ya bidhaa katika uzalishaji. Katika Kanda ya Afrika Mashariki na Kati Kenya inashikilia nafasi ya kwanza kwa sekta ya viwanda na uzalishaji. Pia tunaonyesha wageni wetu zile hatua ambazo zimechukuliwa na serikali yetu kutengeneza miundombinu, kama vile barabara na bandari ambazo zinasaidia sana kuimarisha uchumi wa Kenya.” 
Pamoja na yote hayo Kenya ni maarufu sana kwa utalii vipi kuhusu hili? “Katika ile sekta ya utalii tunaonyesha picha ambazo zinaangazi sana mbuga zetu za wanyama ambazo tuko nazo nyingi sana kama bvile Maasai Mara, Amboseli ndio watalii wajionee , waje kutembelea Kebnya yet una kujionea wenyewe mbuga zetu za wanyanma. Pia tunataka kuwaambia ulimwengu ni uwezo gani haswa Kenya uko naokwa kuzalisha bidhaa na pia kutumia hii fursa kutafuta soko, kwa sababu tuna bidhaa nyingi ndio tunauza hapa lakini hatuuzi sana, na lengo letu sio hapa tu bali jumuiya yote ya nchi za Kiarabu.” 

Emarati ndio nchi ya kwanza Mashariki ya Kati, Afrika na Ukanda wa Asia Kusini kuwa mwenyeji wa maonesho haya ya kiamtaifa.