Tuna wasiwasi mkubwa na ukiukwaji wa haki unaoendelea DRC: OHCHR

Mlinda amani wa kike aendesha semina ya afya ya akili huko Kivu Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
MONUSCO
Mlinda amani wa kike aendesha semina ya afya ya akili huko Kivu Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Tuna wasiwasi mkubwa na ukiukwaji wa haki unaoendelea DRC: OHCHR

Amani na Usalama

Ofisi ya kamishna mkuu wa Haki za Binadamu  wa Umoja wa Mataifa OHCHR imesema hali katika maeneo ya Masisi na Lubero kwenye jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC inatia wasiwasi mkubwa. 

Kwa mujibu wa taaifa ya ofisi hiyo iliyotolewa leo mjini Geneva Uswis migogoro ya ardhi miongoni mwa jamii imesababisha vurugu baina ya jamii, jambo ambalo limechochea kuibuka kwa makundi yenye silaha.  
 
Taarifa imeongeza kuwa “vikundi hivi vimeweza kuchukua karibu udhibiti kamili wa maeneo ya Masisi na Lubero, ambapo uwezo wa vikosi vya serikali ni mdogo na vikosi vichache vya usalama vimetumwa. Tangu mwezi januari hadi Oktoba  mwaka huu jumla ya matukio 966 ya uvunjifu wa haki za binadamu yamerekodiwa” 

Ongezeko la vitendo vya ukiukwaji wa haki

Ofisi hiyo imesema vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyoarifiwa Masisi na Lubero vimeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu mwaka 2015 na hivi sasa zaidi ya nusu ya vitendo vyote vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyorekodiwa katika jimbo la Kivu ya Kaskazini vinatokea katika maeneo hayo mawili. 

Taarifa zilizorekodiwa na ofisi ya pamoja ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo UNJHRO na kuchapishwa leo inasema “Makundi ya watu wenye silaha yametekeleza angalau vitendo 2,359 vya ukatili na ukiukwaji wa haki za binadamu na kukiuka sheria za kimataifa zakibinadamu kwenye moji ya Masisi na Lubero ndani ya miezi 10 ya mwanzo yam waka huu, ikiwa ni ongerzeko la visa 801 ukilinganisha na vitendo vilivyokurekodiwa mwaka 2020 na visa 756 kwa mwaka 2019.” 

Taarifa imeongeza kuwa miongoni mwa matukio 2.359 yaliyoorodheshwa mwaka 2021 ni pamoja na vitendo 484 ya watu kuuawa, vitendo 1455 vya watu kujeruhiwa baada ya kushambuliwa na waathirika 354 ukatili wa kingono. 

Ukiukwaji mwingine kwa mwaka huu wa 2021 ni pamoja kuuawa kwa raia 111, watu 542 kujeruhiwa na visa 58 vya ukatili wa kingono. 

Kugfuatia hali hii sasa ofisi ya haki za binadamu imetoa wito kwa serikali kuanzisha haraka uchunguzi uhuru na wenye ufanissi kuchunguza ukiukwaji huo mkubwa wa haki za binadamu na ukatili kwa lengo la kuwawajibisha wahusika.