Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Kaunti ya Samburu nchini Kenya, mfugaji akizubiri mbuzi wake wachanjwe dhidi ya PPR.

Sababu saba ni kwa nini ufugaji unachangia mustakbali bora:FAO

©FAO/Luis Tato
Kaunti ya Samburu nchini Kenya, mfugaji akizubiri mbuzi wake wachanjwe dhidi ya PPR.

Sababu saba ni kwa nini ufugaji unachangia mustakbali bora:FAO

Tabianchi na mazingira

Ufugaji wa kuhamahama, ni njia ya kitamaduni ya ufugaji, ambayo inawaajiri zaidi ya watu milioni 200 kwenye nchi 100 kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO.  

Wafugaji wa kuhamama huchunga na kulisha mifugo yao katika maeneo tofauti.

Wakiwa na aina tofauti ya mifugo ya kienyeji  wanaweza kubadilika kulingana na mazingira tofauti, ufugaji ni muhimu katika kupunguza umaskini na kuhakikisha uhakika wa chakula katika maeneo hayo. 


Hizi ni sababu saba za kwanini ufugaji wa kuhamahama ni muhumu kwa mustakbali wa chakula 


1. Unaongeza uwepo wa chakula 

Katika ulimwengu ambapo upatikanaji wa mali asili na mabadiliko ya tabianchi vinazidi kutofautiana, kutegemea mahitaji ya maziwa na nyama ni hatari katika uzalishaji. 

Ufugaji wa kuhamama, huchangia protini nafuu na ya hali ya juu na lishe ili kutimiza mahitaji ya jamii na unaweza kusaidia nchi kutotegemea uagizaji wa chakula.   
Na kwa sababu wafugaji husafiri na mifugo yao kutafuta lishe na maji, mazao huwa kidogo kuliko gharama wanazotumia. 

Mfugaji wa kuhamahama akiwa na kundi lake la mbuzi kwenye kambi iliyoko kusini mwa Kandahar, Afghanistan.
© FAO/Alessio Romenzi
Mfugaji wa kuhamahama akiwa na kundi lake la mbuzi kwenye kambi iliyoko kusini mwa Kandahar, Afghanistan.

2. Unazuia mabadiliko ya tabianchi 

Kwa mujibu wa FAO, utafiti unaonesha kuwa mandhari ya ufugaji yana uwezo wa kupunguza viwango vya hewa ukaa kwa kuwa wakati mifugo wanakula malisho inachangia mimea kuota tena. Pia wakati mifugo wanahama wanaweza kuacha mbolea ambayo inachangia kukua kwa mimea

Wafugaji pia husaidia kusimamia vyema mali asili kusaidia kulinda viumbe hao katika mazingira yote, kuanzia maeneo ya jangwa hadi sehemu zenye maji na misitu.   
Kwa kujumuisha ujuzi wa wafugaji wanaweza kusaidia kulinda mifumo na ikolojia.  

3. Unasaidia kama mfumo wa tahadhari ya mapema kuhusu magonjwa 

Janga la COVID-19 limetufunza jinsi ya kukabiliana na changamoto za kiafya likihitaji kutilia maanani afya ya wanyama, mazingira na wanadamu. 
Ni njia mojawapo inayosaidia nchi kufuatilia na kudhibiti magonjwa yanayoambukiza kati ya wanyama na wanadamu.  

Wafugaji wa kuhamahama wana wajibu mkubwa kwa hili kwa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu magonjwa mapya ya kuambukiza, ambayo ni tisho kwa wanyapori. 

Kuhakakisha uwepo wa huduma za afya ya mifugo na hatua za kuzuia ikiwemo chanjo nafuu na ya hali ya juu, ambayo itasadia kuongeza uzalishaji na kupunguza hatari ya maaambukizi ya magonjwa. 
Kati ya mwaka 2016 na 2018 FAO ilichanja mifugo milioni 30 katika maeneo ya wafugaji nchini Ethiopia. 

4. Unachangia kuongeza nafasi za ajira. 

Ufugaji huwa ni tegemeo la maisha kwa mamilioni ya watu kwenye asilimia 75 ya nchi za dunia hii, lakini umepuuzwa kwa miaka mingi kutokana na sera na uwekezaji. 

Kuwasaidia wafugaji kupata elimu, habari, masoko, msaada madaktari, afya na misaada ya kifedha vinaweza kuchangia matokeo makubwa wa kiuchumi na kijamii. 

5. Unapunguza ushindani kati ya kula na chakula 

Mahitaji ya chakula yatokanayo na mifugo inayokuzwa kwa kutumia chakula asilia ambacho ni nyasi yanazidi kuongezeka na kupanua soka la bidhaa hizi na pia kuchangia fursa mpya kwa mauzo ya nje na faida. 

Inakadiriwa kuwa hadi watu milioni 811 duniani walikabiliwa na njaa mwaka 2020.  

Mifumo ya asili ya ufugaji wa kutegemea malisho inaweza kusaidia kuongeza uhakika wa chakula kwa kupunguza ushindani katika nafaka kati ya chakula cha mifugo na chakula cha binadamu. 

Mfugaji wakipeleka mifugo kwenye malisho
FAO/Giulio Napolitano
Mfugaji wakipeleka mifugo kwenye malisho

6. Unalinda utofauti wa wanyama 

Familia za wanyama wa kuhamahama zimekuwa zikifugwa kwa maelfu ya miaka na kuchangia katika baadhi ya viwango vya juu vya utofauti wa vinasaba kwa aina mbalimbali za wanyama. 

Utofauti huu wa mifugo wa kienyeji hutokana na kutegemeana kwa karibu kati ya mazingira, wafugaji na mifugo. 

Kutona na kuchagua kwa kuzingatia aina yamifugo na ufahamu wao wafugaji  wanaendelea kuboresha mifugo wao na kuwawezesha kukabiliana na mabadiliko ya mazingira , magonjwa na kubadilika kwa masoko. 

7. Unasaidia ukuaji wa misitu 

Ufugaji na misitu hutegemeana. Katika Sehemu zingine misitu iliyo karibu na maeneo yenye maji, huwa ni malisho muhimu kwa mifugo wakati wa kiangazi. Kwa kubadilishana ufugaji husaidia kudumisha na kufufua upya maeneo haya. 
Kwa mfano wanyama wanaocheua husaia kumea mbegu za miti ya mshita katika misitu ya nchi kavu. 
Wafugaji barani  Ulaya huchangia kukua kwa miti mikubwa pia.  
Na wafugaji huwa na nafasi kubwa ya kuzuia moto wa nyika kwa kuwa wanyama wao hupunguza majani msituni na hivyo kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. 


TAGS: FAO, wafugaji, kilimo, mabadiliko ya tabianchi