Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fahamu kuhusu wiki ya polisi UN 8 hadi 12 Novemba 2021

Mmoja wa mapolisi wa awali kutoka Ghana kwenda kuhudumu chini ya Polisi wa Umoja wa Mataifa na hapa ni mji wa Leopoldiville huko Congo mwaka 1960. Sasa Leopoldville ni Kinshasa ya DRC.
UNPOL
Mmoja wa mapolisi wa awali kutoka Ghana kwenda kuhudumu chini ya Polisi wa Umoja wa Mataifa na hapa ni mji wa Leopoldiville huko Congo mwaka 1960. Sasa Leopoldville ni Kinshasa ya DRC.

Fahamu kuhusu wiki ya polisi UN 8 hadi 12 Novemba 2021

Amani na Usalama

Leo wiki ya polisi wa Umoja wa Mataifa imeanza na wakuu wa vyombo vya polisi  vya Umoja wa Mataifa na operesheni zake wanakutana mtandaoni ili hadi 12 Novemba 2021. 

Washiriki hao wanatoka katika vitengo vya polisi katika operesheni za ulinzi wa amani, kutoka jumbe maalum za kisiasa na ofisi za kikanda, pamoja na viongozi wakuu kutoka idara ya Umoja wa Mataifa ya operesheni za amani (DPO) na idara na ofisi zingine za mfumo wa Umoja wa Mataifa, na wanakutana kujadili maendeleo muhimu, vipaumbele na changamoto kwa polisi wa Umoja wa Mataifa. 

Mwaka huu, ndani ya muktadha wa vipaumbele vya hatua kwa ajili ya ulinzi wa amani (A4P) na A4P+, vikao vitazingatia kuimarisha ushirikiano na kustawisha utangamano na mshikamano zaidi katika ulinzi wa polisi wa Umoja wa Mataifa; kuimarisha utendaji wa polisi wa Umoja wa Mataifa UNPOL katika ulinzi wa raia na kuzuia vitisho vya kimataifa; kuboresha utendaji, uwezo, na mawazo, kuimarisha mazoea mazuri na mafunzo ili kupunguza athari za COVID-19, na kuhakikisha ulinzi wa kijinsia na mazingira ndani ya operesheni za Umoja wa Mataifa.  

Kwa kuongezea, washiriki watajadili jinsi gani kikosi kazi cha mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kilichoanzishwa hivi karibuni inachohusu uendeshaji wa polisi  ambacho kinachosimamiwa na DPO na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Madawa na Uhalifu UNODC na pia mabadiliko ya kidijitali ya shirika hilo yanavyoweza kuendeleza majadiliano na juhudi hizi. 

Askari wa UNPOL kutoka Slovakia akizungumza na mkulima anayefanya kazi karibu na eneo la mto huko Cyprus
UNFICYP/Maria Homolyova
Askari wa UNPOL kutoka Slovakia akizungumza na mkulima anayefanya kazi karibu na eneo la mto huko Cyprus

Kinachojiri kila mwaka 

Kila mwaka, wakuu wa vitengo vya polisi (HOPCs) kutoka oparesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, mipango maalum ya kisiasa na ofisi za kanda na viongozi wakuu wa Umoja wa Mataifa hukutana ili kujadili vipaumbele vya kimkakati vya sera, changamoto zinazojitokeza, na njia ya kusonga mbele, kwa kawaida ana kwa ana mjini New York lakini katika miaka ya hivi karibuni kutokana na COVID-19 mkutano huo wa juma zima unafanyika kwa njia ya mtandao. 

Wiki ya Polisi ya Umoja wa Mataifa, mwaka huu ni toleo la 16, lna inafanyika kuanzia leo tarehe 8 hadi 12 Novemba 2021, itajumuisha muhtasari wa HOPC kwa Baraza la Usalama na kamati maalum ya operesheni za ulinzi wa amani (C-34) na pia miongoni mwa mambo mengine ni utoaji wa tuzo yam waka 2021 ya Afisa bora wa polisi mwanamke wa Umoja wa Mataifa. 

 

Doria ya pamoja kati ya Misri FPU, polisi wa Umoja wa Mataifa na polisi wa DRC katika mji wa Bukavu
MONUSCO
Doria ya pamoja kati ya Misri FPU, polisi wa Umoja wa Mataifa na polisi wa DRC katika mji wa Bukavu

Historia na kazi ya polisi wa UN 

Kikosi cha Kwanza

Tangu kutumwa kwa kikosi cha polisi wa Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza mwaka 1960 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, hadi sasa makumi ya maelfu ya maafisa wa polisi wanawake na wanaume kutoka nchi 129 wameleta pamoja utaalamu wao wa polisi kulinda idadi kubwa ya watu, kuimarisha utawala wa sheria na kujenga misingi ya huduma za polisi zenye ufanisi, tija, uwakilishi, usikivu na uwajibikaji zinazohudumia na kulinda wakazi wa mataifa mwenyeji. 

