Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres aangazia nguvu ya 'sauti za vijana' kabla ya mkutano muhimu wa biashara na maendeleo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kushoto) akikutana na Mia Mottley, Waziri Mkuu wa Barbados.
Umoja wa Mataifa Barbados na Karibea Mashariki/Bajanpro
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kushoto) akikutana na Mia Mottley, Waziri Mkuu wa Barbados.

Guterres aangazia nguvu ya 'sauti za vijana' kabla ya mkutano muhimu wa biashara na maendeleo

Ukuaji wa Kiuchumi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres Jumapili hii akiwa ziarani nchini Barbados amesema amejitolea kuhakikisha kuwa Umoja wa Mataifa ni mahali ambapo "sauti za vijana zinasikika, na maoni yao yanaongoza.".

Bwana Guterres amewasili katika nchi hiyo iliyoko katika kisiwa cha Karibea Jumamosi na atakuwa akihutubia mkutano wa mesto (ana kwa ana na mtandaoni) wa UNCTAD15 ambao unaanza Jumatatu hii, ukiwa na kaulimbiu, Kutoka kwenye ukosefu wa usawa na udhaifu, kwenda mafanikio kwa wote.

Jumatatu hii Barbados itakuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa UNCTAD, mkutano naolenga hitaji la kujenga uchumi wa kijani duniani na kupona kwa usawa kutoka kwa janga la COVID-19.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta atatoa hotuba ya ufunguzi kwa njia ya mtandao akifuatiwa na mwenyeji wa mkutano huo Waziri Mkuu wa Barbados Mia Mottley na kisha Katibu Mkuu wa UNCTAD, Rebeca Grynspan.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, katika hotuba yake, Bwana Guterres anatarajiwa kusisitiza changamoto za kukabiliana na changamoto za deni na hitaji la kupata nafuu endelevu na sawa kwa wote.

Tweet URL


"Anatarajiwa pia kuonesha hitaji la kuwasha tena injini za biashara na uwekezaji, na kuhakikisha zinanufaisha nchi mas.kini, pamoja na hitaji la kujenga uchumi wa kijani duniani." Alieleza msemaji  Farhan Haq Ijumaa alipoongea na waandishi wa habari jijini New York Marekani.


Linda walio hatarini zaidi


Kupitia mtandao wa tweeter Jumapili hii, baada ya kukutana na Waziri Mkuu Mottley ambaye atahudumu kama Rais wa mkutano huo wa UNCTAD15, Katibu Mkuu Guterres amekumbusha kwamba katika hotuba yenye nguvu kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita, alikuwa ameangazia umuhimu wa kuwekeza katika kulinda walio hatarini zaidi Dunia; "kipaumbele kwa taifa hili la kisiwa, na moja nitakaloendelea kushinikiza", ameongeza Bwana Guterres.


Bwana Guterrres ameitumia siku hii kukutana na maafisa wa Serikali na alitakiwa kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na mabadiliko ya hali ya tabianchi katika Barbados, ili kujionea athari za mmomonyoko na uharibifu wa ardhi. Alitarajiwa pia kutembelea jamii inayopona kutokana na kupita kwa Kimbunga Elsa, kilichotokea mnamo Julai 2 mwaka huu, kama kimbunga cha kwanza cha msimu wa Atlantiki ya 2021.


Pamoja na kukutana na waziri M. Mottley, Katibu Mkuu pia amekutana na kile alichokielezea kwenye mtandao wa Twitter kama "kundi chenye nguvu" cha vijana wa Barbados, "wakifanyia kazi masuluhisho ya kibunifu kwa changamoto kubwa ulimwenguni  kuanzia kwa hatua ya hali ya mabadiliko ya tabianchi, hadi kupona kutoka ugonjwa wa COVID-19."