Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto sita wamekufa Afghanistan baada ya mabaki ya silaha za vita kulipuka:UNICEF

Mizozo na kutokuwepo kwa usalama nchini Afghanistan kumewaacha watoto katika hatari kubwa kuwahi kutokea
© UNICEF/Shehzad Noorani
Mizozo na kutokuwepo kwa usalama nchini Afghanistan kumewaacha watoto katika hatari kubwa kuwahi kutokea

Watoto sita wamekufa Afghanistan baada ya mabaki ya silaha za vita kulipuka:UNICEF

Amani na Usalama

Watu tisa wa familia moja wakiwemo wasichana wanne na wavulana wawili wamepoteza maisha jana Jumatano asubuhi wakati mabaki ya silaha za vita yalipolipuka ndani ya nyumba kwenye mji wa Kunduz nchini Afghanistan, na watoto wengine watatu walijeruhiwa katika tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Alice Akunga, Kaimu mwakilishi wa UNICEF nchini Afghanistan “imeripotiwa kwamba mtoto mmoja bila kujua alibeba kifaa cha mlipuko hadi nyumbani ambacho alikiokota shambani karibu na nyumba yako.

Watoto wako katika hatari kubwa kutokana na mabaki ya silaha na vifaa vya vita ambavyo havijalipuka, na watoto mara nyingi wanapata vishawishi vya kucheza na vifaa hivyo au kuvikusanya kuweza kujipatia kipato kidogo bila kujua hatari yake na hivyo kuwaweka wao na familia zao katika hatari kubwa.”

Alice ameongeza kuwa tukio hilo linadhihirisha umuhimu wa kuchukua hatua haraka kusafisha na kuondoa vifaa vyote vya mlipuko na mabaki ya silaha za vita na kuelimisha jamii kuhusu hatari zake.

Kaimu huyo mwakilishi amesema “Kuongezeka kwa idadi ya vifo vya Watoto ni kumbusho kwamba watoto wanaendelea kulipa gharama kubwa ya vita ambavyo hawajavisababisha.”

Ameongeza kuwa hadi kufikia sasa watoto 460 wameuawa kutokana na vita vinavyoendelea katika miezi 6 ya mwanzo yam waka huu. Vifo hivi nit u ambavyo Umoja wa Mataifa umeweza kuvithibitisha.” Kwa mantiki hiyo amesema UNICEF inatoa wito kwa pande zoto kwenye mzozo wa Afghanistan kufanya juhudi za kuwalinda watoto na raia.

Amesisitiza kwamba “Usalama wa watoto na ulinzi wao ni lazima uwe kipaumbele katika nyanja zote. Ain azote za ukatili dhidi ya Watoto lazima ukomeshwe mara moja.”