Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda yashirikiana na sekta binafsi kufikisha chanjo dhidi ya COVID-19 kwa wananchi 

Mmoja wa Raia wa Uganda akipokea chanjo yake ya kwanza ya Covid-19 huko Hoima, Uganda.
John Kibego
Mmoja wa Raia wa Uganda akipokea chanjo yake ya kwanza ya Covid-19 huko Hoima, Uganda.

Uganda yashirikiana na sekta binafsi kufikisha chanjo dhidi ya COVID-19 kwa wananchi 

Afya

Ili kuudhibiti ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, serikali ya Uganda imeamua kushirikiana zaidi na wadau mbalimbali yakiwemo makampuni ya mawasiliano na yale ya vinywaji katika juhudi za kuimarisha chanjo.  Je, kampeni hiyo inatekelezwaje? Na mtazamo wa Waganda kuhusu chanjo hiyo ukoje sasa? Hii hapa taarifa iliyoandaliwa na mwandishi wetu wa Uganda John Kibego.

Huyu ni mmoja wa wazee waliojitokeza kwa ajili ya kupata chanjo kwenye tukio la kwanza kabisa la chanjo ya Covid -19 kwa umma jijini Hoima kwenye mghahawa wa De-place.
(Sauti)
Christopher Ssebalujja, anaeleza kwa nini yeye ameamua kupokea chanjo hii wakati watu wengine bado wanajikokota.
(Sauti)
Zoezi hili linalowalenga watu 10,000 katika wilaya 21 kote nchini, linatekelezwa na kampuni ya bia ya Nile Breweries Limited katika ushirikiano na wizara ya afya.
Mkurugenzi wa De-place, mwenyeji wa zoezi hili ni Julius Kawiso anasema, 
CLIP:
Julian Aweju ni kiongozi wa wauguzi wanaotoa chanjo hapa
CLIP:
Aweku anawatolea wito wananchi akisema
CLIP:
Meneja wa endelezaji katika kampuni ya Nile Breweries Limited, Clare Asiimwe, amefurahishwa na kubadilika kwa mtazamo wa jamii kuhusu chanjo dhidi ya COVID-19.
CLIP:
Kwa sasa watu 749, 129 kote nchini tayari wamepata chanjo kamili. Wengine 2,570,525 wamepata dozi yao ya kwanza kulingana na waziri wa afya Jane Ruth Aceng. Watu milioni 12 wanatarajiwa kuchanjwa ifikapo mwishoni mwa Desemba mwaka huu. Serikali inataka watu milioni 22 wawe wamechanjwa kabla ya kufunguliwa tena kwa sekta zote zilizofungwaili kudhibiti mlipuko wa COVID-19.