Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 yaongeza vifo vya TB kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya muongo mmoja:WHO

India inaendelea kubeba mzigo mkubwa zaidi wa wagonjwa wa kifua kikuu Duniani
ILO Photo/Vijay Kutty
India inaendelea kubeba mzigo mkubwa zaidi wa wagonjwa wa kifua kikuu Duniani

COVID-19 yaongeza vifo vya TB kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya muongo mmoja:WHO

Afya

Janga la Corona, COVID-19 limebadili mwelekeo wa mafanikio ya kimataifa ya miaka mingi katika kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu au TB, na kwa mara ya kwanza kwa muda wa zaidi ya muongo mmoja vifo vitokanavyo na kifua kikuu vimeongezeka imesema ripoti ya kimataifa ya TB kwa mwaka 2021 liyotolewa leo na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mwaka wa 2020, watu wengi walifariki dunia kutokana na TB, na watu wachache sana waligunduliwa na kutibiwa au kupatiwa kinga ya TB ikilinganishwa na mwaka 2019, na pia matumizi ya jumla kwa huduma muhimu za TB yalipungua. 

Ripoti imesema changamoto ya kwanza ni usumbufu katika upatikanaji wa huduma za kifua kikuu na upunguzaji wa rasilimali.  

Katika nchi nyingi, rasilimali watu, fedha na rasilimali nyingine zimehamishwa kutoka kukabiliana na TB kwenda kwenye vita dhidi ya COVID-19, na hivyo kupunguza upatikanaji wa huduma muhimu. 

Pili ni kwamba imekuwa changamoto kubwa kwa watu kusaka huduma wakati wa vizuivya kusalia majumbani. 

Mkurugenzi mkuu Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema "Ripoti hii inathibitisha hofu yetu kwamba kuvurugika kwa huduma muhimu za afya kwa sababu ya janga la COVID-19 kunaweza kuanzakurudisha nyuma maendeleo yaliyopigwa kwa miaka mingi katika vita dhidi ya kifua kikuu. Hii ni habari ya kutisha ambayo inapaswa kutumika kama kengele ya kuuamsha ulimwengu kwa hitaji la haraka la uwekezaji na ubunifu ili kuziba mapungufu katika utambuzi, matibabu na huduma kwa mamilioni ya watu walioathiriwa na ugonjwa huu wa zamani ambao unaweza kuzuilika na kutibika." 

Mgonjwa anayepokea tiba dhidi ya kifua kikuu Lima, Peru.
PAHO/Joshua Cogan
Mgonjwa anayepokea tiba dhidi ya kifua kikuu Lima, Peru.

Huduma za TB ni miongoni mwa zilizoathirika 

 Ripoti imeongeza kuwa huduma za kifua Kikuu ni miongoni mwa huduma nyingi zilizathirika kwa sababu ya COVID-19, lakini athari kwa TB zimekuwa mbaya zaidi. 

Mathalani ripoti inasema mwaka 2020 takriban watu milioni 1.5 walikufa kwa TB wakiwemo 214,000 miongoni mwao waliokuwa na VVU. 

Pia imetanabaisha kwamba ongezeko la vifo vya TB imebainika katika nchi 30ambazo zinabeba mzigo mkubwa wa TB ambako inatabiriwa kuwa idadi ya watu wanaopata TB na kufa kutokana na ugonjwa huo inaweza kuwa ya juu zaidi kwa mwaka 2021 na 2022. 

Changamoto za kufikia huduma wakati wa COVID-19 ripoti inasema zinamaanisha watu wengi hawakupimwa na walioripotiwa kupimwa kitaifa idadi ilipungua kutoka milioni 7.1 mwaka 2019 hadi milioni 5.8 mwaka 2020. 

WHO inakadiria kwamba watu milioni 4.1wanaugua kifua kikuu hivi sasa lakini hawajapimwa au kuripiti kwa mamlaka kuwa na ugonjwa huo, na idadi hii imepanda kutoka watu milioni 2.9 kmwaka 2019. 

Hali halisi 

Nchi ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguzwa kwa taarifa za TB kati ya mwaka 2019 na 2020 ni pamoja na India (41%), Indonesia (14%), Ufilipino (12%) na China (8%).  

Hizi na nchi zingine 12 zilichangia asi;limia 93% ya jumla ya kushuka kwa taaarifa za ugonjwa huo kimataifa. 

Kulikuwa pia na upunguaji wa kiasi kikubwa wa utoaji wa matibabu ya kuzuia TB. Watu milioni 2.8 walipata huduma mwaka 2020, ikiwa ni punguzo la asilimia 21% tangu mwaka 2019.  

Mtaalam wa maabara nchini Bangladesh akijaribu kuchanganya dawa na kifua kikuu sugu (MDRT)
The Global Fund/Thierry Falise
Mtaalam wa maabara nchini Bangladesh akijaribu kuchanganya dawa na kifua kikuu sugu (MDRT)

Kwa kuongezea, idadi ya watu waliotibiwa TB sugu ilipungua kwa asilimia 15%, kutoka watu 177, 000 mwaka 2019 hadi 150 000 mwaka  2020, sawa na mtu 1 katikaya  3 ya wale wanaohitaji matibabu. 

