Njaa inaongezeka kote duniani wakati wa kuchukua hatua ni sasa:Guterres 

15 Oktoba 2021

Kuelekea siku ya chakula duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 16, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema siku hii sio tu kumbusho la umuhimu wa chakula kwa kila mtu duniani, bali pia ni woto wa kuchua hatua ili kufikia uhakika wa chakula kote duniani. 

Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii amesema “Leo hii karibu asilimia 40 sawa na watu bilioni 3 hawawezi kumudu lishe bora. Njaa inaongezeka, sanjari na utapiamlo na utipwatipwa.” 

Ameongeza kuwa athari za kiuchumi za janga la COVID-19 zimefanya hali mbaya kuwa mbaya zaidi kwani limewaacha watu wengine zaidi milioni 140 wakikosa fursa ya chakula wanachokihitaji. 

Guterres ameongeza kuwa wakati huohuo “Jinsi watu wanavyozalisha, kutumia na kutupa chakula kunaathiri vibaya dunia yetu. Kunaongeza shinikizo kwa maliasili yetu, hali ya hew ana mazingira na hivyo kutugharimu matrilioni yad ola kila mwaka.” 

Amesisitiza kwamba kama ilivyoanisha kaulimbiu ya siku ya mwaka huu, “Uwezo wa kubadili mwelekeo uko mikononi mwetu. Matendo yetu ndio mustakbali wetu.” 

Katibu Mkuu amesema mwezi uliopita vipongozi wa dunia walikusanyika kwa ajili ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mifumo ya chakula , nan chi zilitoa ahadi ya kubadili mifumo hiyo ili kufanya lishe bora kupatikana kwa urahisi na kwa gharama nafuu na kuifanya mifumo ya chakula kuwa yenye ufanisi, yenye mnepo na endelevu katika kila hatua kuanzia uzalishaji, usindikaji hadi uuzaji, usafirishaji na ufikishaji kwa mlaji. 

“Soto tunaweza kubadili jinsi tunavyotumia chakula na kuwa na machaguo bora zaidi kiafya kwa ajili yet una sayari yetu. Katika mifumo yetu ya chakula kuna matumaini.”  

Kwa manitiki hiyo katika siku ya chakula duniani ametoa wito kwa kila mtu kujiunga na jumuiya ya kimataifa katika kuchukua hatua za mabadiliko  na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu kupitia mifumo ya chakula ambayo itazalisha lishe bora, mazingira bora na maisha bora kwa kila mtu. 

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter