Skip to main content

WHO yatoa wito wa watoa hudumu ya afya kulindwa dhidi ya COVID-19

Muhudumu wa afya akimuhudumia mgonjwa katika ukumbi uliobadilishwa matumizi na kuwa wodi ya muda ya wagonjwa wa COVID-19 huko New Delhi, India
© UNICEF/Amarjeet Singh
Muhudumu wa afya akimuhudumia mgonjwa katika ukumbi uliobadilishwa matumizi na kuwa wodi ya muda ya wagonjwa wa COVID-19 huko New Delhi, India

WHO yatoa wito wa watoa hudumu ya afya kulindwa dhidi ya COVID-19

Afya

wafanyikazi wa huduma za afya kwa jumla wamelipa gharama kubwa wakati wa janga la COVID-19. Na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani (WHO) na washirika wake leo mjini Geneva Uswis wamezindua ombi la dharura la kuchukua hatua madhubuti ili kulinda vyema afya na wahudumu wa afya kote ulimwenguni dhidi ya virusi vya Corona na changamoto zingine za kiafya.

Katika taarifa ya pamoja, shirika la WHO na washirika wake wameelezea wasiwasi wao mkubwa "juu ya idadi kubwa ya vifo vya wahudumu wa afya na wauguzi kutokana na COVID-19, lakini pia idadi inayoongezeka ya wafanyikazi wanakabiliwa na msongo wa mawazo, mfadhaiko, wasiwasi na uchovu ”.

Mbali na shirika la afya duniani wengine waliotia Saini wito huo ni pamoja na shirika la kazi duniani (ILO), shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo (OECD) na mashirika mengine matano ya kitaalam, na  ushirikiano wa  masuala ya afya duniani au World Medical Chama.

Wahudumu wa afya wasiopungua 115,000 wamekufa na COVID-19

Kwa mujibu wa WHO, angalau wahudumu wa afya 115,000 wamepoteza maisha kutokana na janga la COVID-19.  

"WHO inakadiria kuwa kati ya wahudumu wa afya na wahudumu wa kijamii kati ya 80,000 na 180,000 wangekufa kutokana na virusi vipya vya corona kati ya Januari 2020 na Mei 2021, ambayo inafanya hali ya wastani ya vifo kuwa 115,500," limesema shirika hilo la Umoja wa Mataifa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Makadirio haya yanatokana na vifo milioni 3.45 vinavyohusiana na COVID-19 vilivyoripotiwa kwa WHO mwezi Mei 2021.  

Idadi hiyo inakadiriwa kuwa kuwa chini sana kuliko idadi halisi ya vifo, asilimia 60% au zaidi ya kile kinachoripotiwa katika WHO.

Kwa vyovyote vile, "vifo hivi ni upotevu mkubwa wa watu na pia ni pengo lisiloweza kuzibika katika vita hivi dhidi ya janga la  kimataifa".

Wakati huo huo, "inatia moyo kwamba kiwango cha maambukizi na vifo vilivyoripotiwa miongoni mwa wafanyikazi wa afya na huduma vimepungua kwa muda," limesema shirika la WHO.  

Lakini ni njia ya kukumbusha kila mtu kuwa bado ni mapema kubweteka kuhusu janga hili. Na "juhudi zaidi zinahitajika kupunguza hatari ya maambukizi mahali pa kazi."

Chanjo za COVID-19 zikiandaliwa katika kituo cha chanjo nchini Ufilipino
ADB/Eric Sales
Chanjo za COVID-19 zikiandaliwa katika kituo cha chanjo nchini Ufilipino

Wajibu wa kimaadili kulinda wahudumu wa afya

Katika taarifa yao ya pamoja, WHO na washirika wake wametaka hatua za haraka na madhubuti zichukuliwe kulinda wafanyakazi wa afya na wato huduma.  

Taarifa yao imetoa wito kwa serikali na wadau wote kuimarisha ufuatiliaji na ripoti za maambukizo ya virusi vya corona, wagonjwa na vifo miongoni mwa  wahudumu wa afya na walezi.

Taarifa hiyo pia imewataka viongozi wa kisiasa na watunga sera kufanya maamuzi ya kisheria, sera na uwekezaji ambayo yanahakikisha ulinzi wa wafanyikazi wa afya na watoa huduma.  

Zaidi ya yote, ni juu ya kuharakisha chanjo kwa wafanyikazi wote wa afya na huduma katika nchi zote duniani.

"Utambuzi na maadhimisho hayatoshi," limesema shirika la WHO na washirika wake wakibaini kwamba Ni "wajibu wa kimaadili kulinda na kuwekeza katika wafanyikazi wa afya na wato huduma".

Janga hilo limeua zaidi ya milioni 4.9 tangu mwisho wa Desemba 2019. Kulingana na ripoti iliyotolewa leo na WHO, idadi kubwa ya wagonjwa waliothibitishwa walioripotiwa duniani kote sasa ni zaidi ya wagonjwa milioni 241.4.

Chini ya muhudumu 1 kati ya 10 Afrika ndiye amepata chanjo na Pasifiki Magharibi

Chanjo zaidi ya bilioni 6.6 zimetolewa duniani. Lakini zaidi ya asilimia 75 ya dozi hizo zimetolewa kwa nchi za kipato cha juu.

Nchi zinazoendelea zimepokea chini ya nusu asilimia ya chanjo ziziliztolewa duniani.

Kwa mujibu wa WHO, ni asilimia 5% tu ya idadi ya Waafrika ndio ambao wamepewa chanjo kamili.  
Nchi tajiri sasa zimesimamia nyongeza ya nusu kama idadi ya chanjo inayotolewa katika nchi zenye kipato cha chini.

Kwa kuongezea, data zinazopatikana kutoka nchi 119 zinadokeza kuwa mwezi Septemba 2021, wafanyikazi wawili kati ya watano wa afya na huduma walipewa chanjo kamili kwa wastani, na kuna tofauti kubwa kati ya kanda na maendeleo ya kiuchumi.

Chini ya mtu mmoja kati ya kumi wamepewa chanjo kamili barani Afrika na maeneo ya Pasifiki ya Magharibi, wakati nchi 22, zenye kipato cha juu, zimeripoti kuwa zaidi ya asilimia 80% ya wafanyikazi wao wa afya na watoa huduma.