Nguvu ya mtoto wa kike inasaidia kupunguza pengo la usawa wa kidijitali mtandaoni:UN

11 Oktoba 2021

Pengo la kijinsia duniani kulingana na utumiaji wa mtandao linaendelea kuongezeka, lakini kuanzia Syria hadi Costa Rica, wasichana wanazidi kupambana kujaribu kupunguza pengo hilo. 

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa pengo la kijinsia kwa watumiaji wa mtandao limeongezeka kutoka asilimia 11 mwaka 2013 hadi asilimia 17 mwaka 2019, na katika nchi zilizoendelea duniani, linafikia asilimia 43.

Mwaka huu, katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya mtoto wa kike, inayofanyika leo Oktoba 11, Umoja wa Mataifa unaonyesha jinsi janga la COVID-19 lilivyoongeza matumizi ya majukwaa ya kidijitali, lakini pia limeanika ukweli wa utofauti wa wasichana na wengine linapokuja suala la kuingia mtandaoni. 

Hapo chini, unaweza kusoma hadithi kutoka UN, ikiwa na wasichana watano kutoka nchi tano tofauti, wanavyotumia teknolojia ili kujenga maisha bora ya baadaye. 

Wajibu wetu 

Katika ujumbe wake kwa siku hii ya mtoto wa kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa wasichana hawa na wengine wote "ni sehemu ya kizazi cha kidijitali. Ni jukumu letu kuungana nao katika utofauti wao wote, kuongeza nguvu na suluhisho zao kama waleta mabadiliko ya kidijitali, na kushughulikia vizuizi vinavyowakabili katika nafasi ya kidijitali.” 

Ameongeza kuwa njia ya kuelekea usawa wa kidijitali kwa wasichana ni ngumu. Zaidi ya theluthi mbili ya nchi zote, wasichana ni asilimia 15 tu ya wahitimu wa masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hesabu, yanaojulikana kwa kifupi, kama STEM. 

Guterres amesema katika nchi zenye kipato cha kati na cha juu, ni asilimia 14 tu ya wasichana ambao walikuwa wanafanya vizuri katika masomo ya sayansi au hisabati walitarajiwa kufanya kazi katika sayansi na uhandisi, ikilinganishwa na asilimia 26 ya wavulana waliofanya vizuri. 

"Wasichana wana uwezo sawa na uwezo mkubwa katika nyanja hizi, na tunapowawezesha, kila mtu hufaidika," Bwana Guterres alisema. 

Amekumbusha kuliona hili muda mrefu kabla ya kuanza kazi yake ya kisiasa, wakati alikuwa mwalimu huko Lisbon, Ureno, na "alishuhudia nguvu ya elimu katika kuinua watu na jamii." 

"Uzoefu huo umeongoza maono yangu ya usawa wa kijinsia katika elimu tangu wakati huo. Uwekezaji katika kuziba pengo la kijinsia la kidijitali huleta mafanikio makubwa kwa wote." 

Katika suala hili, Umoja wa Mataifa una jukwaa jipya, linaloitwa muungano wa utekelezaji wa usawa wa kizazi cha teknolojia na ubunifu, ambapo serikali, asasi za kiraia, sekta binafsi na viongozi vijana, wanakuja pamoja kusaidia ufikiaji wa kidijitali wa wasichana, ujuzi na ubunifu. 

"Umoja wa Mataifa umejitolea kufanya kazi na wasichana ili kizazi hiki, popote kitakapokuwa na katika hali zao zote, kiweze kufikia uwezo wao", amesema Bwana Guterres  

Kundi la wasichana wa Namibia ambao walishiriki katika kambi ya mafunzo ya programu za Kompyuta (AGCC) mjini Pretoria, Afrika Kusini.
UN Namibia
Kundi la wasichana wa Namibia ambao walishiriki katika kambi ya mafunzo ya programu za Kompyuta (AGCC) mjini Pretoria, Afrika Kusini.