Jukumu la kipekee

Polisi wa Umoja wa Mataifa wana jukumu la kipekee miongoni mwa polisi duniani, wakiwa na nguvu kubwa hivi sasa  iliyoidhinishwa kuwa na wanawake na wanaume zaidi ya 9,900 kutoka zaidi ya nchi 90 wanaohudumu kwenye mstari wa mbele katika oparesheni 14 za amani za Umoja wa Mataifa kote duniani kama sehemu ya operesheni kubwa za ulinzi wa amani zinazojumuisha pande nyingi, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Mali na Sudan Kusini, lakini pia kwenye operesheni ndogo za kisiasa ambazo ni maalum nchini Colombia, Haiti na Yemen. 

Kusaidia kudumisha sheria na utulivu

Polisi wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakisaidia mamlaka za nchi mwenyeji kudumisha sheria na utulivu, kulinda raia, na kushirikiana na wakazi wa eneo hilo kupitia polisi wanaozingatia jamii, Pia polisi wa Umoja wa Mataifa wamesaidia kuandaa njia kwa baadhi yaoperesheni  kubwa zaidi za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Côte d' Ivoire, Liberia, na Sudan (Darfur), kubadilisha na kukabidhi majukumu ya msingi ya usalama kwa wenzao wa nchi mwenyeji. 

Uratibu na  mashirika

Kamati ya utendaji ya Katibu Mkuu hivi karibuni iliitaka Jeshi la Polisi la Umoja wa Mataifa kuimarisha uratibu kati ya mashirika kwa kuanzisha kikosi kazi kinachoongozwa na idara ya operesheni za amani za Umoja wa Mataifa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na dawa na uhalifu UNODC.  

Hii inaashiria enzi mpya kwa polisi wa Umoja wa Mataifa na inaimarisha zaidi umuhimu wa kazi yake katika malengo yote ya shirika ya kisiasa, amani, usalama, haki za binadamu na maendeleo kama kuwezesha ajenda ya maendeleo endelevu na mpango wa kulinda amani (A4P) na A4P+). 

Walinda amani wakifanya doria katika mkoa wa Menaka nchini Mali eneo ambalo kuna makundi ya magaidi
MINUSMA/Gema Cortes
Walinda amani wakifanya doria katika mkoa wa Menaka nchini Mali eneo ambalo kuna makundi ya magaidi

Huduma za kipolisi na utaalamu

Kwa kuteuliwa na Katibu Mkuu kutoa huduma za kipolisi na utaalamu katika mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa, polisi wa Umoja wa Mataifa wanazidi kuunga mkono na kusaidia timu za Umoja wa Mataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa, mfuko na programu.  

Hivi karibuni, usaidizi huu umejumuisha kutoa ushauri juu ya usalama wakati wa uchaguzi nchini Malawi na Uganda, mazoea ya kukabiliana na masuala ya kijinsia nchini Liberia, na ulinzi wa haki za binadamu wakati wajanga la COVID-19 nchini Angola, Msumbiji, Tanzania na Zambia.  

Mada kuu za majadiliano ya mkutano wa mwaka huu ni pamoja na

(i) Mahitaji ya usaidizi endelevu wa Umoja wa Mataifa unaozingatia haki za binadamu na jinsia na mazingira; (ii) mbinu na mafunzo mazuri ili kupunguza athari za COVID-19 katika utekelezaji wa majukumu, na

(iii) Kukuza uwiano zaidi katika ulinzi wa polisi wa Umoja wa Mataifa.

Mipango ya Polisi wa Umoja wa Mataifa

Kuzingatia mipango muhimu ya Polisi wa Umoja wa Mataifa kama vile mfumo wa mwongozo wa kimkakati wa uendeshaji wa polisi wa kimataifa na mfumo wa kina wa utendaji na mafunzo ulioimarishwa, na vikao vinajumuisha HOPC na uongozi wa juu wa DPO pamoja na maafisa kutoka kote Umoja wa Mataifa  vitahusu ahadi za A4P na vipaumbele vya A4P+ , vikijumuisha utendaji kazi na uwajibikaji, uwezo na mawazo, tabia na nidhamu, ushirikiano na ushirikiano wa kimkakati na uendeshaji, ulinzi wa raia, mawasiliano ya kimkakati. ubunifu na utendaji wa kidijitali wa polisi, na wanawake, amani na usalama. 

Faida za Wiki ya Polisi wa UN

Wiki ya Polisi itasaidia kuandaa mijadala kuhusu vipaumbele vya Umoja wa Mataifa na ulinzi wa polisi duniani, mahitaji, changamoto, na hatua kuelekea kwa mkutano wa mawaziri wa kutoka nchi zinazolinda amani utakaofanyika mwezi Desemba mjini Seoul Korea na mkutano wa wakuu wa polisi wa Umoja wa Mataifa (UNCOPS) iliofanyika mjini New York mwezi Juni 2021.

Katika matukio haya nchi wanachama zinapata fursa ya kujitolea tena kuchangia kwa polisi wa Umoja wa Mataifa kwa kuahidi wafanyakazi wa polisi wenye ujuzi, mafunzo na vifaa, na rasilimali nyingine.