Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika siku ya ndege kuhama ,Imba, ruka na paa kama ndege ili kuwalinda :UN

Ndege wahamiaji wakiwa katika safari zao kuelekea kusini.
Picha ya WMB
Ndege wahamiaji wakiwa katika safari zao kuelekea kusini.

Katika siku ya ndege kuhama ,Imba, ruka na paa kama ndege ili kuwalinda :UN

Tabianchi na mazingira

Leo ni siku ya ndege wanaohama duniani kaulimbiu mwaka huu ikiwa “Imba, ruka nap aa kama ndege” ambapo watu wote duniani wanaisherehekea kwa kampeni kubwa ya kimataifa yenye lengo la kuelimisha kuhusu Ndege wanaohama na haja ya ushirikiano wa kimataifa kuwalinda.

Maadhimisho yam waka huu yamekuja siku chache kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa bayoanuwai utakaoanza wiki ijayo Kunning China.

Kampeni maalum ya uelimishaji inaunga mkono na Umoja wa Mataifa na imeandaliwa kwa ushirikiano na vyombo viwili vinayohusiana na mikataba hya mazingira ambayo ni mkataba kuhusu uhifadhi wa viumbe wanaohamahama na wanyamapori (CMS) na makubaliano ya Afrika, Ulaya na asia ya aina za ndege maji wanaohamahama (AEWA) wakilihusisha shirika la kujitolea la mazingira kwa ajili ya nchi za Amerika (EFTA)

Kaulimbiu yam waka huu “Ibamba, ruka nap aa kama Ndege” inajikita katika “Ndege kuimba na Ndege kuruka”  kama njia ya kuchagiza na kuunganisha watu wa rika zote kote duniani katika dhamira yao ya pamoja ya kuwalinda na kuwasherehekea Ndege wanaohamahama.

Mali na matukio mbalimbali yanayofanyika kuadhimisha siku hii watu pia watatumia ubunifu na lugha ya kimataifa ya uimbaji na kucheza kuelezea na kuonyesha wanavyowathamini ndege kupitia mitandao ya kijamii.

Flamingo wawili wadogo katika ziwa Nur-Sultan kwenye mji mkuu wa Kazakhstan
UN News/Kulpash Konyrova
Flamingo wawili wadogo katika ziwa Nur-Sultan kwenye mji mkuu wa Kazakhstan

Akizungumzia siku hii mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP Inger Andersen amesema “Ndege wanaohama wanashuhudia na wanaathiriwamara tatu na mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi, upotezaji wa bioanuwai na uchafuzi wa mazingira. Kupiga hatua katika mabadiliko ya tabianchi na kumaliza upotezaji wa bioanuwai ni muhimu kwa uhai wa ndege wanaohama. Safari ya ndege anayehama hajui mipaka na kwa hivyo, pia hatua zetu za kupambana na mgogoro unaoikabili sayari yetu hazipaswi kuwa na mipaka. Natoa wito kwa sisi wote kuongeza hatua, na hatua za kulinda mustakabali wa viumbe vyote katika sayari hii. "

Mabadiliko ya tabianchi yanaongeza shinikizo zaidi kwa ndege wanaohama kwa kuathiri vibaya makazi wanayohitaji kwa kuzaliana, kupumzika na kuongeza mafuta njiani. 

Ndege wa Arctic msimu wa joto wa kaskazini kati ya kaskazini mwa Ufaransa, Iceland na Greenland.
Jakub Fryš
Ndege wa Arctic msimu wa joto wa kaskazini kati ya kaskazini mwa Ufaransa, Iceland na Greenland.

UNEP inasema mabadiliko ya tabianchi pia yanaathiri mizunguko ya ndege ya kila mwaka, na kuathiri wakati wa uhamiaji na kuzaa na kusababisha usawa katika upatikanaji wa chakula.

 Tishio jingine linaloibuka kwa ndege wanaohama kwa mujibu wa UNEP ni uchafuzi wa hewa, ambao huwachanganya ndege ambao wanaruka usiku, unawasababishia kugongana na majengo hali inayoweza kuwasababishia vifo vya ndege wengi mfano mamia ya ndege wanaohama huko mjini New York mwezi uliopita.

Takriban aina 2000 kati ya aina 11,000 za ndege huhama, wengine huenda umbali mrefu, kama Arctic Tern au Bar-tailed Godwit, ambako huruka umbali hadi kilomita 11,680 bila kusimama kati ya Alaska na New Zealand.

Siku ya ndege wanaohama duniani huadhimishwa kwa siku mbili za kilele cha kuhama kila mwaka (Jumamosi ya pili ya mwezi Mei na mwezi Oktoba) kwa kutambua hali ya mzunguko wa uhamiaji wa ndege na nyakati tofauti tofauti za uhamiaji sanjari na safari za ulimwengu.