Taswira kutoka kote ulimwenguni 

Ili kusherehekea siku ya kimataifa ya mtoto wa kike, Umoja wa Mataifa unatoa shukrani kwa wasichana wanaotumia ujuzi wao wa teknolojia ya kidijitali kama ufunguo wa kufungua milango mipya. Hizi ni baadhi ya hadithi zao: 

1.Kuwawezesha vijana wa Syria kufanya kazi bora 

Wakati Madeleine alikuja Damascus miaka minne iliyopita kutekeleza ndoto yake ya utotoni ya kusoma uhandisi wa mawasiliano ya simu, alikuwa amejawa na matamanio. 
Ingawa kifo cha kushangaza cha baba yake katika mwaka wake wa kwanza wa masomo kilimlemea, alikumbuka jinsi alivyomthamini yeye na elimu ya ndugu zake, na hii ilimfanya afanye kazi kwa nguvu zaidi. 

Sasa, Madeleine ni mmoja wa vijana 60 wanaoshiriki kozi inayoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika matengenezo ya mitandao ya kompyuta. 

2. Nchini Sri Lanka, kujenga ujasiri kwa wasichana ni changamoto yah atua kwa hatua  

Kwa wasichana waliokwama nyumbani, mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO wa kushinda tuzo huko Sri Lanka wa NextGen Girls in Technology, husaidia wasichana kugundua mapenzi yao kwa ustadi wa kidijitali , pamoja na mtandao wa vitu (IoT) na programu. 

Tangu janga la COVID-19 lianze, kozi katika mpango huo zimefikia karibu wanafunzi 2,500 wa kiwango cha hule za msingi na sekondari, na zaidi ya walimu 500. 

Diyathma wa miaka 14 kutoka Maharagma ni mmoja wao. Ameshinda mashindano ya coding ya hackathon kwa kikundi cha umri wake. 

3. Kuziba pengo la kidijitali na ajira nchini Cameroon 

Happi Tientcheu mwenye umri wa miaka 12 hivi karibuni alishiriki katika kambi coding ya kuwaunganisha wasichana wa Kiafrika.  

Yeye na kikundi chake, hatari, waliunda mfumo wa mwelekeo wa wasichana, ambalo ni jukwaa la uhuishaji mtandaoni ambalo husaidia wasichana na wanawake wachanga kupata fursa za kazi za ICT. 

Kwa jumla, uvumbuzi aina 70 uliibuka kwenye kambi hiyo na kuweka alama, ambayo ilikusanya wasichana na wanawake wa Kiafrika 8,500 kutoka bara lote nchini Cameroon, na pia kupitia mtandaoni 

4. Kuvunja mwiko Tajikistan 

Nurjan Tolibova, mtunzi mwenye umri wa miaka 17 kutoka Dushanbe, alijiunga na PeshSaf, mradi ulio chini ya maabara ya ubunifu wa vijana (YIL), ili kuboresha ustadi wake wa uandishi na ufundi wa teknolojia Nujran. 
Ingawa anakubali kuwa maoni potofu ya kijinsia bado yanaathiri wanawake katika nyanja zisizo za jadi, kama STEM, Nurjan anawahimiza sana wasichana kote dunianii kutekeleza ndoto zao. 

"Usiogope kusoma teknolojia, bila kujali maoni ya jumla ya jinsi waandaaji wa programu wanapaswa kuonekana kama ikiwa ni kitu ambacho unapenda, fanya", amesisitiza. 

5. Wasichana na pengo la kidijitali Costa Rica 

Kwa Kattia mwenye umri wa miaka  17, kuishi katika eneo la mbali la Costa Rica kunamaanisha hakuna muunganisho wa mtandao. Ili kupata habari na mawasiliano, ilibidi asafiri kutoka nyumbani kwake na simu ya rununu ya familia yake, ili kupata mahali penye network ya kutosha kuweza kufanya kazi zake za shule. 

Mwanzoni mwa mwaka wa 2021, kama sehemu ya mradi unaoungwa mkono na UNICEF na Serikali, Kattia alipokea kompyuta yake ya kwanza na ufikiaji wa mtandao. 

"Hii ni kompyuta ya kwanza ambayo tumewahi kuwa nayo nyumbani kwangu. Na ni raha, ni nzuri sana, kwa sababu pamoja na kuwa mzuri sana, ni ya kugusa tu. Ninaweza kuitumia kuchora. Itasaidia sana, kwa sababu baada ya kuhitimu, nina mpango wa kusoma muundo wa picha, "amesema Kattia." Teknolojia ni muhimu kwangu. 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter