Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanya wa kuepuka zahma ya mabadiliko ya tabianchi unaziba haraka:Guterres

Ukame unaoendelea kwa kasi nchini Somalia umesababisha watu kuhama - kudhoofisha usalama wa chakula na kuwaacha wanawake katika hatari ya unyonyaji wa kijinsia.
IOM/Celeste Hibbert
Ukame unaoendelea kwa kasi nchini Somalia umesababisha watu kuhama - kudhoofisha usalama wa chakula na kuwaacha wanawake katika hatari ya unyonyaji wa kijinsia.

Mwanya wa kuepuka zahma ya mabadiliko ya tabianchi unaziba haraka:Guterres

Tabianchi na mazingira

Hakuna eneo ambalo lina kinga dhidi ya majanga ya mabadiliko ya tabianchi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameliambia Baraza la Usalama leo Alhamisi, akionya kuwa "fursa yetu ya kuzuia athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi inafunga haraka". 

Akizungumza kwenye kikao maalum cha Baraza la Usalama kandoni na mjadala wa Batraza Kuu kinachoatathimini mabadiliko ya tabianchi na usalama Katibu Mkuu “ameangazia ripoti ya kutisha sana ya jopo la serikali kuhusu mabadiliko ya tabianchi (IPCC) iliyotolewa mwezi uliopita, na kusema kwamba "hatua kali zaidi dhidi ya mabadiliko ya tabianchi zinahitajika ili kudumisha amani na usalama wa kimataifa.” 

Ameyahimiza mataifa yaliyoendelea kiviwanda ya G20 kujitokeza na kuchukua hatua kabla ya mkutano wa mabadiliko ya tabianchi Umoja wa Mataifa (COP26) utakaofanyika mapema Novemba mwaka huu. 

Vichocheo vya hatari 

Katibu Mkuu amesema “kinyume na kuongezeka kwa moto wa nyika, mafuriko, ukame na matukio mengine mbaya ya mabadiliko ya tabianchi, hakuna nchi ambayo ina kinga . Changamoto ya mabadiliko ya tabianchi ni kubwa sana na imechanganywa na hali tete na mizozo.” 

Amelezea mabadiliko ya tabianchi na usimamizi mbaya wa mazingira kama vichocheo vya hatari, akisema kuwa mwaka jana, majanga yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi yalisababisha zaidi ya watu milioni 30 kufungasha virago na kuhama makwao na kwamba asilimia 90 ya wakimbizi wanatoka nchi ambazo haziwezi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. 

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa wengi wa wakimbizi hawa wamekaribishwa na mataifa ambayo pia yanayopata athari za mabadiliko yatabianchi, ikiwa ni pamoja na changamoto kwa jamii zinazowakaribisha na bajeti za kitaifa na janga la COVID-19 pia linadhoofisha zaidi uweze wa serikali kukabiliana na majanga ya mabadiliko ya tabianchi na kujenga mnepo. 

Kutanguliza vitendo 

Bwana Guterres katika hotuba yake amesema “Dunia bado haijachelewa kuchukua hatua", akiangazia vipaumbele vitatu, akianza na kupunguza joto duniani na kufikia nyuzi joto 1.5 za Celsius. 

Ili kuepusha athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi, amehimiza nchi wanachama wote kuongeza michango yao iliyoamua kitaifa (NDCs)  mipango ambayo nchi zinajitolea kuchukua hatua kubwa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kabla ya COP26 na kutafsiri ahadi hizo kuwa "hatua madhubuti na za haraka". 

Amesema "Kwa pamoja, tunahitaji kupunguzwa kwa asilimia 45 katika uzalishaji wa dunia wa hewa chafuzi ifikapo mwaka 2030". 

Nusu iliyosahaulika 

Katibu Mkuu amekumbusha kuwa ili kushughulikia athari mbaya za usumbufu wa mabadiliko ya tabianchi kunahitajika uwezo wa kuyakabili na mnepo, ambayo amesisitiza yanahitajika kuweza  kutoa angalau nusu ya fedha zinazohitajika kukabiliana na mabaduiliko ya tabianchi duniani na kujenga mnepo na kusaidia marekebisho. 

"Hatuwezi kufikia malengo yetu ya pamoja dhidi ya bmabadiliko ya tabianchi wala kufikia matumaini ya amani na usalama wa kudumu ikiwa uhimili na mnepo ambavyo ni nusu ya mahitaji vinaendelea kusahaulika katika suala la mabadiliko ya tabianchi. “ 

Kuimarisha pande zote 

 “Marekebisho ya maabadiliko ya tabianchi na ujenzi wa amani vinaweza na vinapaswa kuimarishana", amesema Guterres akiangazia miradi ya mpakani mwa Afrika Magharibi na Kati ambayo "imewezesha mazungumzo na kukuza usimamizi wa uwazi zaidi wa maliasili adimu". 

Na akabainisha kuwa "wanawake na wasichana wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi kutokana na mabadiliko ya tabianchi na mizozo", pia amesisitiza umuhimu wa "ushiriki wao wa maana na uongozi kuleta matokeo endelevu ambayo yanafaidi watu wengi". 
Umoja wa Mataifa unajumuisha hatari za mabadiliko ya tabianchi katika kuzuia mizozo, mipango ya ujenzi wa amani na uchambuzi wake wa kisiasa, Katibu Mkuu amelezea. 

Ameongeza kuwa "Mfumo wa usalama dhidi ya mabadiliko ya tabianchi unasaidia ujumbe timu za nchi na mashirika ya kikanda na ya kieneo na kazi inapata mvuto katika nchi na maeneo ambayo Baraza la Usalama limetambua kuwa mabadiliko ya tabianchi na ikolojia yanadhoofisha utulivu”. 

Ukame wa mara kwa mara na ushindani unaotokana na rasilimali umesababisha mzozo nchini Somalia katika miongo ya hivi karibuni.
undp Somalia
Ukame wa mara kwa mara na ushindani unaotokana na rasilimali umesababisha mzozo nchini Somalia katika miongo ya hivi karibuni.

Sote tunawajibika 

Akikiri kwamba asilimia 80 ya uzalishaji wa hewa ukaa wa Umoja wa Mataifa yenyewe unatoka kwa shughuli zake sita kubwa za kulinda amani, Bwana Guterres amesema shirika linapaswa kufanya vizuri zaidi. 

Amehakikishia kuwa Umoja wa Mataifa unafanya kazi katika njia mpya za kuhamia kwenye uzalishaji wa nishati mbadala, ambao utaenda mbali zaidi ya ujumbe wetu. 

“Sisi sote ni sehemu ya suluhisho. Wote tushirikiane kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi iyanayotusambaratisha ili kujenga jamii zenye amani na utulivu”, amehitimisha Katibu Mkuu. 

Ni wakati wa kutenda 

Akiongoza mkutano huo, waziri mkuu wa Ireland, Micheál Martin amesisitiza umuhimu kwa chombo hicho chenye wanachama 15 kuchukua jukumu kubwa katika upimaji wa mabadiliko ya tabianchi na upunguzaji, pamoja na kupitia shughuli za kulinda amani na mamlaka zake. 

"Watu walioathiriwa na mizozo inayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi wanategemea Baraza hili kwa uongozi", amesema. "Sasa ni wakati wa Baraza kuchukua hatua".