Uwekezaji kupambana na TB ulipungua 

Kwa mujibu wa ripoti ufadhili katika nchi za kipato cha chini na cha kati (LMICs) ambazo zinachangia asilimia 98% ya visa vya TB vilivyoripotiwa bado ni changamoto.  

Kati ya fedha zote zilizopatikana mwaka 2020, asilimia 81% ilitoka kwa vyanzo vya ndani, na nchi za BRICS (Brazil, Shirikisho la Urusi, India, China na Afrika Kusini) ukiwa ni asilimia 65% ya jumla ya ufadhili wa ndani. 

Mfadhili mkubwa zaidi ni serikali ya Marekani huku mfadhili mkuu wa kimataifa ni mfuko wa kimataifa wa kupambana na UKIMWI, kifua kikuu na malaria. 

Ripoti hiyo inabainisha kuwa kimataifa matumizi ya huduma za uchunguzi, matibabu na kinga ya kifua Kikuu, yalipungua  kutoka dola za Kimarekani bilioni 5.8 hadi dola za Kimarekani bilioni 5.3, ambapo ni chini ya nusu ya lengo la kimataifa la kufadhili kikamilifu hatua za kupambana na kifua kikuu la dola bilioni 13 kila mwaka hadi ifikapo 2022. 

Wakati huo huo, ingawa kuna maendeleo katika uchunguzi mpya wa kifua kikuu, dawa na chanjo, hii inaathiriwa na kiwango cha jumla cha uwekezaji wa R&D, ambapo kwa dola bilioni 0.9  mwaka 2019 hazifikii lengo la kimataifa la dola bilioni 2 kwa mwaka. 

Mashine kwa udhamini wa Global Fund ili kupambana na VVU, Kifua Kikuu na Malaria inawasaidia maafisa wa afya wa gereza la Pollsmoor Afrika Kusini kuwapima na kuwatibu wafungwa
Photo: The Global Fund/John Rae
Mashine kwa udhamini wa Global Fund ili kupambana na VVU, Kifua Kikuu na Malaria inawasaidia maafisa wa afya wa gereza la Pollsmoor Afrika Kusini kuwapima na kuwatibu wafungwa

Lengo la kutokomeza TB linakwenda mrama 

Ripoti inasema kubadilika kwa mwelekeo wa hatua zilizopigwa inamaanisha lengo la kimataifa la kutokomeza TB linakwenda mrama na kuonekana kuwa mbali sana kufikiwa ingawa kuna baadhi ya mafanikio yaliyopatikana. 

Ripoti iansema kimataifa idfadi ya vifo bvya TB kati yam waka 2015-2020 ilikuwa asilimia 9.2 ikilinganishwa na asilimia 35 mwaka 2020. 

Pia kimataifa idadi ya watu wanaougua TB kila mwaka ilipungua kwa asilimia 11 kutoka mwaka 2015-2020. 

Ukanda wa WHO wa Ulaya ulizidi malengo yam waka 2020 kwa kupungua kwa asilimia 25, Ukanda wa Afrika nao ulijitahidi karibu ufikie lengo kwa kupungua kwa asilimia 19. 

"Tumebakiza mwaka mmoja tu kufikia malengo ya kihistoria ya kifua kikuu ya 2022 yaliyofwekwa na wakuu wa nchi katika mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kifua kikuu. Ripoti hiyo inatoa habari muhimu na ukumbusho wenye nguvu kwa nchi kuharakisha hatua zao dhidi ya kifua kikuu na kuokoa maisha. Hii itakuwa muhimu wakati maandalizi ya mkutano wa 2 wa kngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kifua kikuu uliopangwa kufanyika mwaka 2023 ukikaribia."amesema Dkt. Tereza Kasaeva, mkurugenzi wa Programu ya kimataifa ya TB ya WHO.  

Chanjo ya BCG ambayo hutumiwa dhidi ya Kifua Kikuu ikiwa inaandaliwa katika kituo cha afya Bougouni, Mali 2018.
© UNICEF/Ilvy Njiokiktjien
Chanjo ya BCG ambayo hutumiwa dhidi ya Kifua Kikuu ikiwa inaandaliwa katika kituo cha afya Bougouni, Mali 2018.

Wito maalum 

 Ripoti hiyo inazitaka nchi kuweka hatua za haraka za kurejesha upatikanaji wa huduma muhimu za kifua kikuu.  

Inataka uwekezaji maradufu katika utafiti wa TB na uvumbuzi pamoja na hatua za pamoja katika sekta ya afya na zingine kushughulikia viashiria vya athari za  kijamii, mazingira na uchumi zitokanazo na TB. 

Ripoti hiyo mpya ina takwimu za mwenendo wa ugonjwa na hatua zinazochukuliwa kudhibiti janga hilo hilo kutoka nchi na maeneo 197, zikiwemo nchi 182 wanachama wa WHO.