Siku ya choo ikiadhimishwa leo watu bilioni 3.6 hawana huduma hiyo duniani:UN

19 Novemba 2021

Leo ulimwengu ukiadhimisha siku ya choo duniani, takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kwamba watu bilioni 3.6 bado wanakosa huduma hiyo muhimu ya kujistiri na usafi ndio maana maudhui yam waka huu ni “kuthamini vyoo” lengo likiwa kuichagiza dunia na wadau wote kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa kila mtu kila mahali. 

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa miongoni mwa waathirika wakubwa wa kukosa huduma za vyoo ni watu wanaoishi katika nchi masikini na hivyo inazihimiza serikali na wadau wengine wa maendeleo kuwekeza zaidi katika miradi na huduma za msingi kwa wasiojiweza ikiwemo huduma ya vyoo ili kutimiza lengo namba sita la maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030. 

Miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na huduma ya vyoo ni Kidemokrasia ya Congo DRC katika maeneo yanayokumbwa na machafuko hasa Mashariki mwa nchi hiyo ikiwemo mji wa Goma ambako kuna idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani kutokana na vita na mabadiliko ya tabianchi. 

Wakimbizi hao wamekuwa wakilalamikia ugumu wa maisha na changamoto ya vyoo katika makambini. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa huduma za usafi wa mazingira, kujisafi na maji (WASH) ni muhimu sana hasa katika maeneo yaliyo na mikusanyiko ya watu ili kuepusha magonjwa ya kuambukia ambayo athari zake ni mbaya.  

Mapenduo furaha  mmoja wa wakimbizi wa ndani kambini hapo anasema “Tunaishi katika hali mbnaya sana hapa kambini, tuko familia katribu elfu mbili na zaidi tunataabika sana kuhusu huduma ya choo, vyoo ni vichache na sisi wote tunatumia hivyo. Sisi wanawake tunaweza pata magonjwa maambukizi yanatusumbua, wengine yamewathiri hata uzazi, ndio maana tunaomba Umoja wa Mataifa utusaidie kujenga vyoo na dawa za kumwaga chooni ili tuwe na amani kidogo, wakati mwingine baadhi ya wanaume wanaweza kukimbia wanawake kwa sababu ya hali mbaya wanaondoka kwa sababu hakuna jinsi wanaweza kuishi katika nyumba za mazingira haya.” 

Wanafunzi wa Kikosi cha Afya wakiwa nje ya vyoo vya Shule ya Msingi ya Dikolelayi iliyoko Kananga, jimbo la Kasai-Occidental, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
© UNICEF/Vincent Tremeau
Wanafunzi wa Kikosi cha Afya wakiwa nje ya vyoo vya Shule ya Msingi ya Dikolelayi iliyoko Kananga, jimbo la Kasai-Occidental, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)

 

Akiunga mkono hilo mkimbizi mwingine wa ndani Rehema Safi anasema “Wakati mvua ikinyesha adha inaongezeka kwani hakuna mifereji mizuri ya kupitisha maji machafu hivyo tunahofia sana hali ya afya hasa magonjwa ya mlipuko nay a kuambukiza ikiwemo kipindupindu.” 

Wakimbizi hawa wanapatiwa misaada na huduma nyingi na serikali lakini pia mashirika ya kimataifa kama lile la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, na la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambalo limesema linatambua changamoto za wakimbizi hawa na linafanya kila liwezalo kuwasaidia.

Antonia Vadala ni afisa mawasiliano wa UNHCR Goma “Tunafanya mambo mengi kusaidia wakimbizi wa ndani na wale wanaotoka nje ya nchi tukishirikiana na serekali ya DRC. Katika mkoa wa kivu ya kusini tunazo ofisi tatu moja Baraka, uvira na Bukavu. Tuna shughulikia wakimbizi kutuka nchi ya Burundi katika makambi na wakimbizi wa ndani pia. Ni kweli kuna changamoto nyingi na hapa kambini zipo lakini tunajitahidi kufanya kila tuwezalo kuwaudumia wakimbizi wandani kamavile wengine wakimbizi.” 

Mbali ya changamoto ya vyoo wakimbizi hawa wa ndani pia wameeleza kkukabiliwa na ufungufu wa huduma nyingine za msimu iliwemo huduma za afya, chakula na malazi. 

Wengi wa wakimbizi hawa wa ndani Uvira wanatokana na vita vya wenyewe kwa wenye, lakini pia athari za mabadiliko ya tabianchi yaliyosababisha kupanda kwa kina cha maji kwenye ziwa Tanganika na hivyo kuleta mafuriko makubwa yaliyosambaratisha nyumba za maelfu ya watu ambao sasa wamelazimika kuwa wakimbizi wa ndani.  

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter